Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuri za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine (curcubitaceae family) kama matango, maboga na maskwash (squash). 

 

Zao la tikiti maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi. Katika shamba la ukubwa wa ekari moja (1 acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa na kuhudumiwa vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha tani 15-36, ambacho kitamsaidia kupata fedha za kukidhi mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na umasikini.

Tikiti-maji
Tikiti maji tayri kwa kuliwa

UCHAGUZI WA ENEO

Matikiti maji husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana, baridi kali, mvua nyingi wala udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu. 
 
Joto: Matikiti hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21 – 30 sentigradi. Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota. 
 
Mvua: Matikiti maji yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400 – 600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungasi na bakteria ambayo huathili mavuno. 
 
Hali ya Udongo: Kilimo cha matikiti huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0 

Mikoa ya Tanzania: Kilimo cha matikiti maji kinakubali vizuri kwenye ukanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM, Tanga, Morogoro, Mtwara, Lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa tatu mpaka wa tisa. 


Uandaaji wa Shamba
Fyeka vichaka na ng’oa visiki vyote. Katua kwa kina cha sm 22.5 kwenye Sesa. Kabla ya kupandikiza udongo utifuliwe vizuri na majani yaondolewe kabisa. Shamba liandaliwe vizuri kwa kusafisha ili kuondoa mimea mingine ambayo inaweza kuwa ni chanzo cha magonjwa. Weka mbolea ya samadi debe moja kwa kila mita 10 za eneo. Tengeneza matuta katika sehemu ambayo ina majimaji.
 

Upandaji wa tikiti maji

Katika shamba la ukubwa wa hekta moja kiasi cha kilo 3 – 4 cha mbegu kinaweza kutumika. Panda mbegu 2 au 3 moja kwa moja katika kila shimo. Usipande katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa mita 1 hadi 2 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 – 3 kutoka mstari hadi mstari. 

Zingatia: usitumie mbegu za tikiti ulilonunua (kwa ajili ya kula) kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi na ubora wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2).
 

Mbegu Bora za Matikiti 

Mbegu maarufu ya tikiti ni Sukari F1, hata hivo madukani zinapatikana nyingi bora na tofauti tofauti kama vile:
 
Upunguzaji Wa Mimea 
Mimea ya mitikiti huanza kuota, baada ya kama wiki 2 hivi. Hivyo katika mbegu mbili au tatu ulizopanda kata moja na uache ile miche yenye afya zaidi ndio uendelee kukua. Ni vizuri ukaacha miche miwili katika kila shimo.

Angalizo: Usinga’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki. Vilevile unaweza kupandishia udongo kwenye mashina ili kusaidia kupunguza maji kutuama kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba. Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya wa kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda. Wakati mimea inapo anza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe (kuielekezea) kwenye waya na kuifungia. 

 
Umwagiliaji 
Shamba linatakiwa limwagiliwe mara kwa mara wakati mvua zinapokosekana au wakati wa mvua chache. Kipindi muhimu zaidi ambapo mimea hii huhitaji maji ni katika kipindi cha uotaji wa mbegu, wakati wa kutoa maua na siku takribani kumi kabla ya kuvuna. Iwapo kutakuwa na ukosefu wa maji kutasababisha kutengenezwa kwa matunda ambayo si mazuri na yenye umbo baya, pia kupungua kwa ukubwa wa tunda.

Angalizo: usimwagilie matikiti wakati wa jioni sana au usiku kwasababu inaweza kusababisha magonjwa ya majani kutokana na unyevu kukaa muda mrefu. Vile vile usimwagilie juu ya maua wakati wa asubuhi au jioni kwasababu unaweza kuzuia wadudu kama nyuki ambao ni muhimu sana wakati wa uchavushaji. 

Mahitaji ya Mbolea ya Matikiti Maji

Mbolea ya kupandia: Wakati wa kupanda tumia DAP weka gram 5 kwa kwa kila shimo (lenye mbegu moja, na weka gram 10 au 15 kama kuna mbegu 2 au 3), hakikisha mbolea na mbegu havigusani.
Mbolea ya kukuzia: Wiki mbili baada ya miche yako kuota weka mbolea ya kiwandani NPK (Yaramila winner) gram 5 tena kwa kila mche, hakikisha unaichimbia chini na isigusane na mmea. Weka mbolea yenye Calcium kama Yaramila nitrabo au CAN gram 10 kwa kila shina unapoona matunda yameanza ili kusaidia kupata matunda makubwa na mazuri.
 
Kwa ekali 1 ya matikiti utahitaji mfuko mmoja wa DAP, mmoja wa NPK na mmoja wa CAN ikiwa utabakiza miche miwili kwa kila shimo.
 
