Utangulizi
Zao la Alizeti hutatambulika kitaalamu kama Helianthus Annus na hulimwa kwa wingi karibu maeneo yote nchini Tanzania katika nyanda za kaskazini, kati, mashariki pamoja na nyanda za juu kusini hasa katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara na Rukwa.
Hii inatokana na uwezo wa alizeti kustawi vizuri katika mazingira mengi tofauti bila ya kuwa na utofauti mkubwa katika uzalishaji wake.
Asili ya zao hili ni nchini Marekani ambako lilienea katika maeneo ya Ulaya na baadae kusambaa sehemu nyingine za dunia ambapo kwa sasa Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa uzalishaji wa alizeti nyuma ya Afrika ya kusini.
Tabia za mmea wa Alizeti unazopaswa kuzijua
- Mmea wa alizeti una mizizi mirefu yenye urefu sawa au zaidi ya urefu wa shina kwenda juu. Urefu wa mizizi yake unaweza kufikia mita 1 hadi 2 kwenda chini ambapo hukoma kukua baada ya kutoka kwa ua.
- Ua kubwa la alizeti hutambulika kwa jina moja kama “kichwa” ambalo ukubwa wake huanzia sm 15 hadi 30. Ndani yake huwa na mkusanyiko wa maua madogo madogo yanayokaa kwa pamoja kama duara juu ya kombe kubwa ambapo kichwa kimoja kina kadiliwa kuwa na maua madogo 800 hadi 3000 na kila ua dogo moja lina uwezo wa kutengeneza mbegu.
- Katika kichwa cha alizeti kuzunguka kombe kuna maua petali yenye rangi ya manjano iliyokolea ambayo kazi yake kubwa ni kuvutia wadudu wachavushaji kama vile nyuki na vipepeo.
- Mbegu za alizeti huanza kutengenezwa katika kichwa kuanzia siku 10 hadi 15 tangu kutoka kwa maua.
- Kichwa kikubwa cha alizeti kina uwezo mkubwa wa kutengeneza mbegu ukilinganisha na kichwa kidogo. Kwa mfano kichwa chenye ukubwa wa sm 30 kinaweza kuzalisha gramu 19 hadi 20 za mbegu wakati kile chenye ukubwa wa sm 16 kinaweza kuzalisha hadi gramu 54.
Matumizi ya Alizeti
Zao la Alizeti hulimwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali ambapo baadhi yake ni kama vile kutengeneza mafuta, kulishia mifugo na matumizi ya viwandani.
- Kutengeneza Mafuta
Mbegu za Alizeti zinapokamuliwa hutoa mafuta yanayoweza kutumika kwa matumizi mbalimbali hasa kupikia. Wataalamu wengi wa afya wanapendekeza matumizi ya mafuta ya alizeti katika mapishi kwa sababu hayana lehemu (cholesterol) na hivyo ni salama kiafya hasa yanapotumika vizuri.
Kwa sababu hiyo mafuta yanayotokana na alizeti yamekuwa na soko zuri na hivyo biashara yake ni njia nzuri ya kumwongezea mkulima na mfanyabiashara kipato.
- Kulishia Mifugo
Mashudu yanayotokana na alizeti baada ya kukamua mafuta ni chakula kizuri kwa kulishia mifugo kama vile ng’ombe wa maziwa, mbuzi, nguruwe, kuku au sungura kwa sababu yana kiasi kikubwa cha protini na mafuta na kiasi cha nyuzi nyuzi muhimu kwa mmeng’enyo wa chakula kwa wanyama.
- Matumizi ya Viwandani
Mafuta yanayotokana na alizeti pia yanaweza kutumika katika utengenezaji wa sabuni, rangi na vipodozi mbalimbali.Vilevile viwanda vya kutengeneza karatasi hutumia baadhi ya sehemu za mmea wa alizeti kama malighafi katika utengenezaji wa karatasi.
Mifumo ya kilimo cha Alizeti
Ukiacha mfumo wa kilimo cha zao moja shambani kitaalamu mono cropping tutakao uzungumzia kwa kina katika somo hii, kuna aina nyingine tofauti za mifumo ambayo inaweza kutumika katika kilimo cha alizeti. Mifumo hiyo ni kama ifuatavyo…
- Kilimo Mseto
Alizeti pia huweza kulimwa katika mfumo wa kilimo mseto ambapo zao la mahindi ndilo linalopendekezwa hasa kulimwa mseto na alizeti kwa sababu mazao haya mawili yana mfanano mkubwa katika matunzo na muda wa ukuaji hadi kukomaa.
Katika kilimo mseto cha alizeti na mahindi panda mbegu za mahindi na alizeti katika mistari iliyo katika mpangilio wa mistari miwili miwili au mmoja mmoja ya alizeti na mahindi katika nafasi ya sm 75 kwa sm 30 katika shamba moja.
- Kilimo cha mzunguko wa mazao
Tabia ya mizizi ya alizeti kukua kwenda chini hadi kufikia kina kirefu cha udongo imeipa sifa zao hili kutambulika kama zao mahususi kwa kilimo cha mzunguko wa mazao. Hii ni kutokana na uwezo wake wa kufikia maji na virutubisho ambavyo haviwezi kufikiwa na zao lolote lile litakalopandwa katika mzunguko na zao la alizeti.
Inapendekezwa zao hili lilimwe katika mzunguko na mazao ya mahindi na mtama ili kukata mzunguko wa maisha ya vimelea vya magonjwa na wadudu wanaoshambulia zao la alizeti.
- Kilimo cha alizeti kwa Mchavusho wa Nyuki
Huu sio mfumo rasmi wa kilimo cha alizeti lakini ni mbinu muhimu inayoweza kutumika ili kuongeza uzalishaji wa alizeti. Kwa kawaida nyuki ndio wachavushaji wakuu wa maua ya alizeti kando ya vipepeo na wadudu wengine warukao ambapo mbegu za alizeti huzalishwa baada ya uchavushaji wa maua madogo yaliyo katika vichwa vya alizeti.
