Karibu kwenye makala hii inayohusu Kilimo cha Matikiti Maji Tanzania. Kama mkulima mzaoefu na mtaalam wa kilimo cha matikiti maji, muda mfupi ujao nitakupa mwongozo wa kitaalam juu ya mbinu bora za uzalishaji, masoko na fursa za kibiashara katika kilimo hiki.
Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuri za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi.
Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine (curcubitaceae family) kama matango, maboga na maskwash (squash).
Tikiti maji ni zao la kipekee ambalo limekuwa likibamba soko la ndani na nje ya Tanzania kutokana na ladha yake nzuri, faida zake kiafya, na matumizi yake katika viwanda vya chakula na vinywaji. Hata hivyo, ili kuweza kunufaika na soko hili, mkulima anahitaji kujua mbinu bora za kilimo, mahitaji ya soko, na fursa za biashara.
Katika makala hii, nitaelezea kwa kina kuhusu masoko ya matikiti maji Tanzania, mahitaji ya soko, jinsi ya kuongeza uzalishaji, na fursa za biashara. Nitakupa miongozo na mikakati ya kufikia masoko ya ndani na nje ya nchi, na kujenga uhusiano mzuri na wanunuzi na wazalishaji wa viwandani.
Kupitia makala hii, utajifunza jinsi ya kuongeza uzalishaji wa matikiti maji, jinsi ya kujenga thamani ya matunda yako, na jinsi ya kufikia masoko ya ndani na nje ya nchi. Kwa hiyo, endelea kusoma ili kuweza kujifunza zaidi kuhusu Kilimo cha tikiti Maji Tanzania na fursa zake za biashara.
Uchaguzi wa eneo linalofaa
Matikiti maji husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana, baridi kali, mvua nyingi wala udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu.
Joto: Matikiti hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21 – 30 sentigradi. Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota.
Mvua: Matikiti maji yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400 – 600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungasi na bakteria ambayo huathili mavuno.
Hali ya Udongo: Kilimo cha matikiti huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0
Mikoa ya Tanzania: Kilimo cha matikiti maji kinakubali vizuri kwenye ukanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM, Tanga, Morogoro, Mtwara, Lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa tatu mpaka wa tisa.
Uandaaji wa Shamba
Fyeka vichaka na ng’oa visiki vyote. Katua kwa kina cha sm 22.5 kwenye Sesa. Kabla ya kupandikiza udongo utifuliwe vizuri na majani yaondolewe kabisa. Shamba liandaliwe vizuri kwa kusafisha ili kuondoa mimea mingine ambayo inaweza kuwa ni chanzo cha magonjwa. Weka mbolea ya samadi debe moja kwa kila mita 10 za eneo. Tengeneza matuta katika sehemu ambayo ina majimaji.
Mbegu Bora za Matikiti
Mbegu bora za tikiti maji zipo nyingi sana, zifuatazo ni baadhi tu ya mbegu hizo na makampuni yanayozalishaji mbegu hizo.
- Arashani F1 – kutoka Syngenta
- Sukari F1 – Kutoka East Africa seeds
- Sugar king F1 – kutoka Africasia
- Juliana F1 – kutoka Kiboseed
- Zebra F1 – Kutoka Balton
- Pato F1 – Kutoka Agrichem
- Soma hapa mbegu Mpya zilizotangazwa na Kamati ya Taifa ya mbegu
Maamuzi ya mbegu nzuri ya kupanda nashauri yaanzie sokoni. Lijue soko lanko, soko ambalo utauza mazao yako. Jifunze bidhaa wanaipenda, yaani wanapenda matikiti ya aina gani? Ukishajua basi utajua mbegu ya kununua na kupanda. Lakini pia hakikisha hiyo mbegu inakubali katika eneo lako kwani kila mbegu ina maelezo ya maeneo inayofanya vziuri.
Upandaji wa tikiti maji
Katika shamba la ukubwa wa hekta moja kiasi cha kilo 3 – 4 cha mbegu kinaweza kutumika. Panda mbegu 2 au 3 moja kwa moja katika kila shimo. Usipande katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa mita 1 hadi 2 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 – 3 kutoka mstari hadi mstari.
Kwenye makala yetu ya kanuni za kilimo bora tumeeleza kwa kina umuhimu wa kuzingatia nafasi za kupandia na athari zake iwapo hutozingatia.
Zingatia: usitumie mbegu za tikiti ulilonunua (kwa ajili ya kula) kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi na ubora wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2).
Sasa unaweza kujipatia Kitabu (PDF) cha Mwongozo wa kilimo cha Matikiti maji sasa hivi kwa bei nafuu sana. Kitabu hiki kimeboreshwa zaidi kwa ushauri wa kitaalam, mapendekezo ya kiasi, na aina za mbegu bora, mbolea na viuatilifu vya kutumia pamoja na mchanganuo wa bajeti ya kilimo na faida. Bofya hapa kukipata ndani ya Whatsapp au bofya hapa kukipata kwa email.
Kupandikiza na kupunguzaji miche
Mimea ya mitikiti huanza kuota baada ya kama wiki 2 hivi. Inapoanza kuota ifuatilie kwa ukaribu sana ili ubaini maeneo yote yenye kasoro kama vile mbegu ambazo hazijaota kabisa au zilizoota zaidi ya mbili katika kila shimo.
Pandikiza kila sehemu ambapo mbegu hazijaota au imeota moja tu. Na punguza miche kwenye kila shimo mbalo zimeota zaidi ya mbili. Lengo hapa ni kuhaikisha kuwa unakuwa na mimea miwili katika kila shimo, sio zaidi, sio pungufu. Tumeeleza kwa kina umuhimu wa kuzingatia kupandikiza na kupunguzia miche kwenye makala ya kanuni za kilimo bora hapa.
Angalizo: Usinga’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki. Vilevile unaweza kupandishia udongo kwenye mashina ili kusaidia kupunguza maji kutuama kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba.