Hivi ukiwa shambani unawezaje kupima gram 5 au 10 za mbolea? Ni vigumu lakini kwa makadirio ya karibu ujazo wa kifuniko kimoja cha maji safi au soda take-away ni sawa na gram 5 hivyo ili upime gram 10 jaza vifuniko viwili vya maji safi. Soma hapa mahitaji ya mbolea katika mahindi
 
Matandazo (Mulches) 
Matandazo ina maana ya kutumia nyasi na mabaki ya mimea mingine kufunika aridhi. Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile vile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.
kilimo-bora-cha-tikiti-maji
Matikiti maji shambani

 

WADUDU NA MAGONJWA YA TIKITI MAJI

Wadudu wa matikiti wako wa aina mbalimbali na wanaoshambulia sehemu za majani na maua, na wengine hushambulia matunda, pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea. 

Magonjwa kama ukungu wa unga (powdery mildew) na wa chini (Downy mildew) na mengine yathibitiwe kabla hayajaleta madhara kwenye mimea. Ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kupata dawa sahihi. Dawa aina ya Mancozeb inaweza kutumiwa kuthibiti magonjwa hayo hapo juu.

 
Vilevile matikiti hushambuliwa na wadudu ambao hukaa katika majani, maua na matunda. Dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda. Soma hapa magonjwa ya nyanya na dawa zake
 

UVUNAJI NA UHIFADHI WA MATIKITI

Matikiti maji ni miongoni mwa mazao yanayochukua muda mfupi sana kukomaa. Kwa kawaida tikiki maji huwa tayari kwa kuvuna baada ya siku 80 hadi 100 baada ya kupanda. Vuna wakati tunda limeiva kabisa. Vuna kwa wakati unaofaa. Epuka kulijeruhi tunda. Hifadhi katika eneo lenye ubaridi nyuzi 15 hadi 20 C. Hifadhi vizuri, unyevua-anga (humidity) uwe 80 hadi 85%. Uza mara tu baada ya kuvuna shambani.

MCHANGANUO WA KIPATO CHA MATIKITI KWA UFUPI

Vitu vya kuzingatia:
 • Hekta 1 = Square meter 10,000
 • Ekari 1 = Square meter 4000
 • Hekta 1 = Ekari 2.5
Tuchukulie mathalani una ekali moja
Ukipanda matikiti yako kwa nafasi ya 1m x 2m utakua na mashimo 2000 ya kupanda mbegu zako. Ikiwa kila shimo utapanda mbegu tatu na ukapunguzia mche mmoja na kuacha miwili ikue basi utakua na mimea 2 x 2000 = 4000.
 
kwa hiyo kwa ekali moja utakua na mimea 4000 ya matikiti. haya tufanye umeipunguzia matunda na hivyo kuufanya kila mmea uzae matunda mawili tu hivyo tunatarajia utavuna matunda 2 x 4000 = 8000.
 
Hivyo basi katika ekali moja ya matikiti uliyopanda kwa nafasi ya 1m x 2m ukakuza mimea 4000 utapata matunda 8000!
 
Tuchukulie mathalani umeamua kuuza matikiti yako shambani kwa bei ndogo kabisa ya Tsh. 1000 kwa tikiti moja, ukiuza matikiti yote 8000 utapata jumla ya Tsh. 1000 x 8000 = Tsh. 8,000,000 (Milioni nane)! 
 
Inawezekana kabisa kuwa huu mchanganuo ni wa nadharia tu lakini ndugu yangu tumechukulia makadirio ya chini sana. Unajua ni kwanini? 
Angalia hapa: 
 • Mmea mmoja unaweza kuzaa matunda mangapi? We unajua lakini licha ya hayo yote sisi tumechukulia matunda mawili tu kwa mmea mmoja. 
 • Pia bei ya tikiti inategemea ukubwa wake lakini sisi tumechukulia yote ni sawa na tunauza kwa bei moja tu. 
 • Halafu pia bei ya matikiti tumechukulia ni Tsh 1000 tu wakati inaweza kuwa hadi Tsh 2000 uki-target wakati mzuri kwa soko.
 
Bila shaka utakuwa umenielewa vizuri sana, sasa fursa nimeiweka mikononi mwako na nimekufumbua macho yako, kazi kwako ndugu yangu. Lakini pia waweza kupitia namna ya kuzalisha matango na mananasi kisasa. Usisahau kuacha comment yako hapa chini.


Mtalula Mohamed

I like blogging. In order utilize my profession I chose to share, to blog, a few tips and tricks about farming and agriculture to anyone interested.