Kwa sababu hiyo ili kuongeza uzalishaji unaweza kulima alizeti karibu na maeneo yenye mizinga ya nyuki ambapo kwa njia hii unaweza kupata faida kubwa kwani mavuno ya alizeti huongezeka maradufu hata kwa mbegu chotara ambazo nyingi maua yake hufanya mchavusho binafsi (self-pollination).
Mbinu hii pia hutumiwa na wafugaji wa nyuki walio wengi katika nchi zilizoendelea ili kuongeza uzalishaji wa asali kwani kutokana na maua ya alizeti asali nyingi na nzuri hutengenezwa katika mizinga ya nyuki. Kwa Tanzania baadhi ya sehemu za mikoa ya Tabora na Kigoma wafugaji wa nyuki wamekua wakiitumia mbinu hii.
Mazingira yanayostawisha alizeti
Udongo
Zao la alizeti hustawi vizuri katika udongo wa aina tofauti wenye rutuba, kina, uwezo wa kuifadhi maji vizuri na husiotuamisha maji. Hata hivyo udongo wa tifutifu hasa wenye rutuba ya kutosha na tindikali kuanzia pH 6.0 hadi 7.5 umeonyesha kufaa sana kwa kilimo cha alizeti.
Udongo wa kichanga katika maeneo yenye joto kali haufai kwa kilimo cha zao hili kwa kuwa aina hii ya udongo huwa na tabia ya kuweza kupata joto kwa urahisi na hivyo kuathiri uotaji wa mbegu za alizeti ambazo kwa kawaida hazihitaji joto jingi wakati wa kuota.
Kwa sababu hiyo basi ni vigumu kuepuka mapengo shambani ikiwa utapanda alizeti katika udongo wa kichanga hasa kwenye maeneo yenye joto kali.
Hali ya hewa
Alizeti ina uwezo wa kustawi na kufanya vizuri katika maeneo mengi yenye hali ya hewa tofauti hata katika maeneo yenye hali ya ukame. Hii huchangiwa na tabia ya mizizi yake ambayo huweza kukua kwenda chini kwa kiwango kikubwa hadi kufikia maji katika kina kirefu cha udongo.
Zao hili huweza kustawi katika maeneo yenye joto la nyuzi za sentigredi 15 hadi 34 lakini hustawi vizuri zaidi linapolimwa katika maeneo yenye joto la nyuzi za sentigredi 23 hadi 28.
Mvua na Mwinuko
Kilimo cha alizeti hukubali katika maeneo ya mwinuko tofauti hadi mita 2500 kutoka usawa wa bahari na yenye mvua za wastani kiasi cha mm 500 hadi 1000.
Maandalizi ya mbegu za alizeti
Aina za mbegu za alizeti
Alizeti zimegawanyika katika aina kuu mbili ambazo ni aina fupi na aina ndefu kama nitakovyoelezea hapo chini…
- Alizeti ndefu
Aina hii ya alizeti huweza kukua hadi kufikia urefu wa mita 1.5 hadi 2.5 ikijumuisha mbegu za asili na zilizotumika kwa muda mrefu ambapo baadhi ya mbegu za aina hii ni kama vile Zebra, Black, Record, Kilimo, Serena, Black-lulu, white na Jupiter.
Kwa kawaida aina hii ya alizeti huchukua siku 120 hadi 150 tangu zilipopandwa kuanza kuvunwa na uzalishaji wake ni hafifu ukilinganisha na mbegu za aina fupi.
- Alizeti Fupi
Aina hii hujumuisha mbegu chotara na zilizoboreshwa zenye uwezo wa kukua hadi kufikia urefu wa kimo cha mita 1.2 hadi 1.4. Alizeti za aina hii hutengeneza vichwa vidogo lakini huzaa mbegu nyingi na hivyo mavuno yake kwa kawaida huwa ni mazuri zaidi ukilinganisha na aina ndefu kwani kwa eneo la ekari moja kama utahudumia vizuri unaweza kupata mavuno ya alizeti sio chini ya gunia 16.
Aina hii pia huwa tayari kuvunwa baada ya siku 90 hadi 120 tangu kupanda kwa sababu hiyo hufaa sana kulimwa katika maeneo yenye vipindi vifupi vya mvua. Baadhi ya mbegu katika kundi hili ni kama vile, NSFH 36, NSFH 145, AGUARA 4 na HYSUN 33.
Uchaguzi wa mbegu bora za alizeti
Ni vyema kutumia mbegu zilizoboreshwa na kupendekezwa na wataalamu kutoka kwa wauzaji wanaotambulika kisheria ili kupata mavuno mazuri kwa kuwa nyingi huwa na tabia ya kuvumilia ukame, magonjwa na wadudu, kuzalisha mbegu nyingi na kutoa mafuta mengi.
Miongoni mwa mbegu bora za alizeti ni AGUARA 4 na HYSUN 33. Zingine ni NSFH 36, NSFH 145. Mbegu hizi ni chotara na mavuno yake ni bora Zaidi ukilinganisha na mbegu za kawaida (OPV).
AGUARA 4
- Aina hii ni alizeti chotara.
- Inastawi katika mwinuko wa kuanzia ukanda wa chini hadi wa juu.
- Inakomaa mapema kwa wastani wa siku 102 hadi 109.
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 2.7 kwa hekta.
- Ina kiwango cha mafuta cha asilimia 46 cha mafuta.
HYSUN 33
- Aina hii ni alizeti chotara.
- Inastawi katika mwinuko wa kuanzia ukanda wa chini hadi wa juu.
- Inakomaa kwa wastani wa siku 98 hadi 106.
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 2.5 kwa hekta.
- Ina stahimili ugonjwa wa ubwiri unga (powdery mildew).
