Kulingana na msimu mahindi hupandwa mwanzoni mwa mwezi wa 11 baada ya mvua za kwanza kunyesha (specifically from 1st to 15th day of November) ambayo huvunwa mwezi Machi mwishoni au aprili mwanzoni. Pia mahindi hupandwa mwanzoni mwa mvua za masika yaani mwezi wa pili mwishoni na mwezi wa tatu mwanzoni ambayo huvunwa mwezi Julai katikati na Agosti mwanzoni….
KUANDAA SHAMBA, KUPANDA NA KUPALILIA
Kuandaa Shamba, Kusafisha, Kulima/Kutifua
Ni vyema mashamba yaandaliwe mapema kabla ya msimu wa kupanda haujaanza ili kumpa mkulima fursa ya kupanda kwa wakati unaotakiwa. Kuna njia mbalimbali zinazotumika kuandaa mashamba. Kati ya njia hizi ni pamoja na kufyeka, kung’oa visiki na kulima. Shamba linaweza kulimwa kwa kutumia:
- Jembe la mkono – wengi wanatumia
- Jembe la kukokotwa na wanyama kama ng’ombe
- Power tillers
- Matrekta
Matumizi ya trekta, power tillers na jembe la kukokotwa na wanyama yanapunguza nguvu kazi kwani vinachimbua udongo na kuufanya kuwa tifutifu (kufanya isiwe na mabonge makubwa, wala isiwe vumbi vumbi). Hii husaidia:
- Mizizi ya mimea kupenyeza ardhini kirahisi
- Udongo kuweza kuhifadhi maji
- Udongo kuwa na hewa inayohitajika na mimea
- Ukuaji mzuri wa mimea hivyo kuongeza mavuno
Matumizi ya mbegu bora ni muhimu katika upatikanaji wa mavuno mengi na bora. Kuna makundi mawili makuu ya mbegu ambayo ni:
- Mbegu za asili: Ni zile ambazo zimetumika miaka mingi katika historia ya kilimo
- Mbegu zilizoboreshwa: Hizi ni zile zilizoboreshwa kutoka mbegu za asili. Kundi hili linagawanywa kwenye makundi mawili – composite varieties na mbegu chotara (Hybrids).
Ushauri wa matumizi ya mbegu zilizoboreshwa unatofautiana kutoka eneo moja na lingine kwa sababu ya:
- Mwinuko kutoka usawa wa bahari
- Kiasi cha mvua katika eneo husika
- Muda unaotumia mbegu hadi kukomaa
Mbegu za mahindi zilizoboreshwa ni kama TMV1, TAN 250, TAN 254, Staha, Situka na zingine zote zinazoanza na herufi “H” kama vile H 250, H 251 na H 615. Pia mbegu mpya zilizotangawa na Kamati ya Taifa ya Mbegu mwaka huu ni WE4102, WE4106, WE4110, WE4114, WE4115 kutoka ARI ILONGA. Jinsi Ya Kuweka Mbolea Za Kupandia
Mbolea hizi zinawekwa shambani kabla ya kupanda/kusia mbegu. Zinawekwa kwa njia mbalimbali kama vile kusambaza kwenye eneo husika na kuchanganya na udongo, au kuweka kwenye mistari au mashimo ya kupandia. Ni bora zaidi kuchanganya mbolea za Minjigu Phosphate au Minjingu Mazao na udongo kuliko kutia kwenye shimo la kupandia. Pia kuchanganya mbolea na udongo huondoa athari za mbolea kwenye uotaji wa mbegu, hasa kama kuna uhaba wa unyevunyevu.
Viwango Vya Mbolea Za Kupandia mahindi
Kiwango cha mbolea za kupandia kilichopendekezwa ni kilo 20 fosfati (P) kwa hektari ambayo ni sawasawa na kiasi cha mifuko 2 ya DAP (= mfuko mmoja kwa ekari). Ikiwa mbolea ya minjingu phosphate itatumika basi mifuko mitatu itatosa kwa hekta (= mfuko mmoja na nusu kwa ekari). Na endapo utaamua kuitumia mbolea ya minjingu mazao basi tumia mifuko minne na nusu kwenye hekta moja au mifuko miwili kwa ekari moja.
