Nanasi

Jinsi ya kufanya Kilimo cha Nanasi

Utangulizi

Nanasi ni tunda la kitropiki, linapendwa na walaji wengi kwa sababu ya ladha yake tamu na harufu yake nzuri. Tunda hili laweza liwa mara tu baada ya kuvunwa, baada ya kulipika, au kama juisi. Nanasi ni chanzo kizuri cha vitamin A na B, pia inakiwango kingi tu cha vitamin C pamoja na madini kama vile: patasiam, magnesiam, kalsiam, na madini chuma. Asili ya mananasi inaaminika kuwa ni Brazil na Paraguay huko Amerika ya Kusini. Hapa Tanzania, mananasi hulimwa zaidi maeneo ya Bagamoyo, Kibaha (Pwani), Tanga, Mtwara, Lindi, Geita na Mwanza. Lakini pia maeneo yote ya pwani ya Tanzania yanafaa kwa kilimo cha nanasi.

Hali ya hewa inayofaa kwa ukuaji wa nanasi
Kilimo cha nanasi kinapendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema katika mwinuko kati ya mita 0-1750 kutoka usawa wa bahari. Mwinuko wa mita 1300 hadi 1750 hufaa zaidi kwa uzalishaji wa nanasi kwaajili ya kusindika na mwinuko chini ya hapo hufaa zaidi kwaajili ya ulaji wa moja kwa moja. Mahitaji ya joto ni kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C.

Udongo unaofaa kwa kilimo cha nanasi
Kwa kilimo cha mananasi chachu (pH) ya udongo inayofaa ni 5.5 hadi 6.0, na hustawi vizuri zaidi katika udongo tifutifu na udongo wenye kichanga usiotuamisha maji. Ingawa nanasi huweza kustawi katika udongo wa aina yoyote ile, udongo wa mfinyanzi haufai kwa kilimo cha nanasi.

Maandalizi ya shamba
Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45. Shamba la nanasi unaweza kulilima kwa sesa (flat-bed) au kwa matuta (furrows).
Kwa sesa: chimba mashimo kwa nafasi ya sm.60 kati ya mistari, sm. 30 kati ya miche na sm. 80 kati ya kila mistari miwili. Weka mbolea kianzio katika kila shimo na upande, hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda. Weka tani 10 hadi 15 za mbolea ya kuku, weka pia viganja 2 vya mbolea ya zizi katika kila shimo.

Upandaji wa mananasi
Zipo aina mbali mbali za ‘mbegu’ (machipukizi/maotea) lakini yale yanayochipua kutoka ardhini hufaa zaidi na hukomaa mapema. Chagua machipukizi mazuri yenye umri mdogo na yenye kulingana kwa ukubwa. Iweke miche kwenye kivuli kwa siku 3 kabla ya kuipandikiza iweze kutoa mizizi haraka. Pandikiza mwanzoni mwa mvua za masika. Nafasi iwe sm.60 kati ya mistari, sm. 30 kati ya miche na sm. 80 kati ya mistari miwili. Pandikiza miche 50,000 katika hekta moja. Chovya miche kwenye dawa ya Diazinon au Fention kwa muda wa dakika 25 kabla ya kuipandikiza ili kuzuia mashambulizi ya wadudu.

Palizi
Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu. Katika kilimo cha nanasi magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu. Matumizi ya viuagugu hurahisisha zaidi palizi ya nanasi ukizingatia kuwa nanasi huwa na miiba katika ncha za majani yake ambazo huchubua ngozi endapo palizi za jembe zitatumika. Njia nyingine ni matumizi ya matandazo (mulch) ya majani au plastiki (plastic mulch) maalum kuzuia magugu.

shamba-la-mananasi
Shamba la mananasi

Mahitaji ya mbolea
Weka mbolea ya NPK gramu 50 hadi 70 kwa kila mche wakati wa kupanda. Weka tena gramu 85 kwa kila mche baada ya miezi 3 na pia miezi 3 baadae.