- Ina kiwango kikubwa cha mafuta cha asilimia 41.
NSFH 36
- Aina hii ni alizeti chotara.
- Inastawi katika mwinuko wa mita 100 hadi 1,800 kutoka usawa wa bahari.
- Inakomaa mapema kwa wastani wa siku 86 hadi 95.
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 3.4 kwa hekta.
- Ina kiwango kikubwa cha mafuta cha asilimia 40.
- Ina uwezo wa kujikinga na ndege kutokana na tabia ya kichwa chake kuelekea chini (bending characteristics).
NSFH 145
- Aina hii ni alizeti chotara.
- Inastawi katika mwinuko wa mita 100 hadi 1800 kutoka usawa wa bahari.
- Inakomaa mapema kwa wastani wa siku 84 hadi 94.
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 3.6 kwa hekta.
- Ina kiwango kikubwa cha mafuta cha ailimia 40
Kitu kingine cha muhimu unachotakiwa kukifahamu mapema kuhusu mbegu unayotaka kutumia ni muda ambao huchukua kukaa shambani hadi kukomaa. Hii itakusaidia kupanga vizuri ratiba ya upandaji itakayokuwezesha kuvuna alizeti wakati mvua zikiwa zimekata.
Kiasi cha mbegu kwa ekari
Unahitaji kg 2 za mbegu ya alizeti kupanda ekari moja kwa mbegu chotara. Na kiasi cha kilo 3 hadi 4 kwa mbegu za kawaida. Hii ni kutegemeana na nafasi ya kupandia na uotaji wa mbegu.
Je ungependa vitabu badala yake? Hivi hapa …
Upandaji wa alizeti
Msimu wa kupanda alizeti
Shamba la alizeti liandaliwe mapema mwezi mmoja kabla ya kupanda ili kuruhusu magugu na mabaki ya mazao kuoza vizuri. Kwa kilimo cha kutegemea mvua anza kutayarisha shamba katikati mwa mwezi Februari ili kuweza kupanda kati ya mwezi Machi na April wakati wa mvua za masika.
Vile vile unaweza kuanza maandalizi katikati mwa mwezi Agosti ili kuweza kupanda mwishoni mwa Septemba au mwanzoni mwa mwezi Oktoba wakati wa mvua za vuli.
Ratiba hii inaweza kutofautiana kidogo kati ya sehemu na sehemu kutegemeana na ratiba ya mvua na mabadiliko ya tabia ya nchi cha msingi shauriana na mtaalamu wa kilimo alie katika eneo lako kabla ya kuanza maandalizi.
Kwa kilimo cha umwagiliaji wakati wa kipindi cha kiangazi unaweza kuanza maandalizi muda wowote kulingana na mahitaji na soko unalolilenga.
Maandalizi ya shamba
Kulima shamba
Lima shamba kwa kutumia jembe la mkono, jembe la kukokotwa na wanyama, power tillers au trekta. Matumizi ya jembe la kukokotwa na wanyama, power tillers na matrekta hurahisisha shughuli ya kulima na kuifanya iwe na ufanisi kwani hukatua udongo vizuri na kuufanya uwe tifutifu.
Unapotumia jembe la mkono katika kulima hakikisha unakatua udongo katika kina cha kutosha sm 20 mpaka sm 30 na kulainisha mabonge. Udongo uliokatuliwa vizuri hupitisha hewa inayohitajika na mmea, hurahisisha ukuaji wa mizizi na kuhifadhi maji vizuri.
Kupima shamba (field layout)
Ni muhimu kuanza kupima shamba kabla ya kuanza kupanda ili kupata mistari ya mimea shambani iliyonyooka vizuri. Kabla ya kupima ni muhimu pia kujua mapema nafasi ya kupandia utakayoitumia. Hii itakuwezesha kupanga mistari katika mpangilio utakao kupendeza kama mistari miwili miwii au mmoja mmoja. Tumia Tape measure au kamba yenye vipimo kupima shamba huku ukiweka alama kwa kuchomeka mambo (pegs).
Jinsi ya kupanda alizeti
Muda wa Kupanda
Kwa ratiba yoyote utakayofuata kutegemeana na mazingira au maelekezo ya mtaalamu wa kilimo wa eneo uliopo hakikisha unapanda alizeti katika kipindi kitakacho kuwezesha kuvuna wakati mvua zikiwa zimekata kwa sababu mvua zinazoendelea kunyesha baada ya kukomaa kwa alizeti zinaweza kusababisha kuoza kwa vichwa na hivyo kusababisha hasara.
Nafasi ya Kupandia
Panda alizeti katika nafasi kuanzia sm 75 hadi sm 100 kati ya mstari na mstari na sm 30 hadi sm 50 kutoka shimo hadi shimo. Nafasi ya sm 75 kwa sm 30 ni pendwa zaidi.
Hata hivyo jambo la muhimu ni kuzingatia maelekezo ya mbegu husika juu ya nafasi ya kupandia inayopendekezwa.
Kuweka mistari
- Unaweza kupanda alizeti kwa kuweka mistari katika mpangilio wa mistari miwili miwili au mmoja mmoja.
- Unapotumia upanzi wa mistari miwili miwili inashauriwa kupanda alizeti katika mistari miwili kwa kuzingatia nafasi inayopendekezwa kisha acha nafasi ya sm 90 hadi mita 1 kabla ya kupanda mistari miwili mingine.
- Endelea kupanda kwa utaratibu huu hadi utakapo kamilisha kupanda katika shamba zima.
- Kwa utaratibu wa mstari mmoja mmoja unachotakiwa kufanya ni kuzingatia tu nafasi iliyopendekezwa kwa mbegu husika.
Hatua za Upandaji
Fuata hatua zifuatazo katika upandaji wa mbegu za alizeti shambani…
- Mwagia maji mengi shambani masaa kumi na mbili kabla ya kupanda mbegu ili kulainisha udongo na kurahisisha upanzi.
