Uchaguzi wa mbegu bora za mihogo

Wakulima wanapaswa kupata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa kilimo kuhusu aina bora za mbegu za mihogo zenye ukinzani wa magonjwa na wadudu waharibifu, zinazostahimili ukame na zenye mavuno mengi.

Katika Makala hii nitakufahamisha aina za bora za mbegu za mihogo zilizopo Tanzania ambazo wewe unaweza kuzitumia, kulingana na kanda za kilimo. Kama bado, bofya hapa usome jinsi ya kulima mihogo

vitabu-vya-kilimo-bora-GIF

Aina za mbegu za mihogo

Kuna zaidi ya aina 45 za mbegu za mihogo zinajulikana nchini Tanzania. Zaidi ya asilimia 80 ya mihogo ni ya asili. Hivyo ni kusema wakulima wengi hawatumii mbegu bora za mihogo.

Wakulima wengi pia hupendelea kulima aina za mihogo michungu kwa sababu haishambuliwi sana na wadudu ama magonjwa shambani na makopa yake yanahifadhika kwa urahisi. Hata hivyo zaidi ya asilimia 70 ya mihogo yote inayolimwa Tanzania ni mihogo baridi.

Mbegu za mihogo ya asili

Mihogo ya asili ni ile iliyoendelea kulimwa miaka mingi iliyopita na kurithiwa vizazi kwa vizazi. Mbegu za mihogo hii zina sifa za zifuatazo:

 • Hutoa mavuno wastani wa tani kwa Hekta.
 • Mingi inachukua muda mrefu kukomaa
 • Inahifadhika shambani kwa muda mrefu bila kuoza
 • Hushambuliwa na magonjwa kama Ugonjwa wa michirizi ya ki-kahawia, batobato na blaiti.
 • Hushambuliwa na wadudu aina ya milibagi
 • Imezoeleka na wakulima hivyo wanaijua tabia yake na jinsi ya kuitunza.

Mbegu za mihogo bora

Hizi ni aina za mihogo iliyofanyiwa utafiti wa pamoja baina ya watalaam na wakulima na kuthibitishwa na Kamati ya Mbegu ya Taifa kama inafaa.

Kituo cha Utafiti wa Mazao ya Kilimo cha Naliendele (cha Mtwara) pamoja na vituo vingine vya utafiti wa mazao ya kilimo, vimebaini mbegu bora mbalimbali za mihogo ambazo zinakomaa mapema, zinazaa sana na zinastahimili magonjwa na ukame kuliko zile mbegu za asili. Kwa mazao mengine, bofya hapa usome aina mpya za mbegu bora zilizothibitishwa.

mbegu za mihogo
Vipande vya Mbegu za Mihogo

Zifuatazo ni mbegu bora za mihogo zinazopendekezwa kulimwa kulingana na kanda za kilimo:

Kwa Kanda ya Ziwa:

(1) Mkombozi

 • Mavuno 16-23t/ha
 • Ukinzani dhidi ya magonjwa batobato na michirizi kahawia
 • Inastawi mita 600-1800m kutoka usawa wa habari
 • Hukomaa kati ya miezi 8-12.

(2) Kyaka

 • Mavuno 16-23t/ha
 • Ukinzani dhidi ya batobato na michirizi kahawia
 • Inastawi mita 900-1800 kutoka usawa wa bahari
 • Hukomaa kati ya miezi 8-12

(3) Meremeta

 • Mavuno 16-23t/ha
 • Ukinzani dhidi ya batobato na michirizi kahawia
 • Inastawi mita 900-1800 kutoka usawa wa bahari
 • Hukomaa kati ya miezi 8-12

(4) Nyakafulo

 • Mavuno 16-23t/ha
 • Ukinzani dhidi ya batobato na michirizi kahawia
 • Inastawi mita 900-1800 kutoka usawa wa bahari
 • Hukomaa kati ya miezi 8-12

(5) Suma

 • Mavuno 16-23t/ha
 • Ukinzani dhidi ya batobato na michirizi kahawia
 • Inastawi mita 900-1800 kutoka usawa wa bahari
 • Hukomaa kati ya miezi 8 mpaka 12

