Viwavi jeshi ni nini?

Viwavi jeshi ni larva katika hatua ya ukuaji wa vipepeo (wanaoruka usiku – moths) ambao hushambulia mimea na mazao ya aina mbalimbali na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima. Viwavijeshi vamizi (Spodoptera frugiperda) wana asili ya maeneo ya kitropiki ya Amerika (Argentina na maeneo ya Caribbean). 

kipepeo wa kiwavi jeshi
kipepeo (moth) wa kiwavi jeshi

Waligundulika Afrika kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na walianza kuonekana mwanzo katika nchi za Benin, Nigeria, Sao Tome and Principe, na Togo. (FAO)

Mpaka January 30 ya mwaka 2018, Viwavijeshi vamizi walikuwa wameshagundulika na kutolewa taarifa kutka katika karibu nchi zote za kusini mwa Jangwa la Sahara isipokuwa katika nchi za Djibouti, Eritrea na Lesotho. (FAO)

Kwa mara ya kwanza walionekana Tanzania mwaka 2017 katika wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa. Mpaka sasa viwavijeshi vamizi wamefika zaidi ya mikoa 15 ya Tanzania.  

Viwavi jeshi wapo wa aina mbili: Viwavijeshi vamizi (Fall ArmyWorm) ambao kitaalam wanaitwa Spodoptera frugiperda. Na Viwavijeshi wa afrika (African Armyworm) ambao nao kitaalam wanitwa Spodoptera exempta. Viwavijeshi hawa wote ni waharibifu kwa mimea na mazao, isipokuwa wanatofautiana katika asili zao, na baadhi ya tabia za ulaji.

Viwavi jeshi hushambulia aina za mimea/mazao zaidi ya 80. Hupendelea zaidi mimea jamii ya nafaka kama mahindi, mtama, uwele, mpunga, shayiri, ngano na miwa na mazao ya mbogamboga.

Kwa mwaka huu wa 2019 viwavijeshi vamizi vimeripotiwa kuonekana katika maeneo ya Mtibwa na Dizungu (Turiani) mkoa wa Morogoro. Kwa kuwa wadudu hawa husambaa kwa kasi sana, ni vyema wakulima wa maeneo ya karibu kuchukua tahadhari. (Picha hizi hapa chini)

Katika Makala hii, tutamzungumzia zaidi viwavi jeshi aina ya Fall ArmyWorm (Spodoptera frugiperda). Ambapo utajifunza jinsi ya kuwatambua, mzunguko wao wa maisha, athari zao kwenye mazao na namna ya kuwadhibiti.Mzunguko Wa Maisha Ya Viwavi Jeshi Vamizi

Kipepeo wa Viwavijeshi hutaga mayai mengi ambayo huanguliwa baada ya siku 3-5, baada ya mayai kuanguliwa kiluilui (kiwavi) hutokea ambacho huishi kwa muda wa siku 14-28. Kutoka katika hatua ya kiwavi, buu hutokea ambapo nae hudumu kwa muda wa siku 7-14. Kutoka katika hatua ya buu ndipo kipepeo kamili hutokea na anaweza kuishi kwa wastani wa siku 14.

 • Kipepeo huruka hadi kilomita 100 kwa siku hivyo huweza kuruka kilomita 2000 katika maisha yake yote
 • Kipepeo jike huweza kutaga mayai mpaka 2000 katika maisha yake
 • Kiluilui (larva) ndicho hushambulia mimea na huishi kwa siku 14-28
 • Kipepeo wa kiwavijeshi huweza kuwa na vizazi 6-12 kwa msimu
alama ya Y kwenye kiwavijeshi
Alama ya “Y” kwenye kichwa cha kiwavi jeshi

Namna Ya Kuwatambua Viwavi jeshi

Viwavijeshi huweza kutambulika kwa sifa zifuatazo:-

 1. Mayai hutagwa kwa mafungu (cluster) ya 100-300
 2. Mayai hufichwa kwa utando mweupe kama pamba
 3. Mayai hutagwa chini ya jani la mmea
 4. Yai huanguliwa baada ya siku 3-5
 5. Vipepeo wao hutokeza na kuruka wakati wa usiku tu
 6. Mabawa ya kipepeo dume huwa na alama ya pembe tatu nyeupe kona ya pembeni na katikati
 7. Mabawa ya kipepeo jike ni rangi ya kahawia yote na mabakamabaka
 8. Kiwavi huwa na alama ya “Y” kichwani
 9. Kiwavi huwa na doti nne za umbo la mraba katika pingiri ya nane kutoka kichwani
Mayai ya kipepeo wa viwavijeshi
Mayai ya kipepeo wa viwavi jeshi


Dalili Za Mashambulizi Ya Viwavi jeshi     

Mashambulizi ya viwavijeshi hutambulika kupitia hatua za ukuaji wa wadudu hawa. Zifuatazo ni hatua za mashambulizi:-

 • Hatua ya kwanza: Kiluilui hula upande mmoja wa jani
 • Hatua ya pili na tatu: Huweka mashimo kwenye majani
 • Hatua ya nne hadi sita: kiluilui hufanya makubwa jani (??)
 • Mara nyingine hutoboa toto la muhindi, hushambulia punje, huweza kujificha kwenye bua la muhindi pia hushambulia mbelewele. 