- Chimba mashimo ya kupandia yenye kina cha sm 3 hadi 5 katika nafasi iliyopendekezwa katika mpangilio wa mistari unaokupendeza.
- Weka viganja viwili vya mkono vya samadi iliyoiva katika shimo la kupandia kisha changanya na udongo kupata mchanganyiko mzuri. Vile-vile unaweza kuweka mbolea ya samadi au mboji kwa kusambaza shamba zima wiki mbili hadi tatu kabla ya kupanda ambapo kiasi cha tani 3 za samadi au mboji hutosha kwa eneo la ekari moja.
- Kwa mbolea ya kupandia kama DAP weka kifuniko kimoja cha soda katika kila shimo la kupandia kisha fukia mbolea kwa tabaka dogo la udongo litakalofanya mbolea na mbegu visigusane wakati wa kupanda kuepuka kuungua kwa mbegu. Kiasi cha kilo hamsini za mbolea ya DAP kinatosha kutumika katika eneo la ekari moja.
- Panda mbegu mbili za alizeti katika kila shimo, fukia kwa udongo mwepesi, shindilia na kisha mwagia maji.
Utunzaji Wa Alizeti Baada Ya Kuota
Kupunguzia miche
Ikiwa umepanda mbegu mbili au tatu katika kila shimo mimea inapofikia kimo cha sm 10 hadi 20 ng’oa mcme mmoja au miwili katika kila shimo na uache mmea mmoja wenye afya.
Hili linaweza kufanyika wakati wa kufanya palizi ya kwanza ambapo mimea iliyong’olewa kutoka katika shimo moja inaweza kupandikizwa katika shimo lingine ambalo mbegu zake hazikuota au lenye miche isiyo na afya nzuri.
Umwagiliaji
Kwa kawaida wakulima wengi wa alizeti nchini Tanzania hulima zao hili kwa kutegemea mvua kama chanzo kikuu cha maji lakini hii si sheria kwamba lazima ulime kwa kutegemea mvua kwa sababu unaweza kulima zao hili kwa kufanya umwagiliaji na kupata mavuno mazuri sana.
Zao la alizeti katika ukuaji wake huitaji maji hasa katika kipindi cha kutengeneza kichwa na kutoka kwa maua hadi kukomaa.
Kipindi hiki hakikisha shamba lako linapata maji ya kutosha na hatakama unalima kipindi cha msimu wa mvua mwagilia maji unapoona mvua zinalegalega au nusu ya unyevu wa udongo unapokuwa umepotea. Usiruhusu udongo wa shambani kukauka kabisa katika kipindi hiki cha ukuaji wa alizeti.
Kwa kilimo cha umwagiliaji unaweza kumwagilia shamba la alizeti kila baada siku mbili hadi tatu kutegemeana na hali ya hewa, udongo na njia ya umwagiliaji unayoitumia hadi vichwa vitakapokomaa. Cha msingi usiache udongo ukauke, bali mwagia maji angalau asilimia hamsini ya unyevu wa udongo unapokuwa umepotea.
Kuweka matandazo
Matandazo ya asili kama vile mabua ya nafaka, pumba za mpunga, maganda ya karanga na maranda ya mbao yanaweza kutumika kwa kazi hii. Lakini pia majani ya migomba yanafaa kuwa matandazo.
Matandazo husaidia kudhibiti magugu, kuifadhi unyevu na kuongeza rutuba katika udongo. Kwa matokeo mazuri katika udhibiti wa magugu weka matandazo kwa kuyatandaza katika udongo katika kina cha sm 10 mpaka 15 maeneo yote kuzunguka mashimo ya mimea.
Unapokuwa na matandazo ya kutosha shamba zima kwa kina kinachopendekezwa ni vyema kuyaweka baada ya kuchimba mashimo kabla ya kupanda au mara baada ya kupanda ili kudhibiti magugu katika hatua za awali za ukuaji wa alizeti na endelea kuongeza matandazo kadili kina kinavyopungua kutokana na kuoza.
Ikiwa una kiasi kidogo cha matandazo kutosha kuwekwa shamba zima katika kina kinachopendekezwa weka matandazo hayo mara baada ya kufanya palizi ya kwanza.
Kudhibiti magugu
Fanya palizi wiki 2 hadi 3 tangu kuota na rudia tena baada wiki 4 hadi 5 kutegemeana na hali ya magugu katika shamba.
Mimea michanga ya alizeti huathiriwa sana na magugu hivyo hakikisha shamba lako halina magugu katika kipindi cha wiki sita za mwanzo tangu kupanda.
Kipindi hiki ndipo alizeti hukua taratibu na hivyo hazina uwezo wa kushindana na magugu kupata maji na virutubisho vingine wala kichaka chake hakina uwezo wa kufunika ardhi kuzuia ukuaji wa magugu.
Kwa sababu hiyo kuacha shamba likiwa na magugu katika kipindi hiki kunaweza kuchangia kupunguza mavuno kwa kiasi kikubwa vinginevyo unaweza pia kuongeza mavuno kwa kiasi kikubwa ukimudu shamba kutokuwa na magugu wakati wa kipindi hiki.
Unaweza kufanya palizi kwa kutumia mikono, jembe dogo la mkono au dawa za viuagugu zinazopatikana katika maduka ya pembejeo za kilimo.