Upandaji wa mahindi
Muda wa kupanda: Kulingana na msimu mahindi hupandwa mwanzonimwa mwezi wa 11 baada ya mvua za kwanza kunyesha (specifically from 1st to 15th day of November) ambayo huvunwa mwezi Machi mwishoni au aprili mwanzoni. Pia mahindi hupandwa mwanzoni mwa mvua za masika yaani mwezi wa pili mwishoni na mwezi wa tatu mwanzoni ambayo huvunwa mwezi Julai katikati na Agosti mwanzoni. Katika msimu huu utayarishaji wa shamba hufanyika mwezi wa pili mwanzoni.
Muda wa kupanda unatofautiana kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na majira ya mvua. Kwa mfano katika wilaya ya Morogoro tarehe za kupanda ni kuanzia februari 15 hadi Machi 15. Mkulima anashauriwa afuate kalenda ya muda wa kupanda kama anavyoshauriwa na bwana shamba wake.
Nafasi ya kupandia mahindi
Kupanda kwa nafasi ni kati ya njia bora za kilimo inayomwezesha mkulima kupata mazao bora. Hivyo ni muhimu sana kuzingatia kupanda kwa mistari na kufuata nafasi zinazoshauriwa na wataalamu wa kilimo. Zifuatazo ni nafasi za kupanda mahindi na idadi ya mbegu kwa kila shimo na kiasi cha mbolea (kwa vizibo vya soda) inayotakiwa kuwekwa kwa shimo:
- Kwa nafasi ya 90 sm X 30 sm, panda mbegu moja na uweke kizibo kimoja cha mbolea
- Kwa nafasi ya 90 sm X 25 sm, panda mbegu moja na uweke kizibo kimoja cha mbolea
- Kwa nafasi ya 90 sm X 50 sm, panda mbegu mbili na uweke vizibo viwili vya mbolea
Kupalilia
Ni muhimu shamba lipaliliwe baada ya mimea kuota ili kuondoa magugu. Magugu ni mimea hivyo hushindana na mimea iliyopandwa na mkulima kwa kunyonya virutubisho ardhini. Magugu yanaweza pia kuhifadhi wadudu na magonjwa yanayoweza kushambulia mimea iliyopandwa na hivyo kupunguza mavuno. Magugu yaweza kuondolewa wa palizi ya mkono (yaani) kung’olea (ikiwa magugu yapo mbali mbali sana) au kulima kwa jembe la mkono au kwa kutumia dawa/viuagugu (herbicides) hasa 2-4D.
Mbolea za kukuzia mahindi
Ni mbolea zinazotumika baada ya mimea kuota kwa lengo la kuikuza mimea ili itoe mavuno bora. Mara nyingi mbolea hizi zinatoa kirutubisho cha naitrojeni. zifuatazo ni mbolea za kukuzia na kiwango chake cha naitrojeni:
- UREA: 46% N
- Calcium Ammonium Nitrate, CAN: 23% N
- Sulphate of Ammonia, SA: 21%
Urea inakirutubisho cha naitrojeni (N) kwa kiwango kikubwa na watu wengi wanauzoefu nayo. Vilevile bei yake ni nafuu ikilinganishwa na mbolea zingine za kukuzia. Mbolea hii iko katika hali ya chengachenga za mviringo (granules) za rangi nyeupe. Kiwango cha urea ni nusu kizibo cha soda kwa kila shina. Mbolea hizi hazidumu kwenye udongo kwa muda mrefu kwa hiyo huwekwa shambani wakati mimea inapokuwa na mahitaji makubwa ya kirutubisho cha naitrojeni na wakati udongo una unyevunyevu na shamba halina magugu.