(6) Belinde

 • Mavuno 16-23t/ha
 • Inastawi mita 900-1800 kutoka usawa wa bahari
 • Hukomaa kati ya miezi 8-12

(7) Kasala

 • Mavuno 16-23t/ha
 • Ukinzani dhidi ya batobato na michirizi kahawia
 • Inastawi mita 900-1800 kutoka usawa wa bahari
 • Hukomaa kati ya miezi 8-12

(8) Rangimbili

 • Mavuno 16-23t/ha
 • Ukinzani dhidi ya batobato na michirizi kahawia
 • Inastawi mita 900-1800 kutoka usawa wa bahari
 • Hukomaa kati ya miezi 8-12

Kwa Kanda ya Mashariki na Kusini:

(1) Kiroba

 • Mavuno 26t/ha
 • Inastawi mita 0-100 kutoka usawa wa bahari
 • Ukinzani dhidi ya batobato na michirizi kahawia
 • Hukomaa miezi 8-12

(2) Mkuranga 1

 • Mavuno 17-25.5t/h
 • Kukomaa miezi 9-12
 • Ukinzani dhidi ya batobato na mchirizi kahawia
 • Uzito wa mazao baada ya kukauka 24-31%

(3) Chereko

 • Mavuno 11.2-29.2t/h
 • Kukomaa miezi 9-12
 • Ukinzani dhidi ya batobato na mchirizi kahawia
 • Uzito wa mazao baada ya kukauka 27-32%

(4) Kizimbani

 • Mavuno 22.6t/h
 • Kukomaa miezi 9-12
 • Ukinzani dhidi ya batobato na mchirizi kahawia
 • Uzito wa mazao baada ya kukauka 23-33%

(5) Kipusa

 • Mavuno 13.4-25.7t/h
 • Kukomaa miezi 9-12
 • Ukinzani dhidi ya batobato na mchirizi kahawia
 • Uzito wa mazao baada ya kukauka 24-34%

(6) Pwani

 • Mavuno 50.8t/h
 • Kukomaa miezi 11-12
 • Ukinzani dhidi ya batobato na mchirizi kahawia
 • Inasitawi mita 0-600 kutoka usawa wa bahari

(7) Mkumba

 • Mavuno 23.3t/h
 • Kukomaa miezi 9-10
 • Ukinzani dhidi ya batobato na mchirizi kahawia
 • Inastawi mita 0-600 kutoka usawa wa bahari

Kwa Kanda ya Kati:

(1) Dodoma

 • Mavuno 36t/h
 • Kukomaa miezi 9-10
 • Ukinzani dhidi ya batobato na mchirizi kahawia
 • Inastawi mita 700-1500 kutoka usawa wa bahari

(2) Mumba

 • Mavuno 26t/h
 • Kukomaa miezi 8-12
 • Ukinzani dhidi ya mchirizi kahawia
 • Inastawi mita 0-1000 kutoka usawa wa bahari

(3) Makutupora

 • Mavuno 30.3t/h
 • Kukomaa miezi 9-10
 • Ukinzani dhidi ya batobato na mchirizi kahawia
 • Inastawi mita 700-1500 kutoka usawa wa bahari

(4) Hombolo

 • Mavuno 39t/h
 • Kukomaa miezi 8-12
 • Ukinzani dhidi ya batobato na mchirizi kahawia na wadudu vidung’ata
 • Inastawi mita 0-1000 kutoka usawa wa bahari

Je wewe unatumia mbegu gani? Kwanini? Tueleze hapa chini kwenye comment.

Mtalula Mohamed

I like blogging. In order utilize my profession I chose to share, to blog, a few tips and tricks about farming and agriculture to anyone interested.

2
Leave a Message

avatar
2 Comment threads
0 Thread replies
2 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
2 Comment authors
Godwin MbwamboJackson mapunda Recent comment authors
  Subscribe  
newest oldest most voted
Notify of
Jackson mapunda
Guest
Jackson mapunda

Mbegu zinapatikana wap?

Godwin Mbwambo
Guest
Godwin Mbwambo

Mimi niko Dodoma ndo mwaka huu nataka msimu wa mvua nilime mhogo. Tatizo ni upatikanaji wa mbegu.Napenda makutupora ili nipate mazao mengi. Naipataje?