Dawa zinazoweza kutumika kufanyia palizi katika kilimo cha Alizeti
Kiambata amilifu | Muda wa kutumia | Aina ya magugu yanayo dhibitiwa | |
1 | 2,4-D (two four D) | Kabla ya kupanda | Magugu jamii ya mboga |
2 | Glyphosate (Round up) | Kabla ya kupanda | Magugu ya aina zote |
3 | Pendimethalin | Baada ya kupanda kabla ya kuota kwa magugu | Nyasi na magugu jamii ya mboga. |
4 | Metolachlor | Baada ya kupanda kabla ya kuota kwa magugu | Nyasi na baadhi ya magugu jamii ya mboga |
5 | Propaquizafop | Baada ya kuota kwa magugu na alizeti | Magugu jamii ya nyasi |
Kama utaamua kutumia madawa ya viuagugu inafaa sana kutumia dawa za kuua magugu baada ya kupanda kabla ya kuota ili kuwezesha shamba kutokua na magugu ndani ya wiki sita za kwanza za hatari ambazo kitaalamu hutambulika kama Critical Period for Weed Competition.
Katika kilimo mseto cha alizeti na mahindi baada ya kupanda usitumie dawa yenye kiambata amilifu cha atrazine ambacho kimekuwa kikitumika kwa palizi katika mfumo wa zao moja la mahindi vinginevyo unaweza kudhuru zao la alizeti ambalo lina tabia ya kuathiriwa na viambata amilifu vya kundi la Triazine (Triazine sensitive crop).
Badala yake unaweza kutumia dawa zenye kiambata amilifu cha Pendimethalin ambacho huweza kutumika katika palizi kwa mazao yote mawili bila kuathiri mimea.
Zingatia: Soma lebo ya chupa ya dawa kujua kiambata amilifu.
Mahitaji ya mbolea
Mbolea za kupandia
Tumia mbolea ya DAP wakti wa kupanda. Kiasi cha kg 50 kinatosha kwa ekari moja. Unaweza pia kutumia mbolea ya samadi. Hii iwekwe shambani wakati wa kuandaa shamba ili ichanganywe vizuri na udongo.
Kwa mbolea ya DAP weka kifuniko kimoja cha soda katika kila shimo la kupandia kisha fukia mbolea kwa tabaka dogo la udongo litakalofanya mbolea na mbegu visigusane wakati wa kupanda kuepuka kuungua kwa mbegu.
Mbolea za kukuzia
Katika eneo la ekari moja unaweza kutumia mfuko mmoja wa kilo 50 za Urea au mifuko miwili (kg 100) kwa mbolea ya CAN.
Weka mbolea ya kukuzia aina ya CAN au Urea mimea inapokuwa katika kimo cha usawa wa magoti sm 40 hadi 60 baada ya kufanya palizi ya kwanza.
Weka kiwango cha kizibo kimoja cha soda cha mbolea ya Urea (au vizibo viwili vya soda kwa mbolea ya CAN) kuzunguka shina sm 5 kutoka shina lilipo. Vilevile ni muhimu pia kuongeza mbolea yenye kirutubisho cha Boron ambacho upungufu wake umeonyesha kuathiri sana uzalishaji wa alizeti.
Wadudu na magonjwa ya alizeti
Magonjwa ya alizeti
Yapo magonjwa makuu mawili ‘yellow blotch’ na ‘Sclerotinia’.
Ugonjwa wa yellow blotch husababisha rangi kuwa ya manjano na muundo wa matawi na maua kuharibiwa.
Ugonjwa wa Sclerotinia (White Mold) hupelekea kuoza kwa mmea wote wa alizeti: yaani shina, matawi na hata kichwa cha alizeti.
Jinsi ya Kudhibiti
Ugonjwa wa yellow blotch hudhibitiwa kwa kuing’oa na kuchoma mimea iliyoathirikaa, aidha kunyunyizia dawa (diazinon) ili kuwadhibiti wadudu wanaousambaza. Tumia: Agrozinon 60EC, Bullet 600EC, Nogozone 60EC, n.k.
Kudhibiti ugonjwa wa Sclerotinia (White Mold), badilisha mimea shambani (fanya crop rotation) baada ya kila miaka 5.
Wadudu na ndege wa alizeti
Ndege na viwavi aina ya ‘African Bollworm’ ndiyo waharibifu hatari wa alizeti. Lakini pia wapo Sota na Panzi.
Viwavi (African Bollworm): hula majani ya kijani kibichi pamoja na mbegu na wanaweza kuharibu zao lote shambani.
Ndege hula mbegu za kwenye kichwa cha alizeti.
Cutworms na Panzi: Wadudu hawa hukata mashina ya mimea michanga inayoota. Na Panzi hula hata majani machanga ya mimea ya alizeti.
Jinsi ya Kudhibiti
Uharibifu kutoka kwa ndege waweza hupunguzwa kupitia kulinda na kuwafukuza.
Viwavi (African Bollworm) waweza kudhibitiwa kwa kunyunyizia madawa ya kuua wadudu kama vile Profecron, Karate, n.k
Ili kudhibiti Sota (cutworms) na Panzi (grasshoppers) tumia madawa yanayotoa harufukali yakuwafukuza. Kama vile Mupa force, na Karate.
Uvunaji Wa Alizeti
Muda wa kuvuna
Anza kuvuna alizeti pale ambapo asilimia 80 ya vichwa vya alizeti katika shamba vinapokuwa na rangi ya kahawia. Wakati huu mbegu huwa na unyevu chini ya asilimia 20 (asilimia 10 hadi 13).
Kutegemeana na aina ya mbegu iliyotumika alizeti huvunwa zikiwa na siku 90 hadi 150 tangu kupanda (rejea aina za alizeti).
Kuchelewesha uvunaji zaidi ya kipindi kinachopendekezwa kunaweza kupelekea hasara zinazoweza kujitokeza kutokana na ndege, kukwama kwa mbegu au kupukutika kwa kichwa kufuatia ukaukaji uliopitiliza. Vile-vile kuwaisha kuvuna kabla ya muda kunaweza kusababisha mbegu kuwa na maganda mengi na nyama kidogo.
Kukomaa kwa Alizeti
Alizeti huwa zimekomaa baada ya maua petali ya njano kuzunguka kichwa cha alizeti kunyauka na kupukutika pindi sehemu ya nyuma na pembeni ya kichwa inapokuwa imebadilika rangi na kuwa ya njano hadi kahawia.