Pia wakulima hutumia mbolea za kukuzia zinazopatikana kwa bei nafuu kama vile BOOSTER (foliage nitrogeneous fertilizers) ambayo hupigwa kwa kunyunyizia katika majani ya mmea kila baada ya wiki 3, kwa mara 2-3 mpaka mahindi kuvunwa. Kiwango cha kupiga ni mchanganyo wa mls 50-80 ktk lita 15 za maji. Mbolea za kukuzia huwekwa kuzunguka kila shina la mimea au pande mbili au tatu au nne za kila shina. Cha muhimu ni kwamba mbolea isirundikwe sehemu mmoja. Minjingu Mazao (kg 50/ekari = gramu 10kwa shimo) pia yaweza tumika kwa kukuzia, hivyo mkulima yko huru kuchagua kulingana na uwezo na upatikanaji wake.
Sasa unaweza kujipatia Kitabu (PDF) cha Mwongozo wa kilimo cha Mahindi sasa hivi kwa bei nafuu sana. Kitabu hiki kimeboreshwa zaidi kwa ushauri wa kitaalam, mapendekezo ya kiasi, na aina za mbegu bora, mbolea na viuatilifu vya kutumia pamoja na mchanganuo wa bajeti ya kilimo na faida. Bofya hapa kukipata ndani ya Whatsapp au bofya hapa kukipata kwa email.
Viwango Vya Mbolea Za Kukuzia Vinavyoshauriwa
Kiwango kinachopendekezwa ni kilo 60 naitrogeni kwa hektari, ambacho ni sawasawa na kiasi cha mifuko miwili ikiwa utatumia UREA. Hata hivyo mbolea zingine kama SA inaweza kutumika kama kuna mahitaji ya salfa. Hivyo basi utumie mifuko mitatu kwa hekta ambayo ni sawa na mfuko mmoja kwa ekari. CAN inaweza kutumika kama kuna mahitaji maalum ya nitrate na ammonium na endapo utaitumia basi mifuko minne na nusu itatosha kwa hekta, ambapo kwa ekari moja utatumia mifuko miwili tu.
Kwenye mahindi mbolea ya kukuzia inawekwa baada ya palizi ya kwanza ambayo ni kama wiki tatu mpaka wiki nne baada ya kupanda. Kwa kila mmea mmoja weka kiasi hiki cha mbolea:
- UREA: kizibo kimoja cha soda
- CAN: vizibo viwili vya soda, na
- SA: kizibo kimoja cha soda
Mambo Muhimu Ya Kuzingatia
Kuweka mbolea: Sehemu za nchi ambazo muda wa kukua mahindi ni mrefu (zaidi ya miezi mitatu), ni vyema kuweka mbolea za kukuzia mara mbili, yaani nusu ya kiwango kinachopendekezwa baada ya mwezi mmoja, na kurudia tena (kutumia nusu iliyosalia) baada ya wiki tatu.
Kupalilia: Katika kilimo cha mahindi, ni muhimu shamba lipaliliwe siku 14 hadi 21 baada ya mimea kuota kufuatana na hali ya shamba wakati wa kupanda. Wataalamu wanashauri kwamba katika kilimo cha mahindi, shamba lipaliliwe mara 2-3, kufuatana na hali ya magugu katika shamba.
– Utafiti unaonyesha kwamba, shamba la mahindi ambalo halijapaliliwa linaweza kupunguza mavuno kwa asilimia 60 hadi 100 ya mavuno yanayotarajiwa. Hata kama mkulima atatumia mbegu bora, aina na kiasi cha mbolea zinazoshauriwa, kupanda kwa mstari pamoja na mbinu nyingine bora zinazoshauriwa, bila kupalilia hali hii itaathiri mavuno yake.
