Acha kulima kwa hisia; soma, jifunze!
Unawezaje kuingia shambani bila kujua gharama utakazotumia au faida utakayopata? Ili kukuepusha na hasara za ‘sapraizi’, tumekuandalia miongozo ya kitaalamu ya mazao mbalimbali itakayokuongoza kwa kila hatua, kuanzia maandalizi ya shamba hadi kuvuna.
Miongozo ya kilimo biashara ni full package kwa mkulima makini. Vitabu hivi vina mbinu zote zitakazomuwezesha mkulima yeyote (hata asiye na uzaoefu) kupanga, kuanzisha na kusimamia uzalishaji wenye faida. Kila kitabu kimoja kinaeleza zao moja tu. Na vitabu vyote vipo katika mfumo wa softcopy (PDF).
Vitabu hivi vinadadavua kwa kina vipengele vyote muhimu katika uzalishaji wa mazao kama ifuatavyo:
- Mbinu bora za kuandaa shamba,
- Mapendekezo maalum (kutoka kwetu) ya aina na kiasi cha mbegu bora, mbolea na viuatilifu vinavyohitajika kwa ekari,
- Uchambuzi wa bajeti ya kilimo (gharama za uzalishaji katika kila hatua) kwa ekari 1, na
- Mbinu bora za vunaji, makadirio ya mavuno, na faida utakayopata.
Jinsi ya kupata vitabu vyetu
Bofya ukurasa huu, ili kuchagua na kulipia vitabu vyako. Utaratibu ni kama ifuatavyo;
- Bofya add to cart kwenye kila kitabu unachotaka.
- Chagua njia utakayotaka kulipia kama ni Mitandao ya simu au kwa kadi.
- Kwenye ukurasa huo huo weka namba yako ya simu utakayotumia kulipia, kisha andika jina lako na email yako.
- baada ya hapo bofya Pay ili kukamilisha malipo.
- Utatumiwa vitabu vyako kwenye email yako papo hapo.