44 Comments

music department · February 20, 2017 at 11:25 am

Enter your comment…number yangu jamanii 0753389875 nahitajii uo ufundi wa matikiti

Francis Denis · March 15, 2017 at 11:41 pm

Nimejipanga ili kuhakikisha natumia elimu niliyoipata humu ndani na kuifanyia kazi

Mtalula Mohamed · March 25, 2017 at 6:39 pm

Nakutakia mafanikio mema kaka Francis Deni, itakuwa vizuri ukitujuza unavyoendelea kwa faida ya wengi

  Eliya · September 6, 2018 at 2:24 pm

  Habari, mimi nimejarib kulima matikiti huko kigambon lkn nilichokipata ni maumivu, nimelaza laki saba nimeambulia laki mbili na nusu. Nimeona hapa muda unaotakiwa lkn mwenyej wangu aliniambia ni miez miwili tu na nilipanda F1ya Kenya. Ila naomba kuuliza coz humu ndani sijakiona, Je ni kweli wiki moja ya mwisho unatakiwa usimwagie ili tunda liweke sukari? Naomba kuwasilisha

   Mtalula Mohamed · September 6, 2018 at 3:07 pm

   Pole sana kwa yaliyokufika. Mara baada ya matikiti kutoa matunda, yanapokuwa makubwa unatakiwa kupunguza maji kadri yanapoelekea kukomaa (refusha “irrigation interval”) kama ilikuwa mara mbili kwa wiki basi iwe mara moja kwa wiki au wiki mbili.

   Pia ni muhimu matitiki yapate muda wa ukame kwa wiki au zaidi, kabla ya kuvuna, ili yaweke sukari nyingi zaidi.

Unknown · April 2, 2017 at 12:51 am

Nimependezwa sana na elimu ya kilimo cha matikiti maji.Ntalifanyia kazi na ntaletà mrejesho hapa

Mdee sulley · April 2, 2017 at 9:49 am

Thanx kwa somo zuri

Ismail Sadick · April 22, 2017 at 9:00 pm

Mambo ni mazuri sana endelea kutuelimisha

Emmanuel Hinju · April 24, 2017 at 11:42 am

kikubwa ni mtaji tu,kweli kilimo kinalipa

Emmanuel Hinju · April 24, 2017 at 11:44 am

kikubwa ni mtaji tu,kweli kilimo kinalipa

Unknown · April 27, 2017 at 3:05 pm

nashukuru kwa elimu yako nzuri sana.nakuhakikishia nitaifanyia kazi fulsa hii na kwa mpango wa mungu nitafanikiwa na wewe ushukuriwe kwani naamini umenisogeza hatua moja mbele

  Mtalula Mohamed · October 31, 2018 at 3:07 pm

  Ahsante sana, fanya juhudi M/Mungu atakuwezesha. Usisahau ku-subscribe kwa mengi mazuri yajayo

Shedrack Rupenda · April 27, 2017 at 3:12 pm

Labda pia naombeni kuondolewa wasiwasi juu ya kilimo hiki.je jipi kuhusu mkoa wa kagera wilaya ya muleba kilimo hiki ni rafiki wa mazingira?Vipi kuhusu vipimo hivi vya pH,mm za mvua na kiwango cha jotoridi na ubaridi nitavipataje mimi mtu wa hali ya chini kikipato?mbegu na mbolea naweza kuzipata wapi kwa urahisi?vipi kuhusu bei ya vitu hivyo nilivyovitaja?nitashukuru nikipata majibu kupitia email yangu ya [email protected]

  Mtalula Mohamed · October 31, 2018 at 3:05 pm

  Mazingira / Hali ya hewa ya Muleba haina tatizo na kilimo cha matikiti maji.

  Vitu kama mbegu na mbolea vinapatikana katika maduka ya pembejeo za kilimo ama kwa suala la bei: Urea kwa kawaida ni Tsh 50,000, CAN ni Tsh 55,000 na DAP ni 80,000. Hizo ni bei kulingana na mazingira ya kwetu, hata hivyo bei zinaweza kubadilika kulingana na mazingira kwa hiyo inaweza kupungua au kuongezeka kidogo kwa niliyotaja mimi.

  Kuhusu vipimo vya Ph, joto na mm za mvua: hivi vinahitaji maelezo ya kutosha kwani ni changamoto kwa wakulima wengi. Hivyo nitaanza makala maalum kwa ajili hiyo.

david emil kikwilu · May 30, 2017 at 1:36 pm

Habari!!

Asante kwa elimu hii ya tikiti maji!!

kilimo cha matikiti katika ukanda wa mto ruvu (mlandizi) kinaweza kukubali bila kuathiri uzalishaji na ubora wa tikiti kama masharti yote ya kilimo hicho yakifwatwa? nikimaanisha hali ya hewa ya eneo inaruhusu?