KUDHIBITI MAGONJWA NA WADUDU WANAOSHAMBULIA MAHINDI
Magonjwa Yanayoshambulia Mahindi
i) Maize streak virus
Dawa/Kudhibiti: Mbegu bora inayostahimili ugonjwa, kupanda mapema, kung’oa mimea iliyoathirika ama kunyunyiza dawa za kuua ‘vectors’ kama vile inzi weupe (white flies).
 |
| Maize streak virus |
ii) Smut (Fugwe)
Dawa/Kudhibiti: Tumia Helerat ukifuata maagizo kamili.
 |
| Ugonjwa wa fungwe kwenye mahindi |
iii) Cob rot (kuoza kwa mhindi)
Dawa/Kudhibiti: Tumia mbegu zinazostahimili kuoza.
 |
| Muhindi uliooza |
Wadudu Na Wanyama Wanaoshambulia Mahindi
Ni wadudu aina ya funza ambao hutokana na Nondo.Hushambulia mahindi kwa kula majaniyake pamoja na shina. Wadudu hawa huangamizwa/kudhibitiwa kwa njia zifuatazo;-
- Kuondoa vichaka karibu na shamba
- Kunyunyizia sumu za asili kama vile Mwarobaini majuma mawili ya mwanzo.
- Kunyunyizia sumu za viwandani endapo wadudu wameanza kuonekana kama vile Karate 1ml/1L
 |
| Viwavi jeshi |
b) Funza wa Mabua (Maize Stalk Borer)
Funza wa mabua hutoboa shina la mahindi na kusababisha kudumaa kwa mahindi.
- Matundu, ungaunga kama wa msumeno huonekana kwenye majani yaliyoathiriwa.
- Mashambulizi huanza juma la pili hadi la tatu baada ya mahindi kuota.
- Njia za kudhibiti zinazotumika
- Kuchanganya mahindi na mazao jamii ya mikunde km vile maharagwe
- Kung’oa mahindi yaliyoshambuliwa
- Sumu za asili mwarobaini
- Sumu za viwandani km vile Karate. pia waweza tumia Malathion, sumithion, vumbi ya cymbush au Sevin 5G na ufuate maagizo kamili.
 |
| Funza wa mabua |
c) Cutworms (Vikata Shina)
Dawa/Kudhibiti: Tumia Dragnet FT na ufuate maagizo kamili.
d) Wanyama waharibifu
Kudhibiti: Kuwatishia na kuwafukuza wanyama.
Ili mkulima aweze kupata mazao mengi na bora inashauriwa kutumia dawa za kuzuia magonjwa na wadudu washambuliao mimea na njia zinginezo.
 |
| Nyani |
KUVUNA, KUKAUSHA, KUSAFISHA NA KUHIFADIHI
Kuvuna
Mahindi yako tayari kuvuna wakati kikonyo kimekuwa dhaifu na mahindi yanaangalia chini. Mahindi yakishakauka vizuri yanatenganishwa na bua halafu majani ya mhindi kutolewa.
Kukausha
Kama mahindi hayajakauka vizuri hukaushwa zaidi katika juani siku 3-4 ili kupunguza unyevunyevu kufikia kiwango kinachofaa kwa kuhifadhi (14%). Ni muhimu mahindi yakauke vizuri ili yasioze yakiwekwa ghalani. Ili kujua kama mahindi yamekauka vizuri, tia mahindi kadhaa kwenye chupa ya soda iliyokauka na uongeze kiganja kimoja cha chumvi. Tingisha chupa halafu uwache itulie kwa dakika tatu. Chumvi ikikwama kando ya chupa, basi mahindi hayajakauka vizuri.
Kusafisha
Mahindi yaliyokauka vizuri hupepetwa na vilevile mahindi mabovu huondolewa.
Sasa unaweza kujipatia Kitabu (PDF) cha Mwongozo wa kilimo cha Mahindi sasa hivi kwa bei nafuu sana. Kitabu hiki kimeboreshwa zaidi kwa ushauri wa kitaalam, mapendekezo ya kiasi, na aina za mbegu bora, mbolea na viuatilifu vya kutumia pamoja na mchanganuo wa bajeti ya kilimo na faida. Bofya hapa kukipata ndani ya Whatsapp au bofya hapa kukipata kwa email.