Wadudu na Magonjwa yanayosumbua minanasi
Nanasi ni zao lisilosumbuliwa na wadudu ama magonjwa mara nyingi. Hii ni faida kubwa sna kwa wakulima wa nanasi! Hivyo endapo patatokea mashambulizi ya wadudu na magonjwa, ushauri zaidi wa kitaalam utafutwe kukabiliana na tatizo husika. Hakikisha unakagua shamba ili kuzuia wadudu kama wataonekana.

Uvunaji wa mananasi
Nanasi huanza kutoa maua miezi 12 hadi 15 baada ya kupanda kutegemeana na aina ya nanasi au maotea ya mbegu yaliyotumika, muda wa kupanda na joto la mahali husika. Kwa kawaida nanasi hukomaa miezi 5 baada ya kutoa maua, hivyo nanasi huchukua miezi 18 hadi 24 kukomaa/kuiva. Katika kilimo cha nanasi, mimea ikitoa maua kwa nyakati tofauti tofauti itasababisha kuvuna kidogo kidogo na kwa muda mrefu. Kwa sababu hiyo ndio maana ni muhimu kupanda kwa wakati mmoja mbegu zenye umri na ukubwa sawa.
Kwa wanaofanya kilimo cha nanasi kibiashara (commercial pinapples production) hutumia kemikali aina ya Ethrel (@ 100 ppm) mwezi mmoja kabla ya kuanza kutoa maua ili mimea mingi iweze kutoa maua kwa wakaii mmoja, angalau 80% ya mimea yote. Vuna wakati kikonyo cha nanasi kimebadilika rangi kuwa njano ya dhahabu. Kata kikonyo cha nanasi chenye urefu wa sm. 30 kikiwa kimeshikana na nanasi na upunguzie majani ya kichungi chake.

Utunzaji wa mananasi
Hifadhi nanasi katika eneo lenye ubaridi huku kikonyo chake kikielekea juu. Hakikisha unauza nanasi mara tu au siku 2 hadi 3 baada ya kuvuna ili kutunza ubora wake.
mananasi-yaliyovunwa
Mananasi yaliyovunwa
Usiache kusoma makala hizi muhimu:
Weka comment yako hapa ili kubadilishana uzoefu na wakulima wengine.
Pls share this post

Farming Tips and Tricks

If you like farming you will definitely love our contents. Join us now

38 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

    • Nanasi huweza kupandwa muda wowote isipokuwa kipindi cha mvua nyingi kuepuka miche kuoza

      mbegu ya nanasi unaweza kuipata kutoka mashamba ya wakulima wenzako chamsingi chagua mbegu nzuri. Kiwangwa inasifika kwa mkoa wa Dar na Pwani kulima nanasi kwa kiwango kikubwa,wilaya zingine nipamoja na Kibaha. Ikiwa utakosa miche tuwasilianeniko Mlandizi Kibaha.

  1. mbegu za mannasi zipo nyingi sana , nenda mbezi kabla ujafika kibanda cha mkaa wanauza mbegu za mannasi , mche mmoja wanauza tsh 250 , mda wa kupanda nanasi ni kwanzia mwezi wa kumi nakuendelea ………..!!

  2. mbegu za mannasi zipo nyingi sana , nenda mbezi kabla ujafika kibanda cha mkaa wanauza mbegu za mannasi , mche mmoja wanauza tsh 250 , mda wa kupanda nanasi ni kwanzia mwezi wa kumi nakuendelea ………..!!

    • Naomba kuongezea majibu kama alivyojibu mtaalamu Mtalula.

      ili kujihakikishia mashina yaliyovunwa nanasi yanaendelea kuzaa nivyema sana ukisha vuna upruni shina mama.

      kupruni shina mama kunakuhakikishia shina hili kuotesha vichipukizi vingi 4 hadi 6

      Unachotakiwa kujua nikwa kadri machipukizi yanavyokua shina mama hufa.

      chagua chipikizi lililoota kutokea ardhini katika shina mama ndilo ulilee kama mnanasi mpya, machipukizi mengine yaliyootea juu yatumike kama mbegu na baada ya miezi 2 hadi 4 yatolewe.

      ukifanya hivo utavuna msimu wa pili na hata wa tatu. ikumbukwe kuwa wakati huu tunda huwa linapungua unene ukilinganisha na tunda la kwanza.

