Aina-mpya-za-mbegu

Aina 29 Mpya za Mbegu za Mazao

Habari njema kwa wakulima…

Kamati ya Taifa ya Mbegu (National Seed Committee) imeidhinisha matumizi ya aina 29 za mbegu mpya za mazao mbali mbali ya kilimo.

Mazao hayo ni mahindi, mpunga, alizeti, karanga na chai. Hatua hiyo ya Kamati inalenga kuongeza tija na kipato kwa mkulima.

Aina-mpya-za-mbegu

Kuidhinishwa kwa aina hizo za mbegu kunafuatia mapendekezo yaliyofanywa na Kamati ya Taifa ya Kupitisha Aina Mpya za Mbegu za Mazao (The NationalVariety Release Committee) katika kikao chake kilichofanyika makao makuu ya Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Dar-es-saalam tarehe 16 na 17 Machi 2016.

Jifunze zaidi kuhusu mbegu bora za mazao;

Aina hizi mpya za mbegu zimepitishwa baada ya kufanyiwa utafiti na kugundulika kuwa zina sifa zifuatazo:

  • Kutoa mavuno mengi
  • Kustahimili ukame
  • Ukinzani dhidi ya magonjwa na wadudu
  • Kukomaa mapema na
  • Kupendwa na wakulima.

Kati ya aina hizo mpya za mbegu, kuna aina 16 za mbegu za mahindi, 2 za mbegu za mpunga, 4 za mbegu za alizeti, mbegu za karanga 3 na 4 za mbegu za chai. Zipo pia mbegu 19 za mihogo.

Orodha ya aina mpya za mbegu za mazao

TAASISI/KAMPUNIZAOAINA YA MBEGU
Kituo cha Utafiti SelianiMahindiSELIAN H215
Kituo cha Utafiti NaliendeleKarangaNARINUT 2013
NACHI 2013
KUCHELE 2013
Kituo cha Utafiti IlongaMahindiWE4102
WE4106
WE4110
WE4114
WE4115
Kituo cha Utafiti TumbiMahindiT104
T105
Kituo cha Utafiti Chollima DakawaMpungaCH-SAT01
CH-SAT09
Taasisi ya Utafiti wa Chai TanzaniaChaiTRIT201/16
TRIT201/43
TRIT201/44
TRIT201/55
Sunflower Development Company (SDC)AlizetiNSFH36
NSFH145
Advanta Seed Company LtdAlizetiAGUARA 4
HYSUN 33
Meru Agro-Tours & Consultancy Co. LtdMahindiMERU LISHE 503
MERU LISHE 511
IFFA Seed Co LtdMahindiKASPIDI HYBRID
KISONGO HYBRID
Krishna Seed Co LtdMahindiKRISHNA HYBRID-1
KRISHNA HYBRID-2
Aminata Quality Seeds & Consultancy LtdMahindiNATA H 401
NATA K8

Mbegu hizo zimefanyiwa utafiti wa kina na vituo vya utafiti vya Umma na sekta binafsi hapa nchini. Sifa za aina hizo mpya za mbegu zilizoidhinishwa na Kamati ya Taifa ya Mbegu zimeambatanishwa hapa.

Aina hizo za mbegu zitaanza kuzalishwa na makampuni mbalimbali ya uzalishaji mbegu pamoja na Wakala wa Taifa wa Mbegu za Kilimo (Agricultural Seed Agency – ASA).

Lengo ni kuzifikisha aina hizo mpya za mbegu bora kwa wakulima kuanzia msimu wa 2017/2018.

Imetolewa na: Mh. Mwigulu Mchemba, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Pls share this post

Farming Tips and Tricks

If you like farming you will definitely love our contents. Join us now

14 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

  1. Nimeona maelekezo mbalimbali juu ya uzalishaji wa mazao ya mbogamboga na matunda je naweza kupata link ya kujua bei ya mazao hayo ya kila siku?

  2. Mimi nataka kuanza kulima matikiti maji nipo pwani, naomba kujua mbegu zipi ni bora kulimia kupata mazao mengi kwa shamba la nusu Hekta pia naomba kujua mbegu punje moja inaweza kutoa matikiti maji mangapi. Ahsante

  3. Aina za mbegu zimekua nyingi natofauti unapoenda katika maduka ya pembejeo unaweza uziwa mbegu ambayo siobora tena kwagarama ukija upande wa mbolea inakua changamoto hili kama nyie wataalamu mmeliwekaje maana cy kila mtu atapata elimu