Madhara Ya Viwavijeshi Kwa Mimea

 1. Hushambulia majani na kuufanya mmea kushindwa kukua vizuri
 2. Hushambulia shina na kuufanya mmea kuanguka na kufa
 3. Matumizi ya viuatilifu kuwadhibiti husababisha madhara kiafya kwa mlaji kupitia mazao ya mimea (Phytotoxicity)
 4. Hushambulia mbelewele na kusababisha hali duni ya uchavushaji
 5. Hushambulia punje na kusababisha mavuno duni pia kupunguza ubora wa mavuno.
Muhindi ulioshambuliwa na viwavi jeshi

Madhara Ya Viwavi jeshi Kiuchumi

Uvamizi wa wadudu hawa husababisha madhara makubwa kiuchumi kwa jamii na taifa kwa ujumla, baadhi ya madhara hayo ni:

 • Huongeza gharama za uzalishaji kwa kwa kununua viuatilifu vya kuwadhibiti
 • Huweza kushambulia shamba zima na kumfanya mkulima kupanda upya
 • Serikali huweza kutumia bajeti kubwa katika mipango ya kudhibiti visumbufu hivi
 • Huweza kusababisha njaa na hatimaye umaskini kwa wakulima na pengine taifa kwa ujumla
 • Matumizi ya viuatilifu kudhibiti wadudu hawa husababisha uharibifu wa mazingira ambao hupelekea gharama nyingine kutunza mazingira hayo

Soma:


Viuatilifu Vilivyosajiliwa Nchini Tanzania na kuthibitika Kuua Viwavi jeshi Vamizi

Hivi hapa ni viuatilifu vilivyothibitika kuua  wadudu hawa vikitumika kwa usahihi:-

Abamectin, cypermethrin, lamda-cyhalothrin, chlorpyrifos 480g/l, emamectin beanzoate 50g/l, pirimiphos methyl and deltametrin, acetamiprid, chlorantraniliprole…

Na Methomyl (carbamate) 900g/kg, lufenuron (benzamide) 50g/l, flubendiamide (belt 480 sc), indoxacarb, methomyl, baccilus thuringiensis, meterihzium anisoplie, lennate, spinosad.


Wakati Sahihi Wa Kutumia Viuatilifu Kwa Viwavi jeshi

Viwavijeshi huzuilika endapo tu viuatilifu vitatumika kwa usahihi na kwa wakati sahihi. Wakati wa kutumia viuatilifu zingatia yafuatayo:-

 1. Tumia kiuatilifu kilichosajiliwa na TPRI
 2. Weka mchanganyiko sahihi wa maji na viuatilifu (soma kibandiko au muulize afisa ugani wa eneo lako)
 3. Dhibiti viluilui wakati bado vidogo mapema kabla havijajificha
 4. Epuka kuchanganya viuatilifu zaidi ya kimoja kwenye pampu moja
 5. Tumia vifaa kinga unyunyiziapo

Soma hapa ujue maana na matumizi sahihi ya viuatilifu.


Ushauri: Tembelea shamba lako mara kwa mara ili kutambua uwepo au kuona hali ya uvamizi na kuchukua hatua stahiki.

Kwa mwaka huu; umeona viwavijeshi shambani kwako au mahali pengine popote pale? Tafadhali tuambie kwenye comment umewaona wapi viwavijeshi na lini, iwe ni kwa mwaka huu tu!


Usiache kusoma makala hizi muhimu:

0 0 vote
Article Rating

Mtalula Mohamed

I like blogging. In order utilize my profession I chose to share, to blog, a few tips and tricks about farming and agriculture to anyone interested.

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
njau
njau
1 year ago

nimewaona na wameshambulia mahindi yangu maeneo ya Wazo Dar

Mohamed Mtalula
Mohamed Mtalula
Reply to  njau
1 year ago

Pole sana Njau. Umeweza kuwadhibiti?

Ester
Ester
3 months ago

Nimeipenda blog yenu, inahabarisha vyema

error: Content is protected !!
4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x

Join Our Farming Community