    • kipato cha kilimo cha nanasi kinategemea eneo ulilomia,mahitaji ya nanasi,mbinu ulizotumia kuzalisha nanasi n.k

      Ili kujihakikishia kipato kizuri cha nanasi hakikisha unazalisha nansi nje na msimu ulio zoeleka kwakutumi homoni mfano Ethrel au Ethephone ambazo zinakufanya uweze control uzalishajina kubalance soko.

      kipndi cha nanasi hamna mara nyingi mashambani nanasi hununuliwa kati ya Sh 1,000 hadi Sh1,500

      kutokana na bei hiyo tunakukadiria kipato cha sh. 15,000,000 hadi Sh. 20,000,000 milioni. kulima nanasi kizamani ningumu kukadiria mavuno kwa kila shina lizaa kwa muda wake.

    • Ekari 1 nisawa na square mita 4000

      kibiasha tunatumia kipimo cha sm 30X60X90 sawa na miche 17,556 lakini hasahasa tunatumia kipimo cha sm 30X60 sawa na miche 22,200

  3. Ninajiandaa kuanza kilimo cha nanasi. Shamba langu liko wilaya ya Kisarawe na naomba kujua nitapata wapi mbegu bora za nanasi na bei ya mbegu ikoje?

    • Kilimo cha nanasi katika mkoa Pwani ni kilimo rahisi sana na kina kubali kabisa.
      Wila ya ya kisarawe ina udongo wenye rutuba kiasi na mazao mengi yanakubali. Mfano mzuri wa kilimo hiki ni Kiwangwa iliyoko Wilaya ya Chalinze.
      Kuhusu miche, kwa ufupi nikwamba nivema kuchukua mbegu kutoka kwa wakulima wanaokuzunguka kuepusha gharama kubwa. utahitaji Mbegu kati ya 17,500 katika ekari 1 ikiwa utapnda kwa kipimo cha sm 30X60X90 na miche 22,000 kwa kipimo cha sm60X30
      Unaweza kusaidiwa kupata technolojia ya kuzalisha nanasi katika kipindi chote cha mwaka mzima na kwa muda mfupi sana.
      tuwasiliane kwa 0757411516,nipo Mlandizi Kibaha Pwani.
      Asante

    • Unafaa, kikubwa nikuhakikisha pH ya udongo iko katika 4.5 hadi 6.5 hali joto iwe kati 22C hadi 32C
      Epuka udongo mfinyanzi.

  4. Nipo bukoba – kagera ni mkulima wa nanasi,,, naomba kama upo bukoba na unahitaji kulima nanasi; au unalima nanasi,,, naomba tuwasiliane ili tuweze kupanua wigo mpana katika kilimo cha nanasi pia tuweze kupata mbegu iliyo bora inayostahimili kulima bukoba pamoja na soko,,,,
    Mawasiliano 0744064308

    • Habari Jackson
      Binafsi ni mtaalam wa kilimo ikiwemo nanasi, kwasasa tumefikia atua ya kuzalisha nanasi muda tunao utaka ili kubalance hali ya soko.kwa mawasiliano zaidi 0757411516
      Kibaha Pwani

    • Bukoba kuna soko zuri la nanasi?
      Nina eneo Muleba naweza kupanda nanasi maana story za fhia zimeshanichosha.

  5. Habar kiongozi mim nataka nifanye kilimo cha nanasi ila nilikuwa naomba ushauri natakiwa niwe na kiasi gani cha fedha kupata shamba,mbegu na vitu vingine kwa shamba nataka tu la kukodi