Viuatilifu ni nini?

Viuatilifu ni wingi wa Kiuatilifu. Kiuatilifu ni sumu ambayo hutumika kuua, kuangamiza, kufukuza, au kuzuia visumbufu katika mimea.

Visumbufu  vya mimea vinaweza kuwa wadudu, kuvu (fungasi), magugu pamoja na baadhi ya wanyama na ndege.

Kiuatilifu kinaweza kunyunyizwa kwa kutumia bomba la kawaida (sprayer) au kutumia tanki maalumu lililoshikwizwa kwenye aidha trekita au aeroplane (ndege)

Ili kiuatilifu kiweze kufanya kazi kwa lengo lililokusudiwa, kuna mambo mengi ya msingi ya kuzingatia katika aidha maandalizi ya kunyunyiza au wakati wa kunyunyiza.

Unyunyiziaji wa viuatilifu ni kitendo cha kufikisha mchanganyiko wa kiuatilifu kwenye shabaha iliyokusudiwa kwa lengo la kudhibiti visumbufu.


Bomba la kunyunyiza viuatilifu
Bomba la mgongoni (knapsack sprayer) la kunyunyiza viuatilifu

Usiache kusoma makala hizi;


Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Wakati  Wa Unyunyiziaji (au Matumizi ya) Viuatilifu

Ili kiuatilifu kiweze kufanya kazi kwa usahihi kuna mambo mhimu ya kuzingatia wakati wa maandalizi ya kunyuyiza au wakati wa kunyunyiza. Mambo hayo ni haya yafuatayo:-

1..Hatua ya ukuaji wa visumbufu

Ili kupata ufanisi bora shambulia visumbufu vikiwa katika hatua dhaifu ya maendeleo ya ukuaji wake kufuatana na makazi yake, tabia na mzunguko wa maisha yake.

Ukikosea unaweza kusababisha wadudu kuharibu mazao na pia wanaweza kuwa sugu juu ya kiuatilifu hicho. Pia kunyunyiza kiuagugu kipindi magugu yamekomaa hushindwa kuleta matokeo mazuri ya lengo.


2. Viwango vya sumu na ujazo kwa eneo (DOZI)

Unapotumia kiuatilifu hakikisha unasoma vizuri maelekezo ya matumizi ili uweze kutumia kipimo sahihi cha sumu katika ujazo sahihi wa maji.

Ukizidisha kipimo cha sumu husababisha athari kwa mmea, mazingira, kwa walaji na pia huongeza gharama kwani viuatilifu vingi vitahitajika kwa eneo dogo.

Aidha ukipunguza kiwango cha sumu husababisha kutotimia kwa lengo lililokusudiwa na hatimaye pia hufanya visumbufu kuwa sumu.


3. Maeneo ya shabaha lengwa

Tumia mbinu tofauti tofauti kunyunyiza kiuatilifu kulingana na maeneo ya shabaha lengwa.

Kwa mfano, kama unazuia wadudu ambao hukaa chini ya majani ya mmea hakikisha nozeli yako unaishusha chini na uigeuzie juu ili inyunyize vizuri chini ya jani.


4. Hali ya hewa

Upepo husababisha kupeperushwa kwa matone na kupelekwa yasikotakiwa. Hivyo unaponyunyiza hakikisha hali ya hewa ni tulivu isiyo na upepo mkali. Aidha kuna baadhi ya sumu hupungua nguvu zake baada ya zikinyeshewa mvua muda mfupi baada ya kunyunyizwa.

Nyunyiza kipindi ambacho hakuna dalili ya mvua kunyesha muda mfupi ujao. Pia kuna baadhi ya sumu hasa za magugu hazitakiwa kunyunyizwa wakati majani/magugu yana umande.


5. Aina ya bomba lifaalo

Uchaguzi wa bomba la kunyunyizia ni muhimu sana kwani kuna baadhi ya mimea hurefuka  na kukufanya ushindwe kutumia bomba la mgongoni.

Kwa mfano; miembe, mikorosho, michungwa, miparachichi. Hivyo tumia bomba lifaalo kulingana na aina ya mazao.


6. Namna ya kutembea wakati wa kunyunyiza (kwa bomba la mgongoni)

Mnyunyizaji anatakiwa awe makini namna ya kutembea wakati ananyunyiza, asipokuwa  makini kuna uwezekano wa kuruka baadhi ya sehemu.