Kawaida hatua hii huonekana wiki tano mpaka sita tangu kutoka kwa maua. Kipindi hiki mbegu za alizeti huwa zimejaa vizuri zikiwa na kiwango cha unyevu kinachokadiliwa kuwa asilimia 30 hadi 35.
Jinsi ya kuvuna alizeti
Andaa vifaa na vyombo vya kuvunia kama vile kisu, ndoo, makapu na magunia.
Wakati wa kuvuna kata mashina sm 10 chini ya vichwa vya alizeti kwa kutumia kisu na kuviweka katika makapu ya kuvunia. Kisha fungasha katika magunia na kusafirisha hadi nyumbani kwa ajili ya kukausha.
Kiwango cha mavuno
Shamba la alizeti huweza kutoa mavuno wastani wa magunia 8 hadi 12 (ya kg 65 @) kwa ekari kwa mbegu za kawaida. Kwa baadhi ya mbegu chotara mavuno huweza kufikia magunia 20 (ya kg 65 @) kwa ekari.
Mavuno ya alizeti yanaweza kuathiriwa na mambo yafuatayo…
- Aina ya mbegu
- Kiwango cha maji wakati wa uzalishaji
- Matunzo kama palizi na mbolea.
Matunzo Ya Alizeti Baada Ya Kuvuna
Kukausha na kupura vichwa
Kupura alizeti
Baada ya kuvuna kausha vichwa vya alizeti kwa kuvianika juu chini juani kwa kuvitandaza katika kina kisichozidi sm 30 kwenye mkeka au maturubai ambapo lengo kuu la ukaushaji ni kurahisisha upuraji.
Baada ya kukausha pura vichwa vya alizeti kwa kupiga taratibu na fimbo katika kichanja, mkeka au turubai ili kutenganisha vichwa na mbegu.
Kupeta na kupembua alizeti
Pepeta na kupembua mbegu za alizeti ili kuondoa, mawe, mabaki ya vichwa, mbegu zilizooza au kupasuka pamoja na wadudu. Upepetaji na upembuzi unaweza kufanywa kwa kutumia ungo au mashine za kupembulia.
Kupunguza unyevu mbegu za alizeti
Kukausha
Baada ya kupura na kupeeta alizeti, kausha mbegu za alizeti juani kwa kuzitandaza katika kichanja, maturubai au mikeka katika kina kisichozidi sm 4 kwa muda wa siku 3 hadi 5 ili kupunguza kiwango cha unyevu hadi kufikia kiwango kinachofaa kwa uhifadhi ambacho si zaidi ya asilimia 9.5.
Namna ya kutambua mbegu zilizokauka vizuri
Kiwango cha ukaukaji wa mbegu huweza kutambuliwa kwa kutumia njia za asili au njia za kitaalamu.
Kwa kutumia njia za asili unaweza kutambua ukaukaji wa mbegu kwa kutumia mikono ambapo unachotakiwa kufanya ni kufikicha kiasi kidogo cha mbegu katika mikono yako.
Mbegu zilizokauka vizuri zina muonekano wa kung’ara na wakati wa kuzifikicha maganda yake hutoka kwa urahisi. Vilevile mbegu kavu zinapomiminwa katika vyombo kama vile debe hutoa mlio mkali.
Njia za kitaalamu za kutambua ukaukaji wa mbegu zinahusisha matumizi ya kipima unyevu ambacho kwa kawaida mbegu zilizokauka vizuri kipimo huonyesha kiwango cha unyevu cha asilimia 8.
Kifaa maalum cha kupima unyevu wa mbegu
Kuhifadhi
Inapendekezwa kuifadhi mbegu za alizeti zikiwa na kiasi cha asilimia 8 za unyevu. Unyevu wowote zaidi ya asilimia 12 unahitaji ukaushaji. Pooza mbegu za alizeti kwa kuziweka kivulini kwenye hewa kabla ya kuzihifadhi ili zisije kuoza mara baada ya kuifadhiwa.
Asante sana kwa taaluma.
Mimi nahitaji mashamba naomba msada jamani ikiwezekana mwezi huu kama sijachelew.
Asante Kwa Makala nzuri sana.ila nahitaji kujua nitapataje viuagugu vya kuzuia kuota magugu Kwa zile wiki 6 za mwanzo(Metolachlor).
Asante
OK
Makala ni nzuri na inaelimisha. Je,ni magonjwa gani yanayoshambulia zao la alizeti na yanadhibitiwaje?
Somo zuri sana asanteni sana.
Makala ni nzuri na inaelimisha, natamani mngekua mnaweka na makadirio ya gharama zinazohusika kwenye uzalishaji, ingesaidia zaidi.
Nashukuru kwa makala nzuri iliyonielimisha vizuri,nashauri uwepo mpango maalumu wa kuwawezesha wakulima kupata zana za kilimo hasa planter ili kuwarahisishia wakulima ktk upandaji wa mazao mbalimbali,kilimo cha kisasa kinahitaji nyenzo kama hizo.
Nashukuru kwa darasa,lakini bado nina swali moja
1.Gunia moja linaweza toa lita ngapi za maduta?
Inategemea na aina ya mbegu,mbegu za ushavishaji huria hutoa kati ya lita 12-14,kama ikihudimiwa vizuri,mbegu chotara hutoa kati ya lita 16 -22 kwa gunia la kilo 75
Nimejifunza namna bora ya kulima alizeti, bila shaka nitazingatia yote mliyoyaeleza na pia nitashirikiana na wataalamu wa kilimo. Swali langu,je ni kiasi gani cha alizeti kinatoa lita moja ya mafuta?
Debe moja hutoa wastani wa lita 3-4 za mafuta.
