Utangulizi

Imekuwa kawaida kwa mkulima wa nyanya kuona matunda mengi shambani yameoza sehemu ya kitako ambacho huwa na ngozi ngumu yenye rangi nyeusi. Hali hii hutokea hasa hasa matunda yanapokuwa mabichi (yanayoendelea kukua) na hata yanapokuwa yameanza kuiva.

nyanya imeanza kuoza kitako
Nyanya imeanza kuoza kitako

Linapoanza tatizo la nyanya kuoza kitako, matunda hutengeneza malenge lenge ya maji (muozo) kwenye kitako ambapo kadri matunda yanapokuwa muozo nao huongezeka ukubwa na kitako hubadilika rangi na kuwa cheusi na baadae hukakamaa na kutengeneza ngozi ngumu nyeusi.

Muozo huu unaweza hata kuathiri nusu ya tunda zima kutokea chini. Na tatizo hili huweza pia kutokea kwenye mazao kama pilipili, matango, nyanya chungu, matikiti na maboga.

Tatizo la nyanya kuoza kitako si ugonjwa bali ni hali ya kifiziolojia inayosababishwa na ama kutokuwepo kwa madini ya chokaa (Calcium, Ca2+) kwenye udongo, au mimea kushindwa kufyonza madini ya chokaa (Calcium, Ca2+) kwenye udongo (kama yapo) au kutokuwepo kwa uwiano sawa wa madini ya chokaa (Calcium, Ca2+) katika sehemu mbalimbali za mmea hasa matunda.

Hivyo basi unatakiwa kuelewa kwamba tatizo hili halisambai kutoka shamba moja kwenda lingine, wala kutoka mmea mmoja kwenda mwingine, wala kutoka tunda moja kwenda jingine. Na hivyo basi hakuna dawa yoyote iwe ya wadudu au ya fangasi inayoweza kutibu tatizo hili.


Nyanya  zilizo athiriwa na tatizo la kuoza kitako

Nini hasa kazi ya Calcium (Ca2+) kwenye mmea?

Calcium ni kiungo (kirutubisho) muhimu katika kuta za seli za mmea, hivyo uwepo wake ni muhimu sana kwa ukuaji sahihi wa mmea. Na inapotokea inahitajika kwa wingi kuliko inavyopatikana mengi hutokea; matunda huoza (Mfano; nyanya kuoza kitako), mmea hudumaa, majani machanga hufa kwenye ncha na mizizi kushindwa kurefuka. (4)


Soma  zaidi kuhusu kilimo cha nyanya:


Visababishi vya matunda ya nyanya kuoza kitako

Kwakuwa tayari tunajua kuoza kitako kunasababishwa na upungufu wa Calcium, hapa tunaangalia sababu zinazopelekea mmea kushindwa kufyonza Calcium (Ca2+) kwenye udongo ambapo baadae hupelekea mmea kukosa au kushindwa kuitumia (Calcium, Ca2+) iliyopo.

 1. Kutokuwa na ratiba maalumu ya umwagiliaji kwa kuwa mmea unahitaji maji na wakati mwingine unahitaji ukame usio na madhara. Ukame sana au maji ya kutuama muda mrefu hufanya mmea ushindwe kufyonza Calcium (Ca2+) kwenye udongo.
 2. Kuwepo kwa virutubisho vya Nitrogen kwa wingi sana kwenye udongo. Hii hufanya mmea ukue kwa kasi kubwa kuliko mmea wenyewe unavyoweza kufyonza Calcium, (Ca2+) kwenye udongo
 3. pH kubwa sana (Zaidi ya 7.0) au ndogo sana (chini ya 6). pH inatakiwa iwe 6.5; isipungue sana wala isizidi sana.
 4. Udongo kuwa na chumvi chumvi nyingi sana.
 5. Kuharibika kwa mizizi kutokana na shughuri za ulimaji/palizi shambani.
 6. Baridi kali sana kwenye udongo hufanya mmea ushindwe kufyonza Calcium, (Ca2+) kwenye udongo.

