Unapoanzisha mradi wa kilimo biashara, unatarajia mwisho wa siku uumalize kwa kupata faida, sasa basi leo nataka nikufahamishe mambo makubwa mawili unayotakiwa kuyajua kabla hujaanza mradi wako wowote wa kilimo.


Habari ndugu msomaji wangu, na pole kwa shughuri mbalimbali za ujenzi wa Taifa. Wiki iliyopita nilikuandikia makala inayokufahamisha Kilimo bora cha zao la muhogo lakini leo nimekuletea kitu cha tofauti kidogo. Unapoanzisha mradi unatarajia mwisho wa siku uumalize kwa kupata faida, sasa basi leo nataka nikufahamishe mambo makubwa mawili unayotakiwa kuyajua kabla hujaanza mradi wako wowote wa kilimo.


Mambo-unayotakiwa-kuyafahamu-katika-kilimo-biashara

Jambo la kwanza: Hatua kwa hatua za utunzaji wa zao (Farming master-plan)

Katika kilimo biashara, hili ni jambo la kwanza na muhimu sana kulifahamu. Farming master-plan ni muongozo wa shughuri zote unazotakiwa kuzifanya katika kilimo chako tangu kuandaa shamba mpaka kuvuna.

Hii ijumuishe shughuri kama kupanda, kudhibiti magugu, uwekaji wa mbolea na kupulizia madawa ya wadudu na magonjwa. Unatakiwa kujua shughuri hizi zote, muda wa kuzifanya, namna ya kuzifanya na mahitaji yake ili uzifanye.  

Kwa mfano uwekaji wa mbolea: wakati gani uweke? kiasi gani? uwekeje? Unatakiwa ufahamu haya yote kabla hujaanza mradi wako wa kilimo ilii usipate usumbufu wakati wa utekelezaji.


Jambo la pili: Makadirio ya Gharama za Uzalishaji na faida

Hili ni jambo lingine muhimu sana. Naamini unapofanya kilimo biashara hujaamua kulima ili ujifurahishe tu, unalima ili upate faida. Hivyo basi unatakiwa ujue mradi wako utakugharimu kiasi gani katika utekelezaji wake na mwisho wa siku utakulipa kiasi gani? Pengine hutopata gharama halisi lakini ni lazima ufahamuu japo makadirio ya gharama ili kwanza uweze kujipanga lakini pia usikwame katika utekelezaji wa mradi wako.

Kwanini ni muhimu kufahamu mambo haya?

  1. Utajua mahitaji muhimu unayotakiwa kuwa nayo kabla hujauanza mradi wa kilimo 
  2. Utapata fursa ya kuuona mradi wako katika hatua mbalimbali hata kabla hujauanzisha
  3. Utaweza kujua makadirio ya gharama za uzalishaji na faida tarajiwa 

Kwa hiyo nikunasihi ndugu yangu usianzishe mradi wako wa kilimo mpaka ujiridhishe kuwa una ufahamu wa mambo haya mawili.


Mogriculture Tz katika kuhakisha kuwa tunakurahisishia kilimo biashara, tunakuandalia miongozo miwili inayogusa vilivyo mambo hayo mawili kwa kila zao. Miongozo yenyewe ni Farming master-plan (Muongozo wa shughuri za tunzaji wa zao) na Production cost and benefit analysis (Mchanganuo wa gharama za uzalishaji na faida).

Gharama ya kila muongozo kwa kila zao ni TZS 5000 tu; yaani master-plan TZS 5000 na Mchanganuo wa gharama TZS 5000! Mpaka sasa miongozo iliyopo tayari ni kwa mazao ya Mahindi na Maharage na mingine bado tunaifanyia kazi. Unaweza kuwasiliana nasi hapa.

Hiki ndicho nilichokuandalia kwa leo na natumai utakuwa umefaidika nacho. Kabla hujamaliza, nimekuchagulia baadhi ya makala ambazo nimeona zisikupite;

Katika kilimo biashara, je kuna jambo lingine mkulima anapaswa kulifahamu na sijaeleza hapa? Tujuze kwenye comments.

0 0 vote
Article Rating

Mtalula Mohamed

I like blogging. In order utilize my profession I chose to share, to blog, a few tips and tricks about farming and agriculture to anyone interested.

Subscribe
Notify of
guest
7 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
baraka john
baraka john
2 years ago

Kazi nzuri mno,Ahsanteni sana.

dotto shauri
dotto shauri
2 years ago

Mwanza wilaya za sengerema na geita pia inakubali san

Philemon Gobre
Philemon Gobre
2 years ago

ahdanteni sana kiukweli nimejifunza sana mazuri leo kutokana na makala haya

Imma Mutty
Imma Mutty
2 years ago

Nawashukuru Sana ktk mchango wenu wa uendelezaji wa kilimo chenye tija kwa Mkulima.ningependa kujua nimikoa ipi iliyokwisha kupimwa na wataalam kwa kuzalisha kilimo cha muhogo?

error: Content is protected !!
7
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x

Join Our Farming Community