Kuhifadhi
Mahindi huhifadhiwa ghalani baada ya kuwekwa viatilifu vya kuzuia bungua wa mahindi Njia za kisasa za uhifadhi hutumiwa kama vile matumiz ya ACTELLIC SUPER DUST katika uwiano wa 1kg kwa gunia 5-10 za ujazo wa 100kg. Kiatilifu kingine ni actellic solution katika rate ya 5mls katika gunia moja la kg 100. Njia nyingine ya kienyeji katika kuhifadhi mahindi ni kuweka juu ya ghala ambalo chini yake kuna jiko la kupikia ambalo hutoa moshi unaotumika kufukuza na kuua wadudu.
Mwisho wa makala yetu. Tafadhali weka usiache kuweka comment yako hapa chini.
Nimekukusanyia baadhi ya makala muhimu, bofya kuzisoma:
Safi kijana
Keep it up
Shukran sana brother, nafurahi kuona unanishika mkono mdogo ‘ako
Namba yako ya simu please
0626464191 niunge whtspp
Tunawategemea katika kilimo hongera sana
Ahsante. Endelea kuwa nasi
Big work
Asante sana kwa Somo zuri na Mungu akubariki,
Naomba unisaidie kujua makadilio ya
Mavuno( kiasi gani ) kwa hekari moja??
Pia ukiitaji ushauri piga simu
Namba 0655570084
Hekari moja ya weza kuzalisha magunia mangapi?
Hekali moja unwez kubuna kias gan Cha mahindi
Kuna tofaut gan kati ya hekar na hekta?
Hakuna tofauti. Hekari = Hekta
Labda anamaanisha, eka na hetra
nashukuru mkuu kwa elim bora
Endelea kuwa nasi!
Asante kwa elimu nzuri
Endelea kuwa nasi
Asante kwa elimu nzuri, Mungu aendelee kukujalia afya na maarifa zaidi
Aamin. Allahuma aamin!
Shukulan sana brother,
But can we have geographical distribution of seeds according to zones/regions
Can we do that?
Naomba ushauri nilikodi shamba katika eneo lenye udongo mwekundu lakin baada ya mazao kuota yamedumaa chini ndipo nikagundua hakuna rutuba sehemu hiyo, Sasa nimeshauriwa nitumie booster hebu nisaidie mtaalamu mbolea nzuri ni ipi
Tumia mbolea ya Urea kwanza, matokeo yake ndio yatakupa muongozo wa nini cha kufanya baadaye.
Naomba kujua tofauti Kati hekari na hekta. Je hekari moja iliyoboreshwa hutoa gunia ngap?
Hekari (au hekta) moja ni sawa na ekari mbili na nusu.
Eneo la hekta moja la mahindi linaweza kutoa tani 4 mpaka 5 kwa mahindi ya kawaida (OPV) au tani 6 mpaka 7 kwa mahindi ya mbegu chotara.
Mkuu mimi nimepata kiu kubwa sasa ya kuanzisha kilimo mwaka huu kikubwanilichonufaika hapa nikutumia wataalam wa kilimo hakika naamini nitafikia ndoto ya mkulima mkubwa.
Samahan naomba kuuliza ukanda wa tanga hsa mkata ni mbegu gani nzuri yamahindi ina ustaw mzr na mazao mengi
Dkt 777 itakufaa maana ni mbegu ya muda mfupi
Nimejifunza mengi sana, mbegu gani ni bora ukanda wa ziwa
Nimepata maarifa kupitia makala hii, ahsante Sana
Masomo haya ni mazuri sana, asante kwa elimu nzuri sana.
Nimejifunza kitu kizuri sana .Asante
Nashukuru Kwa elimu
Kijarida kizuri
Ahsante kwa elimu
Asante kwa elimu muhimu sana
asante
asante,pia naomba kujua ekari moja ina uwezo wa kutoa mavuno gunia ngapi za debe sita?