Kutembea harakaharaka sana bila umakini husababisha dawa kutofikia kwa usahihi maeneo lengwa, aidha kutembea polepole sana hupelekea sumu nyingi kutumika katika eneo dogo, pia mnyunyizaji anatakiwa awe makini kukariri matone yanapoishia ili yaweze kukutana na matone mengine (overlap)


Soma hapa;


7. Kutumia viuatilifu sahihi na vilivyothibitishwa /sajiliwa na mamlaka husika

Unapotumia kiuatilifu hakikisha unatumia kiuatilifu kilichosajiliwa ili kuepuka kutumia vilivyo feki. Mamlaka inayohusika na usajili wa viuatifu hapa Tanzania ni Tropical pesticides research institute (TPRI). Katika kifungashio cha kiuatililifu kagua alama zifuatazo kama zimewekwa kwa usahihi.

 • Aina ya kiuatilifu
 • Maelekezo ya matumizi ya kiuatilifu
 • Maisha rufani (tarehe ya kutengenezwa/kuisha matumizi)
 • Mtengenezaji
 • Msambazaji
 • Namba ya utambulisho
 • Namba ya usajili na nembo ya TPRI
 • Tahadhari
 • Lugha – Kiswahili/kiingeleza

8. Aina ya kinyunyizo (nozeli) unayotumia

Vinyunyizo (nozzles) ni semu ya upande mmoja wa bomba iliyominywa ambapo kimiminika kinatoka kama mtrizi (a jet).

Kwa lugha rahisi vinyunyizo ni hujulikana kama NOZELI ambayo ndipo mchanganyiko wa kiuatilifu hutokea na kufika katika mmea.

Ukubwa wa matone kutoka katika nozeli hutegemea aina ya kisumbufu lengwa kilicholengwa. Hivyo ili kumrahisishia mkulima kutambua ni matone ya aina gani yanatakiwa, ni vyema akafahamu rangi za nozeli na matumizi yake.

Nozeli zinatofautishwa kwa rangi tofauti kufuatana na ukubwa wa matone na kazi iliyokusudiwa. Rangi zinazotumika katika nozeli ni:- BLUU, NYEKUNDU, NJANO, KIJANI, NYEUPE NA MACHUNGWA


Nozeli za bomba la kunyunyiza viuatilifu
Mgawanyo wa nozeli kulingana na rangi na matumizi yake

Jedwali lifuatalo linaonyesha mgawanyo wa nozeli kulingana na ukubwa wa matone na matumizi na rangi zake.


Hitimisho

Viuatilifu ni sumu hivyo tahadhari inatakiwa wakati wa kutumia kwani husababisha madhara makubwa sana kwa mimea, binadamu na mazingira. Baadhi ya tahadhari muhimu kuchukua ni:-

 • Vaa mavazi kinga unaponyunyiza kiuatilifu
 • Usitumie kifungashio tupu cha kiuatilifu (empty container) kwa matumizi mengine
 • Usitupe ovyo kifungashio tupu cha kiuatilifu (empty chemical containers)
 • Usihifadhi kiuatilifu karibu na vyakula
 • Usile wala kunywa chochote baada ya kutumia kiuatilifu bila kunawa na kuosha mikon vizuri

Usipitwe na makala hizi muhimu:

Karibu Jukwaa la Mkulima
Karibu Jukwaa la Mkulima

Jukwaa la Mkulima ni nini? Hili ni jukwaa ambalo tumeliandaa kwa ajili ya mijadala na hoja za kilimo baina ya wakulima, wafugaji na wataalam wa kilimo na mifugo

Utabiri wa Mvua za Vuli 2019
Utabiri wa Mvua za Vuli 2019

Katika msimu wa mvua za vuli 2019, maeneo mengi ya nyanda za juu kaskazini mashariki pamoja na pwani ya kaskazini yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi…

Aina Bora 19 za Mbegu za Mihogo
Aina Bora 19 za Mbegu za Mihogo

Zaidi ya aina 45 za mbegu za mihogo zinajulikana hapa nchini. Zaidi ya 80% ya mihogo ni ya asili. Hivyo wakulima wengi hawatumii mbegu bora za mihogo.

0 0 vote
Article Rating

Mtalula Mohamed

I like blogging. In order utilize my profession I chose to share, to blog, a few tips and tricks about farming and agriculture to anyone interested.

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x

Join Our Farming Community