Jinsi ya Kudhibiti tatizo la nyanya kuoza kitako

Tatizo la nyanya kuoza kitakohaliwezi kutibika, na tunachoweza kufanya ni kuondoa au kupunguza tu kwa kiasi sababu zinazochochea kutokea kwa tatizo hili:

 1. Wekautaratibu maalumu wa umwagiliaji na uufuate. Kama una mwagilia mara mbili kwawiki basi iwe hivyo.
 2. Hakikishakuwa udongo wako hautuamishi maji na tumia samadi au mboji ukiweza ili nyanyazipate mahitaji yake muhimu na hivyo upunguze matumizi ya mbolea za nitrogeni.
 3. Unapotumia mbolea za nitrogeni, tumia mbolea ambazo zina kiwango kidogo cha nitrogeni na utumie viwango vinavyoshauriwa au utumie nusu ya kiwango hicho. Pia mbolea za nitrogeni ziwe na kiwango kingi cha Phosphorus na epuka kuweka mbolea nyingi wakati nyanya zinaanza kutoa matunda.
 4. Tumiamatandazo (Mulch) ili kupunguza kupotea kwa maji kwenye udongo.
 5. Dhibiti pH ya udongo, na uhakikishe haizidi sana wala kupungua sana kutoka 6.5
 6. Tumia mbolea ya maji ya Calcium (Ca2+) – Ca foliar fertilizer
 7. Kita miti ya kupandia mimea ya nyanya (Stakes)
 8. Epuka kuharibu mizizi wakati wa kulima/kupalilia shambani.

Nini kifanyike tatizo likisha tokea?

 1. Chuma au ondoa matunda yote yaliyoathirika na uyatupe, yaliyo athirika kidogo unaweza kukata na kutumia sehemu nzima, hayata kuzuru. Ukisha yaondoa matunda yaliyooza mmea utaweka tena maua na kuzaa matunda mengine, mazuri. (2) (1)
 2. Pulizia mbolea ya maji ya Calcium baada ya kuondoa matunda yote yaliyoathirika. (2)
nyanya-zilizooza-kitako
Nyanya zilizooza kwenye kitako

Mazingatio muhimu:

Tatizo la nyanya kuoza kitako agahalabu hutokea kwa sababu za kimazingira zaidi na hivyo kufanya lisiwe ndani ya uwezo kulidhibiti kabisa lisitokee.

Na baadhi ya rejea zinasema tatizo hili ni (kama) lazima litokeee katika hatua moja wapo ya uzaaji wa matunda kwenye nyanya ambapo mara nyingi huwa ni ile ya kwanza.

Hata hivyo baadaye tatizo hili huisha lenyewe bila wewe kufanya chochote kulidhibiti (…na pengine bila kusababisha matatizo makubwa sana). (1)


Rejea muhimu:

1. http://gardeningknowhow.com/edible/vegetables/tomato/tomato-blossom-rot.htm
2. http://almanac.com/pest/blossom-end-rot
3. http://gardeners.com/how-to/blossom-end-rot/5354.html
4. http://www.tetrachemicals.com/Products/Agriculture/The_Importance_of_Calcium.aqf
0 0 vote
Article Rating

Mtalula Mohamed

I like blogging. In order utilize my profession I chose to share, to blog, a few tips and tricks about farming and agriculture to anyone interested.

Subscribe
Notify of
guest
7 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Godfrey
Godfrey
1 year ago

Asante sana mtaalam, Je hii inaweza kuwa pia sababu ya baadhi ya Matunda kama stafeli, papai michungwa kuangusha Maua badala ya kuweka Matunda?

Asia
Asia
1 month ago

Thanks

Mohamed Mtalula
Mohamed Mtalula
Reply to  Asia
1 month ago

Karibu sana

Mboje, M.J
Mboje, M.J
25 days ago

Thanks bro.

Alex kasanda
Alex kasanda
1 day ago

Je tatizo la nyanya kuoza kitako linaweza kusababishwa na athari za ukungu?

error: Content is protected !!
7
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x

Join Our Farming Community