Naomba ushauri namna kupanda mbegu aina ya mtu chapa ngamia nafasi ya shimo kwa shimo na je ekeri moja inatosha kg ngapi
Naomba ushauri namna kupanda mbegu aina ya meru chapa ngamia nafasi ya shimo kwa shimo na je ekeri moja inatosha kg ngapi
Habali naitwa ibrah nipo mkoa wa Rukwa nahitaji kulima mahid nitumie mbegu gan nzuri sijawah kulima kabisa
Naomba ushauri Nina shamba Huwa linavamiwa na maji mara Kwa mara na kutwama humo shambani je ni zao Gani naweza kulima linaweza kumudu hata kama Kuna maji mengi
Mpunga unafanya vizuri kwenye maeneo yanayotuamisha maji, fikiria hilo
Shukrani:
Makala ni nzuri inayofundisha especially kwa Mimi ambaye nataka kuanza kuingia kwenye biashara ya kilimo.
Maoni yangu:
Kuwepo na Data base ya Mabwana shamba wa nchi nzima na mawasiliano yao ili endapo mkulima anapokutana na changamoto kwenye Mradi wake aweze kuwasiliana nao Moja kwa Moja kulingana na mkoa alipo.
Asanteni sana
0754274752
0715274752
Ahsante sana kwa maoni yako. Tunaliweka kwenye To-do list hili jambo. Endelea kuwa nasi
Hongereni sana kwa elimu nzuri mnayoitoa, kwa sasa kilimo darasa ni muhimu sana katika nchi yetu.
Ahsante sana. Endelea kuwa nasi
Nimependa sana somo liko safi sana nimepata pa kuanzia
Endelea kuwa nasi, na usiache kushare makala hii
Nmeenunua mbolea ya OCP ratio 11:22:21 kwa mahindi je inafaa maana yaramila (23:10:5) niliikosa mwanza mjini
Niunge kwenye group 0755262488
Mahindi yako vizuri mwanza mko seems gani
Tunapatikana Morogoro boss
Ushauri wenu unatusaidia sana wakulima
Tunafurahi kuwa msaada kwako
Elimu hii nimeioenda
06923329
Asante kukutupatia elimu ya kilimo
Thank you for an education
Nimefurahishwa na ufafanuzi huu juu ya kilimo Cha mahindi,
Nahitaji kuanzisha kilimo Cha mahindi mkoani dodoma eneo la kibaigwa je nimwezi upi unafaa zaidi kupanda mahindi?
Mda sahihi wa kupanda Mahindi hutegemea na aina ya mbegu pamoja na hali ya hewa , kwani tuna mbegu za mda mrefu wa kati na mfup mbegu za mda mrefu hupandwa kuanzia kumi tareh 25 ad wa kumi na moja tareh 15 kutegemea na msimu , za mda wa kati hupandwa kuanzia mwez wa kumi na ad wa kwanza , za mda mfup wa kwanza ad wa pili, by [email protected]
Mungu akubariki sana tunajifunza mengi kupitia hii tovuti
Napenda kilimo Cha kisasa
Naomba kuwa sehemu ya wanao jifunza kwenye mazao ambayo nitakuwa nayalima kwa wakati huo. Kwa sasa nipo kwenye mahindi na tikiti na vitunguu maji. Nahitaji kujifunza kwako kiongozi
Maelekezo mazuri ila mm nalima mahindi pwani na ninalima kuanzia Juni na July aridhi na kua na unyevunyevu mvua hainyeshi uwekaji wa mbolea ya chenga inawezekana?
Nice
Napenda Sana kilimo hata mm nataka mkulima mkubwa nifanyajeee??
nahitaji vitabu
Unahitaji vitabu gani boss? Huu hapa mwongozo wa kilimo cha mahindi. Na vingine vinapatikana hapa.
kilimo niuti wamgongo
Asante nimejifunza mengi,nitaboresha kilimo changu.