Mmenifundisha kitu kikubwa ambacho sikukifahamu, kwani Mimi ni mdau na mpenda kilimo cha alizeti. Nipo mkoa wa Rukwa Nkundi.
jmagesa85@gmail.com
Ninashukuru kwa elimu ya zao la alizeti. Ni makala nzuri ambayo imenipa mwanga kuhusu kilimo cha alizeti. Ni matumaini yangu kuwa makala hii itakuwa msaada kwa kuwaongezea maarifa wakulima wa alizeti wazoefu na zaidi kwa wale wanaotaka kuanza kilimo cha alizeti kama mimi hapa. Kwa makala hii hakika sitakuwa mgeni pindi nitakapoanza kilimo cha alizeti.
Mm ni mkulima mdogo ambaye naanza kilimo mwaka uja cha alizeti ,somolenu zulisana nawashukuru sana.
Somo zuri Sana
Thanks for sharing
Marvelous article! Knowledgeable indeed.
The informations are so useful,
Especially for us beginners..
We still need you for more advice,
Incase there’s an application that is special for this program,it will be more better
Gunia moja ya arizet inatoa Lita ngapi
Nimeipenda sana hii elimu,I’m going to be the best farmer. Asante sana mtaalamu.
daaaaah nimefurahi sana kukutana na hii makala, maana nilipanda alizeti zangu february katikat sasa nikashangaa sana hazikuota, yaani wiki 2 zimeota kwa mbali mbali sana.. sasa nimejua sababu kwamba ziliungua na mbolea maana zilipanda kwa pamja… aiseee
sante hapa nimeelewa vizuri sana next time itakua kitaalamu zaidi.
ni ya yapi majira maZurich ya kulima a lifetime?
Nashukuru kwa elimu sad naenda kulima
tunashukuru sana kwa ushauri na makala safi, sasa mimi nataka nikalime kondoa ili niepukane zana za kuajiliwa maana utajili upo shambani na wala sio maofisini.
Asante nimeelewa Sasa
Habari za majukumu.
Kiongozi mimi nimelima alzeti aina ya Record kama sikosei ila cha kushangaza zimeota mbalambali sana, halafu mbona mbegu zimebaki nyingi sana baada ya kupanda eneo la heka mbili?
Nini tatizo, hata hivyo sehemu ambapo hazikuota vizuri ni heka ya kwanza maana nilipanda mvua ikanyesha kubwa sana. Ila heka ya pili zimeota vizuri mno. Wasiwasi wangu ni kwanini eneo la heka mbili mbegu pakit moja zilibaki?
Na mfumo niliopanda ni kama mahindi tu.
Na nimelima kilimo cha matuta. Kuhusu afya zipo vizuri nategemea kuanza kuweka mbolea, je mbolea aina ya KYNO PLUS inafaa?
Mfuko mmoja ni sh ngapi? Na unakuwa na kilo ngapi?
Habari. Hiyo mbegu Ni ya kisasa?, Mfuko mmoja unauzwa sh ngapi? Na unakuwa in kilo ngapi?
Sorry ningependa kupata ufafanuzi:
1. Je ni lazima kutumia mbolea ya samadi kabla ya kupanda wakati wa kuandaa shamba, ama mbolea ya kupandia inaweza tumika pekee tu
2. je nikitaka kulima mseto kati ya mahindi na alizeti unafikri ni mbegu gani ni sahihi kwa kutumia? je ni mbegu ndefu zote za mahindi na alizeti ? je ni mbegu fupi zote? au kuna angalizo jingine??
Asante na Ubarikiwe zaidi
Hongera kwa Elimu nzuri juu ya kilimo cha Alizeti. Nimevutiwa sana na ni zao bora sana kwa biashara.
Asante kwa mada yako nzuri, mimi ninataka kulima zao hili la alizeti maeneo ya Kitukutu mkoani Singida, mpaka sasa sijaanza maandalizi ya shamba je bado niko ndani ya muda au nimeishachelewa?
Je unaweza kulipa kilimocha alizeti kipindi cha mvua na kilimo chake kinakuaje?
Asante kwa elimu nzuri kiongozi.
Ningependa kufahamu idadi ya kuweka mbolea mpaka mavuno.
Asante kwa ufafanuzi
Je nipate wapi mbegu chotara hspa Mwanza?
I want to join the discussion
Mbegu chotara za alizeti zinapatikana wapi
Good
Kuna tofauti gani kati ya hizi mbegu HYSUN33 na HYSUN36
Nashukuru kwakweli nimepata mwanga la sivyo ilikuwa hatari kiasi cha kupoteza pesa
Nashukuru kwa somo zuri..
Nitakutafuta inbox mkuu
Francis simon kutoka Arusha, nataka nianze kulima mafuta naombeni ushauri wa nini nifanye na mandliz gani nichukuwe ya mwanzo
Maandalizi muhimu ni…
Maandalizi mengine yatategema mfumo utakao utumia kutunza shamba lako. Kila la heri
Habari
Safi Nestory, karibu…
Iringa ni mbegu gani inafaa kwa kilimo Cha alizeti hasa kwa hii mbegu fupi
Tunapendekeza matumizi ya mbegu chotara
Bei ya mbegu ni kiasi gani
Tafadhali wasiliana na wauzaji
Nimefurahi sana kujifunza Kilimo hiki, nataka kujaribu
Kila la heri
Shukuran sana kwa haya machapisho kuhusu kilimo cha Alizet.. Naenda kujarib sasa.Asante
Kila la heri
Shukuran sana kwa machapisho haya kuhusu Elimu nzima ya zao la Alizet
Endelea kuwa nasi
Thanks for the lesson
You’re welcome
Safi sana elimu nzuri, niko shambani msimu ujao natumai nitajifunza mengi kupitia jukwaa hili
Asanten sana
Karibu sana na endelea kuwa nasi
Makala nzuri sana, ubarikiwe ila mi nipo Chamwino Dodoma sijui ni aina gani nzuri kwa maeneo yetu na kingine ungekuwa unatuwekea na bei ya mbegu ili na sisi wageni kabisa tupate na mwanga wa bei zake. Shukrani sana na ninesha share makala hii ila msaada wa hapo juu 👆
Tunapendekeza matumizi ya mbegu chotara. Hatuna msaada sana kwenye suala la bei za mbegu kwa sababu hatuuzi mbegu na hatuna ushirika na makampuni ya mbegu. Hivyo itakulazimu kuulizia madukani au kwenye kampuni zalishaji
Naitwa Anastasia mkoa Kam rukwa nawez kupand hiyo mbegu mwez wa ngap
Sijui ni muda gani sahihi wa kulima shamba..