Asante!!!!

George Sanane · June 26, 2017 at 10:10 pm

Nitumie pdf ya Kilimo cha matikiti, nimesha lipia 1000 kwenye Airtel money

Unknown · July 4, 2017 at 12:45 pm

Habari naomba namba yako ili tuweze kuwasiliana ili uweze kunielekeza 1kama kuna kulipia Huduma you n.a.
2 ili niweze kupata maelekezo zaidi

Desdel Nyamiti · July 12, 2017 at 2:37 pm

Asante sana kwa elim zur VP mkoa Wa Ruvuma matikiti yanaweza kustaw

dotto shauri · July 19, 2017 at 10:21 pm

Nimefaidika sana na elimu ya kilimocha tikiti maji……

dotto shauri · July 19, 2017 at 10:35 pm

Nimejipanga kupiga pesa tu

Mariam Idrisa · August 1, 2017 at 8:18 pm

Nashukuru kwa somo hili. Naomba number yako tafadhali

Erick Valentine · October 17, 2017 at 8:25 am

Napimaje ardhi ili kujuwa rutuba kama ina fahaa kwa hicho kilimo cha matikiti..!!? je naweza ku chota udogo wa eneo la shamba nakwenda wanako uza pembejeo na mbegu za mimea wana weza kupima pia..? au sehemu stahiki ni ipi..ili nijirizishe na eneo stahiki..!!?

  Mtalula Mohamed · September 6, 2018 at 3:12 pm

  Lengo la kupima udongo laweza kuwa kujua pH ya udongo au kiwango cha virutubisho kwenye udongo wako. Na hii inafanywa na wataalam (kuandaa sampuli ya udongo shambani, na kisha) kupima sampuli kwenye maabara ya kupima udongo au kwa vifaa maalum vya kupimia.

Sebastian · September 13, 2018 at 6:37 am

kwa mikoa ya Kanda ya ziwa zao hili linaweza kukua vizuri? hasa mkoa wa kagera na geita

Glory kamugisha · September 14, 2018 at 3:57 pm

Asante kwa elimu nzuri ….ila kunauvumi unasema kuwa kuna mbegu na dawa feki za Tikiti maji sasa basi utajuaje kama hii ni mbegu /dawa halisi na sio feki ?

  Mtalula Mohamed · October 31, 2018 at 2:25 pm

  Njia nzuri ni kuangalia “lebo” ya uthibitisho kwenye paketi ya mbegu au kopo la dawa. Kwenye paketi ya mbegu bora kuwe na nembo ya TOSCI – hii ni taasisi rasmi ya kuthibitisha mbegu bora kabla ya kuuzwa kwa wakulima. Na makopo/paketi za dawa ziwe na nembo ya TPRI – taasisi rasmi ya utafiti wa viatilifu

Herman Stephen · September 17, 2018 at 1:13 pm

Habari, mimi naomba kuuliza maana nimeshalima matikiti nimekula hasara Ile mbaya, maswal yangu ni 2,.lnasemekana unaweza kulima matikiti mara nne kwa mwaka je unaweza kuniambia ni miez ipi? Swal la pili, wanasema kwamba matikiti yakishakomaa kipindi cha mwisho kama wiki mbili au moja na nusu unayakatia maji ili yaweke sukari, na hili likoje? Naomba kuwasilisha

  Mtalula Mohamed · October 31, 2018 at 2:42 pm

  Pole kwa yaliyokufika.
  Swali la kwanza: Ukitumia green house, unaweza bila shida. Lakini kwa shamba la wazi ni lazima uepuke maji ya mvua wakati wa maua, lkn pia uhakikishe hakuna maji ya kutuama na mwisho ujidhatiti kudhibiti wadudu na magonjwa ya fungus.

  Kwa swali la pili: Jibu ni ndio. Ili kuongeza sukari, matitiki yanahitaji kipindi fulani cha ukame usio na madhara. Kukata maji wiki au mbili kabla ya kuvuna kunaweza kufaa.

Nick · November 13, 2018 at 6:44 pm

Vijana wajiunge vikundi then wajichange hata kidogo waanze na eneo dogo nguvu zao zitumike kuhudumia shamba, baada ya mavuno mtaji Utaongeza ndipo waweze kuchukua eneo kubwa

Fred · January 14, 2019 at 12:16 am

Keep it up br, najua utasaidia watanzania wengi kwa elimu hii ya bure. Mungu akusaidie pia

Biseko Kimasa · February 14, 2019 at 6:40 am

Najihusisha na Kilimo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *