The Story
Kilimo ni sayansi. Hata hivyo Kilimo kimeanza kufanywa siku nyingi hata kabla ya kugunduliwa kwa sayansi yenyewe.
Hii ina maana gani? Maana yake ni kwamba licha ya kuwepo sayansi ya kilimo, kuna wakulima ambao tayari wanalima na wana uzoefu mkubwa tu kwenye kilimo na hawana habari kabisa kuhusu huo utaalam. Hali hii imezaa vita kati ya UTAALAM [kanuni za kilimo bora] na MAZOEA [uzoefu].
Kati ya 80% ya watanzania wote waliojiajili kwenye sekta ya kilimo, inawezekana wanaolima kitaalam hawafiki hata asilimia 10. Hii inachagizwa na ukweli kwamba wakulima wengi hawajui hata uwepo wa maafisa ugani [wataalam wa kilimo] katika maeneo yao kitu ambacho kinawakosesha maarifa muhimu kuhusu kazi yao tukufu.
Uzoefu bila Maarifa:
Sio kila mkulima aliyekosa utaalam hajui kilimo, laa! Bali uzoefu ni hazina. Lakini tukiongezea maarifa [utaalam] kwenye uzoefu tutapata matokeo bora zaidi kwenye kilimo.
Na kwa sababu hiyo, sisi hatulengi kukosoa kila njia unayotumia kwenye kilimo chako na wala hatuna mbinu ya ajabu isiyojulikana. Lengo letu sisi ni kukuonesha mbinu sahihi, kukuongezea utaalam [maarifa] kwenye uzoefu ulionao ili ujifunze mbinu sahihi na uzitekeleze kwa mafanikio zaidi.
Lakini pia kwa maarifa hayo utazijua mbinu zisizofaa na tunategemea utaziacha ili upunguze hasara na uongeze tija zaidi kwenye kilimo chako.
Suluhisho:
Tunaandika masomo mbalimbali yakukusaidia kujifunza mbinu bora za kilimo. Tukachapisha vitabu kadha wa kadhalika kama njia mbadala ya wewe kujifunza, na zaidi ya hayo tunatoa nafasi ya kushauriana na wewe juu ya mambo mbalimbali yanayohusu kilimo. Ni juu yako kuamua njia bora ya kujifunza nasi.
Ukiwa tayari, utakuta tunakusubiri. Karibu sana.
About the author
Hi,
Naitwa Mohamed Mtalula
Mwanzilishi na Msimamizi mwendeshaji wa Mogriculture.com. Nina shahada ya Sayansi ya Kilimo kutoka SUA. Nilianzisha mtandao huu mwaka 2016 kwa lengo la kutatua kero za wakulima kama wewe.
Nimekuwa kwenye sekta ya kilimo tangu nilipomaliza elimu ya juu, kama mtaalam wa kilimo (Mtibwa Sugar Estates ltd - mpaka sasa) na mkulima kadhalika.