Umwagiliaji
Shamba linatakiwa limwagiliwe mara kwa mara wakati kiangazi. Kipindi muhimu zaidi ambapo mimea hii huhitaji maji zaidi ni katika kipindi cha uotaji wa mbegu, wakati wa kutoa maua na siku takribani kumi kabla ya kuvuna. Iwapo kutakuwa na ukosefu wa maji kutasababisha kutengenezwa kwa matunda ambayo si mazuri na yenye umbo baya, pia kupungua kwa ukubwa wa matunda.
Mzunguko wa umwagiliaji utategemea mambo yafuatayo: mfumo wako wa umwagiliaji, msimu au hali ya hewa, aina ya udongo wako na hatua ya ukuaji wa zao lako.
Angalizo: usimwagilie matikiti wakati wa jioni sana au usiku kwasababu inaweza kusababisha magonjwa ya majani kutokana na unyevu kukaa muda mrefu. Vile vile usimwagilie juu ya maua wakati wa asubuhi au jioni kwasababu unaweza kuzuia wadudu kama nyuki ambao ni muhimu sana wakati wa uchavushaji.
Mahitaji ya Mbolea ya Matikiti Maji
Mbolea ya kupandia: Wakati wa kupanda tumia DAP weka gram 5 kwa kwa kila shimo (lenye mbegu moja, na weka gram 10 au 15 kama kuna mbegu 2 au 3), hakikisha mbolea na mbegu havigusani.
Mbolea ya kukuzia: Wiki mbili baada ya miche yako kuota weka mbolea ya kiwandani NPK (Yaramila winner) gram 5 tena kwa kila mche, hakikisha unaichimbia chini na isigusane na mmea. Weka mbolea yenye Calcium kama Yaramila nitrabo au CAN gram 10 kwa kila shina unapoona matunda yameanza ili kusaidia kupata matunda makubwa na mazuri.
Kwa ekali 1 ya matikiti utahitaji mfuko mmoja wa DAP, mmoja wa NPK na mmoja wa CAN ikiwa utabakiza miche miwili kwa kila shimo.
Kwa makadirio ya karibu ujazo wa kifuniko kimoja cha maji safi au soda take-away ni sawa na gram 5 hivyo ili upime gram 10 jaza vifuniko viwili vya maji safi. Soma hapa mahitaji ya mbolea katika mahindi
Uwekaji wa matandazo (Mulching)
Matandazo ina maana ya kutumia nyasi na mabaki ya mimea mingine kufunika udongo. Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile vile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.
Wadudu na Mgonjwa hatari ya Matikiti maji
Wadudu Waharibifu wa Matikiti Maji
1. Nzi weupe [White flies]
Dalili: Wadudu hawa wanaonekana kama nzi weupe na huwa wanakaa juu ya majani, na hutoa juisi inayoweza kusababisha ukuaji wa kuvu na kuonekana kwa kuvu nyeupe kwenye majani.
Madhara: Huleta madhara kwa kusababisha uharibifu wa majani na kusambaza magonjwa.
Udhibiti: Njia za kuwadhibiti ni pamoja na kutumia mitego yenye feromoni, na kutumia wadudu wanaowala kama vile Entomopathogenic fungi. Dawa za kuwadhibiti ni pamoja na imidacloprid, acetamiprid, na thiamethoxam.
2. Nzi wa matunda [Fruit flies]
Dalili: Wadudu hawa huonekana wakizurura kwenye matunda ya tikiti maji, na pia hutaga mayai yao kwenye matunda yanayoanza kukomaa.
Madhara: Mayai yanayotagwa na nzi wa matunda hupelekea kuwa na matunda yasiyo na ubora na yanayoharibika.
Udhibiti: Njia za kuwadhibiti ni pamoja na kutumia mitego yenye feromoni, kuondoa matunda yaliyooza na kuharibiwa, na kuzingatia usafi wa bustani. Dawa za kuwadhibiti ni pamoja na spinosad, malathion, na deltamethrin.
3. Mende wa matango [Curcubit beetles]
Dalili: Mende hawa huonekana wakizurura kwenye majani na maua ya mimea na na kuyala. Na pia hutaga mayai yao kwenye majani.
Madhara: Wadudu hawa hula majani na maua ya mimea, hivyo kupunguza uzalishaji.
Udhibiti: Njia za kudhibiti wadudu hawa ni pamoja na kutumia mitego ya kuvuta wadudu [feromone hormone], kutumia wadudu wanaowala kama vile Bacillus thuringiensis, na kutumia dawa za kudhibiti wadudu kama vile Carbaryl, Malathion, na Imidacloprid.
4. Nzi wa matikiti [Melon flies]
Dalili: Wadudu hawa huonekana wakizurura na kula majani, maua na matunda ya mimea na hutaga mayai yao kwenye matunda yanayokua.
Madhara: Mayai yanayotagwa na nzi hawa hupelekea kuwa na matunda yasiyo na ubora na yanayoharibika.
Udhibiti: Njia za kuwadhibiti ni pamoja na kuondoa mimea iliyoambukizwa na kuweka mitego yenye feromoni. Dawa za kuwadhibiti ni pamoja na carbaryl, malathion, na permethrin.
5. Vidukari [aphids]
Ni wadudu wadogo, wenye miili laini ambao hukusanyika kwenye majani na shina.
Dalili: Wadudu hawa wanaweza kuwa rangi ya kijani, nyeusi, au nyeupe na huwa wanakaa juu ya majani na shina.
Madhara: Wanaweza kusababisha manjano na kujikunja kwa majani, kudumaa kwa ukuaji na kupunguza mavuno. Wanaweza pia kutoa umande ambao huvutia mchwa na ukuaji wa fangasi.
Udhibiti: Nyunyiza kwa maji ya sabuni. Changanya kijiko kikubwa kimoja cha sabuni ya maji kwenye lita 1 ya maji na nyunyiza sehemu zote za majani. Dawa za kuwadhibiti ni pamoja na imidacloprid, acetamiprid, na thiamethoxam.
6. Vithiripi [thrips]
Ni wadudu wembamba wenye mabawa yenye pindo ambao hula maua na matunda.
Dalili: Wadudu hawa ni wadogo sana na huwa wanakaa kwenye majani na maua.
Madhara: Wanaweza kusababisha makovu na kuharibu maumbo ya matunda, kupunguza ubora wake na hatimaye soko lake. Wanaweza pia kusambaza virusi kwa mimea.
Udhibiti: Nyunyiza kwa maji ya sabuni. Changanya kijiko kikubwa kimoja cha sabuni ya maji kwenye lita 1 ya maji na nyunyiza sehemu zote za majani. Dawa za kuwadhibiti ni pamoja na spinosad, acetamiprid, na imidacloprid.
7. Sota [Cutworms]
Dalili: Wadudu hawa ni viwavijeshi ambao hukata mashina ya miche wakati wa usiku na kusababisha mimea kuanguka. Sota huleta madhara makubwa hasa kwa mimea michanga.
Madhara: Uharibifu wa shina unaweza kusababisha kupoteza miche yote, na hivyo kupunguza uzalishaji.
Jinsi ya kudhibiti: Njia za kuwadhibiti ni pamoja na kutumia mitego, kuchimba mashimo karibu na mimea, na kutumia dawa kama Carbaryl, Diazinon, au Chlorpyrifos.
8. Utitiri [Spider mites]
Utitiri ni wadudu wadogo sana ambao hushambulia majani ya mimea na kusababisha majani kuwa ya manjano, na baadaye kubadilika kuwa ya kahawia.
Dalili: Majani ya tikiti maji yanageuka rangi na kuwa manjano kabla ya kupauka na kufa.
Madhara: Utitiri huacha nundu nyeupe kwenye majani ambayo huwa kama ishara ya kuharibika kwa majani na kusababisha upungufu wa juisi ndani ya majani ya tikiti maji. Hii inaweza kusababisha mimea kudumaa, kupoteza majani, na kusababisha uharibifu wa mazao.
Jinsi ya kuwadhibiti: Njia ya kuzuia ni kuhakikisha unahifadhi usafi wa shamba na kuzuia wadudu hawa kuenea. Matumizi ya mimea yenye harufu kama vile lavender, peppermint, na garlic huweza kuwazuia utitiri. Dawa zinazoweza kutumika ni pamoja na sulphur, Neem oil, na Acaricides.
Magonjwa ya Matikiti maji
1. Ukungu jani wa Alternaria [Alternaria Leaf Spot]
Chanzo: Fangasi anayeitwa Alternaria cucumerina.
Dalili: Madoa meupe hadi kahawia yenye umbo la duara kwenye majani ya mimea ya tikiti maji. Madoa haya hukua na kuwa makubwa kadiri yanavyoendelea kuenea na kuharibu majani.
Uharibifu: Ugonjwa huu unasababisha upungufu wa majani kwenye mmea wa tikiti maji, kupungua kwa ubora wa matunda, na kupungua kwa mavuno ya mmea.
Udhibiti: Njia za kudhibiti ugonjwa wa Alternaria Leaf Spot ni pamoja na kuepuka kupanda tikiti maji kwenye udongo ulio na mvua nyingi na unyevu mwingi, kuondoa majani yaliyoathiriwa na ugonjwa, na kutumia dawa za kudhibiti magonjwa kama vile Chlorothalonil, Mancozeb, na Azoxystrobin.
2. Ugonjwa wa kutoka utomvu [Gummy Stem Blight]
Chanzo: Fangasi anayeitwa Didymella bryoniae.
Dalili: Madoa madoa ya rangi ya njano au hudhurungi yenye umbo la mviringo au mviringo uliochongoka kwenye majani; kutoka utomvu wenye rangi ya hudhurungi au nyeusi kwenye shina na matunda [gummosis]. Ugonjwa huu unaweza kuenea kwa kasi katika hali ya joto, yenye unyevunyevu.
Uharibifu: Kupunguza uwezo wa mmea wa kupumua na kufanya usanisinuru. Ugonjwa huu husababisha mmea kukauka na kufa, na hivyo kupunguza uzalishaji wa mmea wa tikiti maji.
Udhibiti: Njia za kudhibiti ugonjwa wa Gummy Stem Blight ni pamoja na kupanda mimea kwa nafasi inayofaa [mistari iwe umbali wa mita 1.5 hadi 3] na kuzingatia mzunguko wa mazao, kuondoa majani yaliyoathiriwa na ugonjwa, na kunyunyizia dawa za fangasi kama vile Thiophanate-methyl na Carbendazim.
3. Mnyauko fusari [Fusarium Wilt]
Chanzo: Fangasi anayeitwa Fusarium oxysporum.
Dalili: Dalili za ugonjwa huu ni majani kuonekana ya manjano, mmea kukauka, na kuoza kwenye shina na mizizi ya mmea. Mnyauko Fusarium unaweza kudumu kwenye udongo kwa miaka mingi, na hivyo kufanya kuwa vigumu kudhibiti.
Uharibifu: Kupoteza maji na virutubisho vya mmea; kudhoofisha au kuua mmea kabisa, hivyo basi kusababisha kupungua kwa ubora na kiasi cha mavuno kwa mazao ya tikiti maji.
Udhibiti: Njia za kudhibiti ugonjwa wa Fusarium Wilt ni pamoja na kutumia mbegu bora zisizo na maambukizi; kupanda tikiti maji katika udongo wenye pH ya 6.5-7.0; kutumia mbolea za phosphorus; kupanda tikiti maji katika maeneo mapya yasiyoathiriwa na ugonjwa huo; kunyunyizia dawa za fangasi kama vile copper, benomyl au thiophanate-methyl mara kwa mara.
4. Muozo mkaa [Charcoal Rot]
Chanzo: Fangasi anayeitwa Macrophomina phaseolina.
Dalili: Mmea unaonekana kuishiwa nguvu, majani hupoteza rangi yake na kuwa na rangi ya njano, na mizizi ya mmea huonekana kuwa na rangi nyeusi kama makaa.
Uharibifu: Ugonjwa huu unaweza kusababisha kufa kwa mmea wa tikiti maji na kupunguza mavuno ya mmea.
Udhibiti: Njia za kudhibiti ugonjwa wa Charcoal Rot ni pamoja na kuepuka kupanda tikiti maji kwenye udongo wenye unyevu mwingi, kuhakikisha udongo umekauka kikamilifu kabla ya kupanda, na kutumia dawa za fangasi kama vile Azoxystrobin, Carbendazim, na Flutolanil.
5. Ubwiri unga [Powdery Mildew]
Chanzo: Fangasi wa familia ya Erysiphaceae [Erysiphe cichoracearum]. Also Sphaerotheca fuliginea.
Dalili: Majani yaliyoshambuliwa huonekana kama yamemwagiwa unga au majivu meupe upande wa juu na unga huu unaweza kusambaa hadi kwenye shina na matunda ya mmea.
Uharibifu: Ugonjwa huu unaweza kusababisha kupungua kwa uzalishaji wa mmea wa tikiti maji na kuharibu ubora wa matunda.
Udhibiti: Njia za kudhibiti ugonjwa wa Powderly Mildew ni pamoja na kuepuka umwagiliaji wa maji kwenye majani ya mmea, kupunguza unyevu kwenye mazingira, na kunyunyizia dawa za fangasi kama vile Azoxystrobin, Sulphur, na Potassium Bicarbonate.
6. Ubwiri vinyoya [Downy Mildew]
Chanzo: Fangasi wa familia ya Peronosporaceae [Peronospora parasitica]
Dalili: Majani yaliyoshambuliwa hugeuka rangi na kuwa kama ya njano, huku baadhi ya majani yakiwa kama yanakauka na madoadoa meusi kwa mbali. Kwenye sehemu ya chini ya jani huonekana ukungu mweupe au wa rangi ya zambarau ambao huenea haraka na kufunika jani lote. Majani yaliyoathirika sana hugeuka rangi na kuwa kahawia au nyeusi na kuanguka.
Uharibifu: Ugonjwa huu husababisha kupungua kwa usanisinuru (photosynthesis) kutokana na kuharibiwa kwa majani. Hii husababisha kupungua kwa ukuaji wa mimea na matunda. Matunda yaliyoathirika huwa madogo, yasiyoiva vizuri na yenye ladha mbaya.
Udhibiti: Njia za kudhibiti ugonjwa wa Down Mildew ni pamoja na kuepuka umwagiliaji wa maji kwenye majani ya mmea, kupunguza unyevu kwenye mazingira, na kutumia dawa za fangasi kama vile Azoxystrobin, Propineb, na Metalaxyl na Mancozeb.
7. Mnyauko bakteria [Bacteria Wilt]
Chanzo: Bakteria wa aina ya Erwinia tracheiphila. Usichanganye na Ralstonia solanacearum ambaye husabibisha mnyauko bakteria kwenye jamii ya nyanya.
Dalili: Dalili za ugonjwa wa ukungu wa bakteria katika tikiti maji ni majani kunyauka ghafla na mmea mzima kufa bila kuonyesha dalili zozote. Majani yanaweza kuwa na rangi ya njano au hudhurungi na kunyauka haraka, wakati shina na marando ya mmea yanaweza kuwa na rangi nyeusi au hudhurungi. Mara nyingi, shina linaweza kupasuka karibu na ardhi.
Pia ukikata shina la mmea ulioathirika, utomvu mweupe wa krimu hutoka. Utauona kwa urahisi zaidi ukiliweka kwenye bilauri angavu yenye maji.
Uharibifu: Ugonjwa wa ukungu wa bakteria husababisha upotevu mkubwa wa mavuno katika zao la tikiti maji, hasa ikiwa ugonjwa huo unatokea mapema katika msimu wa kupanda. Mimea iliyoambukizwa kawaida hufa ndani ya wiki chache baada ya dalili za ugonjwa kuanza kuonekana, na hii inafanya kuwa vigumu kutibu ugonjwa mara baada ya kuenea.
Udhibiti: Nyunyuzia dawa za bakteria kama vile Streptomycin sulfate, Copper hydroxide, na Bordeaux mixture [mchanganyiko wa copper(II) sulphate (CuSO4) na chokaa (CaO) unotumika kutibu magonjwa ya bakteria na fangasi].
8. Chule [Anthracnose]
Chanzo: Fangasi wa familia ya Colletotrichum [Colletotrichum orbiculare]
Dalili: Majani, shina na matunda ya mmea kuwa na madoa ya kahawia au meusi. Madoa haya huongezeka ukubwa na kuunganika pamoja na kusababisha jani au matunda kukauka na kuanguka.
Uharibifu: Kupunguza uwezo wa mmea wa kupumua na kufanya usanisinuru; kuharibu muonekano wa matunda na kupunguza ubora wake.
Udhibiti: Njia za kudhibiti ugonjwa wa Anthracnose ni pamoja na kuepuka unyevu mwingi kwenye mazingira, kufanya usafi kwenye shamba la tikiti maji, kutoa mimea michanga katika shamba ili kuepuka maambukizi, na kunyunyizia dawa za fangasi kama vile Chlorothalonil, Azoxystrobin, na Propineb.
Uvunaji wa matikiti maji
Matikiti maji ni miongoni mwa mazao yanayochukua muda mfupi sana kukomaa. Kwa kawaida tikiki maji huwa tayari kwa kuvuna baada ya siku 80 hadi 100 tangu kupanda. Vuna wakati matunda yameiva kabisa, usiwahishe wala kuchelewesha baada ya kufika wakati wake. Wakati wote wa uvunaji umakini unahitajika kutoyajeruhi matunda.
Ekari moja huweza kutoa kati ya tani 15 mpaka tani 35 za matikiti kutegemeana na aina ya mbegu na matunzo shambani. Baada ya kuvuna, matikiti yahifadhiwe katika eneo lenye ubaridi wa nyuzijoto 15 hadi 20 za centigrade. Eneo liwe na unyevua-anga (humidity) kati ya 80 hadi 85%.
Sasa unaweza kujipatia Kitabu (PDF) cha Mwongozo wa kilimo cha Matikiti maji sasa hivi kwa bei nafuu sana. Kitabu hiki kimeboreshwa zaidi kwa ushauri wa kitaalam, mapendekezo ya kiasi, na aina za mbegu bora, mbolea na viuatilifu vya kutumia pamoja na mchanganuo wa bajeti ya kilimo na faida. Bofya hapa kukipata ndani ya Whatsapp au bofya hapa kukipata kwa email.
Mahitaji ya soko la Matikiti Maji Tanzania
Matikiti maji ni zao muhimu katika soko la ndani na nje ya Tanzania. Nchini Tanzania, matikiti maji hutumiwa kama chakula cha moja kwa moja na pia hutumika kama malighafi kwa ajili ya viwanda vya kusindika.
Kwa upande wa soko la nje, matikiti maji ya Tanzania huuzwa katika nchi mbalimbali kama vile Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Afrika Kusini, Ulaya, na Mashariki ya Kati.
Mahitaji ya wateja na wasindikaji wa matikiti yanaongezeka kila siku kutokana na faida zake za kiafya na lishe. Matikiti maji yana virutubisho muhimu kama vile vitamini A, C, na E, pamoja na madini kama vile potasiamu na magnesiamu. Aidha, tikiti husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili, kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo na kiharusi, na pia husaidia katika kuzuia kansa.
Mbinu za kuongeza thamani ya matikiti maji kwa ajili ya soko la ndani na nje ya Tanzania zinajumuisha mambo kama vile kusindika matikiti maji na kutengeneza bidhaa nyingine kama vile juisi, siagi, na matunda ya kukaushwa.
Hii itasaidia kuhifadhi matikiti maji kwa muda mrefu na pia kuongeza thamani yake. Mbali na hilo, kuhakikisha ubora wa matikiti maji kwa kuchagua wa aina bora za mbegu, mbinu bora za kilimo, na udhibiti wa magonjwa na wadudu pia ni muhimu katika kufikia mahitaji ya masoko ya ndani na nje ya Tanzania.
Fursa za kibiashara katika Kilimo cha Matikiti Maji
Kilimo cha matikiti maji nchini Tanzania kina fursa nyingi za biashara kwa wakulima. Hapa nitazungumzia fursa tatu kubwa ambazo ni: Ushirikiano na wasindikaji wa matikiti, Kushiriki katika masoko ya kimataifa ya matikiti au matunda kwa ujumla wake, na Ujasiriamali wa kuongeza thamani ya matikiti maji kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali.
Fursa ya kwanza: Ushirikiano na wasindikaji wa matikiti na matunda maengine. Hii ni fursa muhimu ya biashara kwa wakulima wa matikiti Tanzania. Wasindikaji hawa hununua matikiti maji kwa wingi kutoka kwa wakulima na kisha kuyasindika kuwa juisi, siagi, matunda ya kukaushwa na bidhaa nyingine za matikiti.
Kwa kushirikiana na wasindikaji hawa, wakulima wanaweza kupata soko la uhakika la matikiti na pia kuongeza thamani ya mazao yao.
Fursa ya pili: Kushiriki katika masoko ya kimataifa ya matikiti au matunda kwa ujumla wake. Hii ni fursa nyingine ya biashara kwa wakulima. Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuzalisha matikiti yenye ubora na kwa kiasi kikubwa. Hivyo, kushiriki katika masoko ya kimataifa ya matunda ni fursa kubwa ya kujiongeza mapato na kuongeza thamani ya zao hili.
Kupitia ushirikiano na wafanyabiashara wa kimataifa, wakulima wanaweza kusafirisha matunda nje ya nchi kwa bei nzuri na pia kujifunza teknolojia na mbinu mpya za kilimo.
Fursa ya tatu: Ujasiriamali wa kuongeza thamani ya matikiti maji kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali. Hii ni fursa nyingine tena ya biashara kwa wakulima wa tikiti nchini Tanzania.
Wakulima wanaweza kutengeneza bidhaa kama vile juisi, siagi, matunda ya kukaushwa na bidhaa nyingine za matikiti maji. Bidhaa hizi zinaweza kuuza kwa bei nzuri katika soko la ndani na nje ya Tanzania.
Kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali za matikiti, wakulima wanaweza kuongeza thamani ya mazao yao na kuboresha mapato yao.
Jinsi ya kufikia masoko ya tikiti maji
Kilimo cha tikiti ni moja ya shughuli za kilimo zinazoweza kuleta faida kubwa kwa wakulima nchini Tanzania. Hata hivyo, ili kufanikiwa katika kilimo hiki, ni muhimu kuzingatia njia bora za kufikia masoko ya ndani na nje ya nchi. Katika sehemu hii, tutazungumzia jinsi ya kufikia masoko ya matikiti maji Tanzania.
1. Kujenga mahusiano mazuri na wateja wa ndani na nje ya nchi
Uhusiano mzuri na wateja ni jambo muhimu sana katika kufikia masoko ya mazao nchini Tanzania.
Kwa mfano, unaweza kujenga uhusiano mzuri na wasambazaji wakubwa wa matunda kama vile supermarket na maduka makubwa ya vyakula ili kuweza kuuza matikiti yako kwa wingi.
Vilevile, unaweza kuwafikia wateja wako kwa njia ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram, na Twitter. Hii itakuwezesha kuwa karibu na wateja wako na pia kutoa taarifa kuhusu bidhaa zako kwa wateja wako wa ndani na nje ya nchi.
2. Kushiriki katika maonyesho ya kilimo na ya biashara
Kushiriki katika maonyesho ya kilimo na maonesho ya bidhaa ni njia nzuri ya kufikia wateja wengi na pia kujenga uhusiano mzuri na wateja wako. Mfano mzuri ni maonyesho ya kilimo ya Nane Nane yanayofanyika kila mwaka Agosti 8. Na maonyesho ya biashara ya Saba Saba yanayofanyika kila mwaka Julai 7.
Maonyesho haya yanakutanisha wakulima, wafanyabiashara na wanunuzi wa ndani na nje ya nchi, na hivyo kuwezesha kujenga mahusiano mazuri ya kibiashara. Kupitia maonyesho haya, unaweza pia kujifunza kuhusu teknolojia mpya na mbinu bora za uzalishaji wa matikiti maji.
3. Matumizi ya teknolojia za masoko
Matumizi ya teknolojia za masoko ni njia nyingine nzuri ya kufikia wateja wako. Kwa mfano, unaweza kutumia barua pepe, ujumbe wa maandishi (SMS) au tovuti ya biashara yako kufikia wateja wako wa ndani na nje ya nchi.
Vilevile, unaweza kutumia mitandao ya kijamii na majukwaa ya biashara kama vile Jumia, Kilimo Mart, na Zoom Tanzania ili kuuza bidhaa zako mtandaoni na kufikia wateja wengi zaidi.
Kwa kuzingatia njia hizi za kufikia masoko, utaweza kuuza ya matikiti yako kwa wingi na pia kufikia wateja wengi zaidi ndani na nje ya nchi. Hivyo, ni muhimu kuzingatia njia bora za kufikia masoko ili uweze kuongeza tija kwenye kilimo chako.
Hitimisho
Katika makala hii, tumegusia mambo kadhaa kuhusu kilimo cha matikiti maji Tanzania, ikiwa ni pamoja na Mbinu bora za uzalishaji, faida zake, mahitaji ya soko, fursa za kibiashara, na jinsi ya kufikia masoko ya matikiti maji.
Kilimo cha matikiti maji ni muhimu kwa sababu ni zao linalolimwa kwa wingi nchini Tanzania na linaweza kutoa fursa nyingi za biashara.
Tunapendekeza wakulima wote wa matikiti na mazao mengine ya mbogamboga na matunda kufuata mbinu bora za kilimo, kushirikiana na wasindikaji na wateja, na kutumia teknolojia za masoko ili kufikia masoko mengi zaidi ndani na nje ya Tanzania.
Kwa kuboresha kilimo cha matikiti maji Tanzania, tunaweza kuzalisha mazao mengi zaidi na kuongeza mapato ya wakulima na taifa kwa ujumla.

Enter your comment…number yangu jamanii 0753389875 nahitajii uo ufundi wa matikiti
Nimejipanga ili kuhakikisha natumia elimu niliyoipata humu ndani na kuifanyia kazi
Nakutakia mafanikio mema kaka Francis Deni, itakuwa vizuri ukitujuza unavyoendelea kwa faida ya wengi
Habari, mimi nimejarib kulima matikiti huko kigambon lkn nilichokipata ni maumivu, nimelaza laki saba nimeambulia laki mbili na nusu. Nimeona hapa muda unaotakiwa lkn mwenyej wangu aliniambia ni miez miwili tu na nilipanda F1ya Kenya. Ila naomba kuuliza coz humu ndani sijakiona, Je ni kweli wiki moja ya mwisho unatakiwa usimwagie ili tunda liweke sukari? Naomba kuwasilisha
Pole sana kwa yaliyokufika. Mara baada ya matikiti kutoa matunda, yanapokuwa makubwa unatakiwa kupunguza maji kadri yanapoelekea kukomaa (refusha “irrigation interval”) kama ilikuwa mara mbili kwa wiki basi iwe mara moja kwa wiki au wiki mbili.
Pia ni muhimu matitiki yapate muda wa ukame kwa wiki au zaidi, kabla ya kuvuna, ili yaweke sukari nyingi zaidi.
Asante mtaaramu umeenda deep
Jamani ekari moja inakiasi gani cha mbegu?..
Hakika hii elimu ni nzuri sana.
Nimependezwa sana na elimu ya kilimo cha matikiti maji.Ntalifanyia kazi na ntaletà mrejesho hapa
Karibu sana
Nimepanda bila Sukari F1 tarehe 5.10.2019 ila sijapanda kwa mbolea yeyote ni mbolea gani inafaa kwa kukuziaa.
Mm matikitiki maji yangu majani yanajikunja nitumie Dawa gani msaada yana umri wa miezi miwili sasa
Siwezi kushauri bila kuona hali halisi. Wasiliana nami whatsapp hapa
Thanx kwa somo zuri
Shukrani, karibu sana
Nahitaji kjjifunza zaidi kwenu kuhusu kilimo cha tikiti maana nimelima na kupanda bado hazijaota mbegu
Mambo ni mazuri sana endelea kutuelimisha
kikubwa ni mtaji tu,kweli kilimo kinalipa
kikubwa ni mtaji tu,kweli kilimo kinalipa
Karibu sana, Endelea kuwa nasi
nashukuru kwa elimu yako nzuri sana.nakuhakikishia nitaifanyia kazi fulsa hii na kwa mpango wa mungu nitafanikiwa na wewe ushukuriwe kwani naamini umenisogeza hatua moja mbele
Ahsante sana, fanya juhudi M/Mungu atakuwezesha. Usisahau ku-subscribe kwa mengi mazuri yajayo
Labda pia naombeni kuondolewa wasiwasi juu ya kilimo hiki.je jipi kuhusu mkoa wa kagera wilaya ya muleba kilimo hiki ni rafiki wa mazingira?Vipi kuhusu vipimo hivi vya pH,mm za mvua na kiwango cha jotoridi na ubaridi nitavipataje mimi mtu wa hali ya chini kikipato?mbegu na mbolea naweza kuzipata wapi kwa urahisi?vipi kuhusu bei ya vitu hivyo nilivyovitaja?nitashukuru nikipata majibu kupitia email yangu ya [email protected]
Mazingira / Hali ya hewa ya Muleba haina tatizo na kilimo cha matikiti maji.
Vitu kama mbegu na mbolea vinapatikana katika maduka ya pembejeo za kilimo ama kwa suala la bei: Urea kwa kawaida ni Tsh 50,000, CAN ni Tsh 55,000 na DAP ni 80,000. Hizo ni bei kulingana na mazingira ya kwetu, hata hivyo bei zinaweza kubadilika kulingana na mazingira kwa hiyo inaweza kupungua au kuongezeka kidogo kwa niliyotaja mimi.
Kuhusu vipimo vya Ph, joto na mm za mvua: hivi vinahitaji maelezo ya kutosha kwani ni changamoto kwa wakulima wengi. Hivyo nitaanza makala maalum kwa ajili hiyo.
kaka mm mgeni katika kazi hii tuseme mm mgeni nataka kujinasua Bariadi vip udongo wetu mweusi vp unafaaa kaka kilimo hiki Cha matikiti
Hekari 1 inatoa kias gan ch fedha
Habari!!
Asante kwa elimu hii ya tikiti maji!!
kilimo cha matikiti katika ukanda wa mto ruvu (mlandizi) kinaweza kukubali bila kuathiri uzalishaji na ubora wa tikiti kama masharti yote ya kilimo hicho yakifwatwa? nikimaanisha hali ya hewa ya eneo inaruhusu?
Asante!!!!
Ndio, Kinakubali
Nitumie pdf ya Kilimo cha matikiti, nimesha lipia 1000 kwenye Airtel money
Habari naomba namba yako ili tuweze kuwasiliana ili uweze kunielekeza 1kama kuna kulipia Huduma you n.a.
2 ili niweze kupata maelekezo zaidi
Namba yangu ni +255 655 570 084
Asante sana kwa somo la maelekezo mazur kuhusu kilimo cha zao hili umenifunza kitu kikubwa sana hasa kwa mm ambaye ndo nataka nianze kilimo icho
Karibu tujifunze pamoja.
Asante sana kwa elim zur VP mkoa Wa Ruvuma matikiti yanaweza kustaw
Ndio, yanastawi
Nimefaidika sana na elimu ya kilimocha tikiti maji……
Karibu sana
Nimejipanga kupiga pesa tu
Nashukuru kwa somo hili. Naomba number yako tafadhali
Wadudu hujawataja
Kwenye maboresho yajayo tutaweka!
+255 655 570 084
Napimaje ardhi ili kujuwa rutuba kama ina fahaa kwa hicho kilimo cha matikiti..!!? je naweza ku chota udogo wa eneo la shamba nakwenda wanako uza pembejeo na mbegu za mimea wana weza kupima pia..? au sehemu stahiki ni ipi..ili nijirizishe na eneo stahiki..!!?
Lengo la kupima udongo laweza kuwa kujua pH ya udongo au kiwango cha virutubisho kwenye udongo wako. Na hii inafanywa na wataalam (kuandaa sampuli ya udongo shambani, na kisha) kupima sampuli kwenye maabara ya kupima udongo au kwa vifaa maalum vya kupimia.
kwa mikoa ya Kanda ya ziwa zao hili linaweza kukua vizuri? hasa mkoa wa kagera na geita
Naam! Linaweza kumea vizuri tu
Asante kwa elimu nzuri ….ila kunauvumi unasema kuwa kuna mbegu na dawa feki za Tikiti maji sasa basi utajuaje kama hii ni mbegu /dawa halisi na sio feki ?
Njia nzuri ni kuangalia “lebo” ya uthibitisho kwenye paketi ya mbegu au kopo la dawa. Kwenye paketi ya mbegu bora kuwe na nembo ya TOSCI – hii ni taasisi rasmi ya kuthibitisha mbegu bora kabla ya kuuzwa kwa wakulima. Na makopo/paketi za dawa ziwe na nembo ya TPRI – taasisi rasmi ya utafiti wa viatilifu
Asante sana kwa elimu mm na hiyo program kuanzisha kilimo cha watermelon mwaka huu nitakuwa narudi kwako kupata ushaur itakavyo kuwa
Habari, mimi naomba kuuliza maana nimeshalima matikiti nimekula hasara Ile mbaya, maswal yangu ni 2,.lnasemekana unaweza kulima matikiti mara nne kwa mwaka je unaweza kuniambia ni miez ipi? Swal la pili, wanasema kwamba matikiti yakishakomaa kipindi cha mwisho kama wiki mbili au moja na nusu unayakatia maji ili yaweke sukari, na hili likoje? Naomba kuwasilisha
Pole kwa yaliyokufika.
Swali la kwanza: Ukitumia green house, unaweza bila shida. Lakini kwa shamba la wazi ni lazima uepuke maji ya mvua wakati wa maua, lkn pia uhakikishe hakuna maji ya kutuama na mwisho ujidhatiti kudhibiti wadudu na magonjwa ya fungus.
Kwa swali la pili: Jibu ni ndio. Ili kuongeza sukari, matitiki yanahitaji kipindi fulani cha ukame usio na madhara. Kukata maji wiki au mbili kabla ya kuvuna kunaweza kufaa.
Vijana wajiunge vikundi then wajichange hata kidogo waanze na eneo dogo nguvu zao zitumike kuhudumia shamba, baada ya mavuno mtaji Utaongeza ndipo waweze kuchukua eneo kubwa
Ushauri mzuri kwa vijana wenye nia ya dhati. Shukran
Keep it up br, najua utasaidia watanzania wengi kwa elimu hii ya bure. Mungu akusaidie pia
Amin. Shukran sana kwa kunitia moyo
Najihusisha na Kilimo
IKO VIZURI
Nitatizo gani husababisha tikiti maji kuwa na uwazi unapolibonyeza na wakati mwingine kupasuka sehemu ya nyuma/kwenye kitovu chake
Mie humu ni mgeni ninahitaji kujifunza kuhusu kilimo na ufugaji
Kwa majina yangu naitwa
MR.BERNARD MANOTA
Mr.mtalula Mohammed
Kwa upande wangu niseme asante saana kwa elimu yako , niseme2 kuwa mie nakupenda saana hikibkilimo cha matiki maji hapo niliwahi kulima na nikaambulia hasala lakini kuna mambo ambayo niliyabaini kutokana na kutokuwa na uzoefu, kwa sasa nimejipanga kuwekeza tena katika Kilimo hiki , nikiwa lini n kuongea na bwana mmoja akanishauli kutumia mbengu sina ya “JULIANA”
Naomba kuuliza
Je Juliana na baby sukal
Na African Queen
Kati ya hizi mbegu IPI ilivyo bora saaana kushinda zote hapo?
Pia nilikuwa nahitaji kupata kitabu cha mwongozo wa Kilimo hiki ,,,,na Kilimo cha vitunguu,,,,,,
Naoatikana pia kwa WhatsApp 0757 88 98 00
Au unaweza call 0657 88 84 29
Au kwa e-mail. [email protected]
Nataka mtu anayetokea maeneo wanakolima tikiti my no 0758507208
Nashukuru kwa maelezo mazuri nahitaji kujua zaia na kupata vitabu zaidi
Asanta kwa elimu…nimelima tikiki kuanzia mwezi wa sita kati kati kuna baadhi ya miche imesha toa matunda bt miche mingine ndo kwanza imetoa mauwa hivi sasa bcz nilipata changamoto ya maji kipindi cha upandaji. Je haita nipa shida katika kipindi cha kuvuna??
