Magonjwa ya Kuku

Share on facebook
Facebook
Share on twitter
Twitter
Share on linkedin
LinkedIn
Share on email
Email
Share on facebook
Share on twitter
Share on email
Share on whatsapp
Share on linkedin

IIi uweze kudhibiti magonjwa ya kuku yanayotokea katika kundi lako unahitaji kufahamu dalili za jumla za magonjwa hayo. Unapoigundua moja au zaidi ya dalili za ugonjwa au wadudu chukua hatua mara moja.


Magonjwa ya kuku yapo mengi. Hata hivyo siyo yote yanatokea mara kwa mara hapa Tanzania. IIi uweze kudhibiti yale yanayotokea katika kundi lako unahitaji kufahamu dalili za jumla za magonjwa hayo. Unapoigundua moja au zaidi ya dalili za ugonjwa au wadudu chukua hatua mara moja.

Yapo magonjwa ambayo yanaweza kuangamiza kundi lote la kuku katika muda mfupi. Jihadhari na uwezekano wa kupatwa na hasara zinazoletwa na magonjwa ambayo unaweza kuyazuia.

Dalili za Jumla za Magonjwa ya Kuku
 • Kuku kupoteza hamu ya kula.
 • Kuzubaa na kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu (Kutochangamka).
 • Kushuka kwa kiwango cha utagaji wa mayai.
 • Vifaranga kutokua upesi au kudumaa. – Macho kuwa na rangi nyekundu.
 • Kujikunja shingo.
 • Kutetemeka, kutoa majimaji puani, mdomoni na machoni.
 • Kutoa mharo (kinyesi) wa rangi ya kijani au wenye mchanganyiko na damu au cheupe.
 • Kukonda.
 • Kukohoa.
Ukiona moja au zaidi ya dalili hizi katika kundi lako chukua hatua za kutibu zilizoelezwa hapa chini. Kama hali ni ngumu zaidi omba msaada kwa mtaalam wa tiba ya mifugo ili achunguze mara moja na kukushauri jambo la kufanya.

Kuku-akichanjwa
Kuku akichanjwa

Hili ni jedwali linaloonesha ugonjwa, chanzo dalili na kinga au chanjo ya ugonjwa husika wa kuku

UGONJWA
CHANZO
DALILI
KINGA / CHANJO
1. Kideri (NewCastle)
Virusi
 • Kukohoa, kupumua kwa shida
 • Mwili kukosa nguvu
 • Shingo kujikunja
 • Kuharisha kijani
 • Kuku wengi hufa
 • Kuhara damu
 • Vifaranga wachanjwe katika juma lao la kwanza
 • Wachanjwe tena wanapofikisha umri wa miezi minne na nusu
 • Kuku wachanjwe kila baada ya miezi mitatu
2. Kuhara damu (Coccidiosis)
Bakteria
 • Kuku hujikusanya, hawachangamki, hushusha mbawa
 • Tunza usafi katika banda
 • Lisha vifaranga chakula kilichochanganywa na dawa ya kinga ya Coccidiosis kama vile Amprolium au Salfa
 • Watenge kuku wote walioambukizwa na uwape dawa kama Amprolium au salfa au Esb3
3. Ndui ya kuku (Fowl Pox)
Virusi
 • Malengelenge kwenye kishungi, kope za macho na sehemu zisizokuwa na manyoya
 • Kuchannja kuku wote wakiwa na umri wa miezi miwili
 • Watenge kuku wote walio ambukizwa na uwape ANTIBIOTIC kama OTC Plus au salfa
4. Mafua ya kuku (Fowl Cryza)
Bakteria
 • Kuku huvimba uso
 • Kamasi hutiririka puani na mdomoni
 • Kuhema kwa shida sana hata kukoroma
 • Usafi wa banda
 • Kuchanja kuku wote kabla hawajaambukizwa
 • Na kama ni tatizo sugu basi watibu wote waliougua kwa kuwapa ANTIBIOTICS kama Sulphamethazine, Steptomycin na Vitamin
5. Kuharisha Nyeupe
Bakteria
 • Kuharisha nyeupe na 
 • Kupungua hamu ya kula
 • Usafi wa vyombo na  banda kwa ujumla
 • Watenge kukuu wagonjwa 
 • Tumia dawa kama Furazolidone au Sulfadimidine
 • Hata vitunguu swaumu menya robo kilo utwange na uchanganye na maji lita moja. Chuja halafu uwape haya maji kwa muda wa wiki moja


Njia kuu za ujumla za kudhibiti magonjwa ni:
 • Kutunza hali ya usafi ndani ya banda na kudhiditi kusiwe na unyevu 
 • Matandazo yakichafuka yabadilishwe. 
 • Vyombo vya maji visafishwe kila siku 
 • Jitahidi uepuke kufuga kwa njia ya huria ili kuku wako wasiambukizwe magonjwa kirahisi 
 • Epuka kufuga kuku wako pamoja na bata na khanga.Hawa ni wabebaji wa vimelea vya magonjwa ya kuku japo wao hubaki salama
 • Zingatia ratiba za chanjo kwa magonja yasiyo na tiba kama kideri na mengineyo ya virusi 

Hayo ndo magonjwa ya kuku kwa ufupi lakini tumeakuandalia makala zingine zinazohusiana na ufugaji wa kuku, hizi hapa chini, bofya kuzisoma:

Share on facebook
Facebook
Share on twitter
Twitter
Share on linkedin
LinkedIn
Share on email
Email
Share on facebook
Share on twitter
Share on email
Share on whatsapp
Share on linkedin
MAKALA NILIZOKUCHAGULIA
COMMENTS
Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
1
0
Would love your thoughts, please comment.x

Sharing is caring...

Share on facebook
Facebook
Share on twitter
Twitter
Share on linkedin
LinkedIn
Share on email
Email
Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp

Join Our Farming Community