Yaani Shamba inatakiwa ilimwe kabla ya mvua au baada ya kunyesha mvua ?
Maandalizi ya shamba yafanyike kabla mvua hazijaanza kunyesha
Asante sana kwa makala yako kaka mkubwa. Nipo simiyu Bariadi ninampango Wa kulima ekari tatu za alizeti na mvua ndo ishaanza kunyesha mbegu gani inafaa kwa maeneo yangu haya?. Vilevile ningependa kujua Gharama ya mbegu na mbolea ya samadi, CAN na Urea. Asante,,,, 0682784781
Bwana Bernad, tunashauri matumizi ya mbegu chotara. Hata hivyo hatuuzi yoyote ktk pembejeo za kilimo, hivyo kujua gharama zake utalazimika kuulizia kwa mawakala au wauzaji husika.
Kila la heri!
Mungu Akubariki sana, Naingia kilimo cha Alizeti Morogoro Dakawa, hivo nakala yako imenipa Picha Kubwa sana ya Kilimo hiki
Shukan sana. Endelea kuwa nasi
asante sana mkuu kwa darasa hili, nipo nnaandaaa shamba langu maeneo ya kisarawe pwani, je n mbegu gani itafaa na msimu upi n mzuri kulima alizeti? masika au vuli?
Tunapendekeza mbegu chotara. Vuli au masika; msimu wowote unaweza kufaa
Jamani nawezaje pata mbegu fupi
Tafuta kwenye maduka ya pembejeo za kilimo. Au wasiliana na wataalamu kutoka kituo cha utafiti wa kilimo ulicho karibu nacho
Ubarikiwe Sana kwa makala zako
Amin! Shukran sana, endelea kuwa nasi.
Nashukuru sana kaka, coz Mimi najiandaa kulima alizet heka 2 mkoani Tanga, Handeni. Ila bado sijajua mbegu nzuri ya kisasa na inauzwaje dukani. Nipo dar es salaam endapo kuna uwezekano Wa kunikutanisha na mtaalamu nitashukuru sana, 0754074673
Itafute “Hysun 33” Mr Mwasopo. Inafanya vizuri sana
Mtaalam mbegu ipi nzuri zaidi fupi na chotara Kati ya hysun33 na Nsfh 36 shresta kwa uku kagera?
Sina hakika. Linganisha sifa na tabia zake, itakayoendandana na mazingira yako ni bora zaidi
hekari moja ya alizeti inatoa mavuno kiasi gani?
“Shamba la alizeti kutegemeana aina ya mbegu huweza kutoa mavuno wastani wa magunia 8 hadi 16 kwa ekari.”
Asante kwa makala nzuri mkuu! Nipo Songea, mbegu gani inafaa kwa nature ya huku!
Tunapendekeza mbegu za chotara. Tafuta mbegu chotara zinazokubali ukanda huo
umetoa elimu nzuri sana kuhusu kilimo cha alizeti.mimi pia nimeelewa namna ya kulima
Zipo makala zingine pia, usiache kuzisoma na wajuze wadau wengine
Nashukuru kwa makala hii nitakutafuta hata mim pia kwa ushauri zaidi usituchoke
Karibu sana. Hii ni kazi yangu, sitawachoka. Njooni kwa wingi tu!
Asante kwa kushare na ss
God bless u
Shukrani sana, endelea kuwa nasi
Habari,
Je Alizeti inaweza kupandwa kwenye mashamba yenye mwinuko yaani mashamba ya milimani kama maeneo ya Lushoyo
Ndio, unaweza kupanda hata maeneo ya milimani.
Sasa mimi niko mwanza wilaya kwimba nahitaji kulima heka 20 ni mbegu gani nitumie Katk eneo langu
Mbegu chotara (hybrid) ni bora zaidi
Thanks alot kwa elimu nzuri.
Shukrani sana. Endelea kuwa nasi
Nashukuru sana kwa makala hii nanimehamasika kufafanya japo heka moja kwa majaribio nipo Kahama shinyanga.
Karibu sana Mr Daud, nakutakia kila la kheri
Asante sana brother kwa somo hili maana naingia shamba mwezi wa huu kwa ajili yakilimo cha Alizeti. Nipo Daresala na nalimia maeneo ya Kisarawe. hivyo ningeomba nambayako ili niweze kukutafuta kwa ushauri zaidi.
Karibu sana Mr. Khalid, 0655570084
Nimejipanga msimu huu kulima sana alizeti tatizo ni bei tu ya mbegu ni kubwa mno kwa anaejua mbegu nzur yenye bei nzur anijuze Shamba langu ni ekari 20 nipo Dodoma 0627197813
Umewatembelea ASA pale Morogoro? Jaribu kuwatembelea uone kama unaweza kupata mbegu kwa bei nafuu kiasi
Wasiliana na ASA(agriculture seed Agency wapo morogoro na wanauza 1kg kwa shilingi elfu nne
Nashukuru Sana kwa ushauri wa kilimo unaendelea kutupatia!!
Endelea kuwa nasi kaka Lyimo. Kama hutojali tumia dkk 1 tu ku-share makala hii