Hapana Johnson haiwezi kukupa shida. Matikiti huyavunwi yote kwa mara moja, yanavunwa kwa awamu kulingana na kukomaa kwake.
Thanks in advance the materia are well organised.
Asante sana kwa somo la maelekezo mazur kuhusu kilimo cha zao hili umenifunza kitu kikubwa sana hasa kwa mm ambaye ndo nataka nianze kilimo icho
Habari asante kwa taarifa nzuri, naomba kufahamu zaidi kuhusu kilimo hiki hasa upande wa masoko ya uhakika
Gwakisa kutokea Mbeya-Tanzania
Asante sana Mr. Mtalula masomo yako yananisaidia katika kazi zangu
Nimewapenda kwa maelekezo yenu asanteni sana
Asanteni kwa elimu hii
Asante kwa elimu hii
Nataka kujua jinsi ya kupanda tikitiki
Makala ziko poa
Matikiti kupasuka b4 kukomaa?
Chanzo na suluhisho ni nini?
Iv unaweza kulima matikiti heka 2 yakagoma kutoa mavuno mpaka mtaji ukakatika
Naweza kulima mbeya
Nimeelewa vizur Sana ndugu zanguni
Asante sana mr. mohammed nimeelewa na nitafanya kadri ya muongozo uliotoa. Lakini naomba kuuliza ni mara ngapi inatakiwa kumwagilia kwa siku tangu ninapokuwa nimepanda mmea.
kwa yeyote anaepatikana mkoa wa morogoro,ruvuma,mtwara na lindi na amefanya au anafanya kilimo hiki naomba tuwasiliane kwa simu 0758152710 au 0657152710.
Ahsante.
Nefurahishwa na kuvutiwa na elimu mnayoitoa kuhusu Kilimo hususan Kilimo Cha matikiti
Elimu nzuri sana
Nimepata Mambo mazuri nimejifunza vizuri kuhusu kilimo Cha tikiti maji napenda kuwashukulu Kwa Elimu yenu .
Nashukuru kwa somo zuri, naulizia idadi ya matikiti kwa ekari moja, pia swali jingine idadi gani ya matunda tuna paswa kuacha kwa kila mche mmoja. swali la mwisho, kwa ekari moja inatakiwa au inaweza kupandwa miche mingapi? asante
Napenda kutoa shukran zangu za dhati, kwan nimejifunza vitu vingi kuhusu kilimo bora cha matikiti na vilimo vingine mbalimbali.
Ilanaomba nipewe somo kuhusu shamba langu ni la slop na nahitaji lima tikiti., je nitumie mbinu gani.?
Asante sana nmejifunza mengi pia ila nataman kujifunza zaid na zaid
Tunao mwongozo wa kilimo cha tikiti maji ambao una mwongozo wa hatua kwa hatua za ulimaji na utunzaji wa tikiti, uchambuzi wa ghrama za uzalishaji katika kila hatua na makadirio ya faida utakayopata ktk mradi wako. Bofya hapa kuupata
kaka naomba mwongozo wa
kilimo Cha matikiti tuwasiliane nitalipia kama kuna galama my phone namba is 0788586369
Tunashukuru kwa Elimu nzuri mnayoitoa asanteni sana
Ahsante sana. Tafadhali usiache kushare makala hii
Napenda sana kilomo na nomefurahi Kwa elimu munayotoa
Ahsante sana, endelea kuwa pamoja nasi
kaka mm mgeni katika kazi hii tuseme mm mgeni nataka kujinasua Bariadi vip udongo wetu mweusi vp unafaaa kaka kilimo hiki Cha matikiti
Utafaa boss
Je unaweza kupandia mbolea ya samadhi, na je unaweza kupanda mbegu za kukamua mwenyewe?
Unaweza kupandia samadi. Mbegu ya kukamua mwenyewe unaweza kuitumia lkn isiwe chotara kwa kuwa haitakupa matokeo mazuri, kwa hiyo iwe ni mbegu ya tikiti ya kawaida, OPV.
Website hii ni msaada mkubwa kwa sisi wakulima wageni
Nahitaji zaidi kujifunza kuhusiana na kilimo na ufugaji
Endelea kusoma makala zilizopo na zingine zitakazokuja
nashukuru kwa elimu hii nzuri ya kilimo Cha matikti nitaifanyia Kaz na nitakuja na majibu baada ya kazi
Kila la heri na karibu tena
Naomba kupata soko la matikiti. Nimelima nategemea kuvuna December tarehe 27
Hakika hii elimu ni nzuri sana.
Smart
Asante sana endelea kutuelimisha
👌
Endeleeni kutupatia elimu husika hasa sisi ambao niwa changa kwenye sector hii ya kilimo
Naomba kupata elimu zaidi kuhusu kilimo, napenda sana. Pia kama Kuna vitabu naweza kupata Kwa ajiri ya kujifunza zaidi naomba kuvipata.
Jamani Kilimo cha tikitiki kwa ekari moja unanaweza tumia gharama ngapi hadi kuiva zao
Mahitaji kula tikiti maji hivyo naomba kufahamu soko na bei
Nahitaji kjjifunza zaidi kwenu kuhusu kilimo cha tikiti maana nimelima na kupanda bado hazijaota mbegu
Habari mimi nimdau mpya kwenye sekta ya kilimo napenda kuuliza swali kila mche mmoja wa tikiti uweza kutoa matunda mangapi
Mungu awatangulie mnatoa elimu nzuri,
Na pia ni fulsa kwa vijana na wapenda maendeleo,ila tu hizo dawa kwakweli madukani hazipatikani sana japo zipo nyingine ambazo pia zinajitahidi kusaidia hasa wale nzi wanaotoboa na kuleta uozo wa ndani kwenye tunda hawa kwa mtu ambaye hawezi kununua Ile mitego.
Nimejifunza mashallah
natamani sana kulima kilimo cha matikiti maji niko gairo, ningependa kuunganishwa katika maeneo yanayonizunguka yanayoweza kuzalisha kwa wingi zao hili.