Ndugu mkulima, ili ufanye kilimo bora na cha kisasa cha mahindi, Mogriculture Tz inakuasa kuachana na matumizi ya mbegu za kienyeji, kwani mbegu za kienyeji zina mavuno madogo sana na zinachukua muda mrefu sana kukomaa na nyingi zinashambuliwa sana na magonjwa.
Habari ndugu msomaji wetu karibu tena katika mwendelezo wa makala zetu za mafunzo ya kilimo bora na ufugaji wa kisasa kila Jumatatu ya kila wiki. Leo tumekuandalia makala hii ya mbegu bora za mahindi hapa Tanzania. Katika makala hii utajifunza mbegu bora za mahindi zilizofanyiwa tafiti hivi karibuni na vituo vya utafiti wa mazao ya kilimo hapa Tanzania. Kwa kila mbegu ya mahindi utafahamu kituo cha utafiti kilichozalisha hiyo mbegu, mahali kilipo na sifa za mbegu husika zikiwemo: muda mpaka kukomaa, uzaaji na uvumilivu dhidi ya ukame na magonjwa. Kumbuka kuwa hizi ni miongoni mwa Mbegu bora zilizotangazwa na Kamati ya Taifa ya Mbegu Machi 2016. Ungana nami hadi mwisho, karibu….
![]() |
| Mbegu bora za mahindi |
- Aina hii ni mahindi chotara.
- Inastawi katika mwinuko wa mita 800 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.
- Inakomaa kati ya siku 105 hadi 148.
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5 kwa hekta.
- Inastahimili ugonjwa wa bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) hususan katika maeneo ya kanda ya kaskazini.
- Soma hapa: Kilimo bora na chakisasa cha mahindi
- Aina hii ni mahindi chotara.
- Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
- Inakomaa kwa wastani wa siku 106.
- Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
- Inakoboleka vizuri (good poundability).
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.8 kwa hekta.
- Inastahimili ukame.
- Aina hii ni mahindi chotara.
- Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
- Inakomaa kwa wastani wa siku 105.
- Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
- Inakoboleka vizuri (good poundability).
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.7 kwa hekta.
- Inastahimili ukame.
- Aina hii ni mahindi chotara.
- Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
- Inakomaa kwa wastani wa siku 101 hadi 111.
- Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu
- wa majani (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
- Inakoboleka vizuri (good poundability)
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.6 kwa hekta.
- Inastahimili ukame.
- Soma hapa: udongo na mahitaji ya mbolea kwenye kilimo cha mahindi
- Aina hii ni mahindi chotara.
- Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
- Inakomaa kwa wastani wa siku 102.
- Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
- Inakoboleka vizuri (good poundability).
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5.9 kwa hekta.
- Inastahimili ukame.
- Aina hii ni mahindi chotara.
- Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
- Inakomaa kwa wastani wa siku 104 hadi 112.
- Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
- Inakoboleka vizuri (good poundability).
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.4 kwa hekta.
- Inastahimili ukame.
- Aina hii ni mahindi chotara.
- Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
- Inakomaa kwa wastani wa siku 103.
- Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), Ukungu kijivu wa mahindi (grey Leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
- Inakoboleka vizuri (good poundability)
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.5 kwa hekta.
- Inastahimili ukame.
- Soma hapa: kilimo cha kisasa cha mpunga
![]() |
| Vituo vya utafiti wa mbegu bora za mahindi |
- Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV)
- Inastawi katika ukanda wa kati katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,500.
- Inakomaa kwa wastani wa siku 104 hadi 128.
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 4.5 kwa hekta.
- Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV)
- Inastawi katika ukanda wa kati katika mwinuko wa mita 600 hadi 1500.
- Inakomaa kwa wastani wa siku 103 hadi 129.
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5.4 kwa hekta.
- Aina hii ni mahindi chotara.
- Inastawi katika ukanda wa chini na kati katika mwinuko wa mita 400 hadi 1,500.
- Inakomaa kwa wastani wa siku 120 hadi 130.
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 7 kwa hekta.
- Inastahimili ugonjwa wa bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot), baka jani (leaf blight) na kutu ya majani (leaf rust).
- Inakoboleka vizuri (good poundability).
- Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV).
- Inastawi katika ukanda wa chini na kati katika mwinuko wa mita 0 hadi 1,600.
- Inakomaa kwa wastani wa siku 110 hadi 120.
- Inastahimili magonjwa ya bakajani wa mahindi (grey leaf spot), milia (maize streak virus) na ‘Turcicum blight’.
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 4.9 kwa hekta.
- Soma hapa: kilimo bora cha maharage
- Aina hii ni mahindi chotara.
- Inastawi katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.
- Inakomaa kwa muda wa siku 128.
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.9 kwa hekta.
- Inastahimili magonjwa ya majani wa ukungu kijivu wa mahindi (grey leaf spot) milia ya mahindi (maize streak virus).
- Aina hii ni mahindi chotara.
- Inastawi katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.
- Inakomaa kwa muda wa siku 134.
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 7.6 kwa hekta.
- Inastahimili magonjwa ya ukungu kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya mahindi (maize streak virus).
- Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV).
- Aina ya mahindi lishe yaliyo na kiwango kikubwa cha viini muhimu vya protini.
- Hustawi katika mwinuko wa mita 800-1,200 kutoka usawa wa bahari.
- Inakomaa mapema kwa wastani wa siku 99.
- Ina stahimili magonjwa ya bakajani kijivu wa mahindi(grey leaf spot)na milia ya mahindi ( maize streak virus).
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 4.3 kwa hekta.
- Inakoboleka kirahisi.
- Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV).
- Aina ya mahindi lishe yaliyo na kiwango kikubwa cha viini muhimu vya protini.
- Hustawi katika mwinuko wa mita 800-1,200 kutoka usawa wa bahari.
- Inakomaa kwa muda wa wastani wa siku 98.
- Ina ukinzani wa magonjwa ya bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya mahindi (maize streak virus).
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5.2 kwa hekta.
- Inakoboleka kirahisi.
- Soma hapa: kilimo bora cha nyanya
- Aina hii ni mahindi chotara.
- Hustawi katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.
- Inakomaa kwa muda wa siku 150 hadi siku 155.
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.1 kwa hekta.
- Inastahimili magonjwa wa bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya mahindi (maize streak virus).
- Aina hii ni mahindi chotara.
- Hustawi katika ukanda wa mwinuko wa mita 600 had 1,200 kutoka usawa wa bahari.
- Inakomaa katika siku 138.
- Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.8 kwa hekta.
- Inastahimili magonjwa ya bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya mahindi (maize streak virus).




Ahsante sana kwa makala inayoelimisha umma Wa watanzania!! Natambua umuhimu Wa makala hii kwani natarajia kuwa mkulima bora!
Endelea kuwa nasi Paulo!
Nashukuru sana kwa elimu nzuri mnayoendelea kutupatia! Natarajia kulima msimu ujao kwa kuzingatia ushauri wenu na nina ahidi kuleta mrejesho hapa baada ya mavuno
Shukrani sana. Endelea kuwa nasi Desdel
Ahsante sana kwa elimu hii ya aina za mbegu za mahindi
Endelea kuwa nasi
hongereni
Shukrani sana
asanteni jamani nime share kupitia mafunzo haya
Endelea kuwa nasi
Bei gan boss
Mbegu nzuri kwa ajiri ya mahindi ya kuchoma ni ipi?
Habari! Hizi mbegu() kwa dar es salaam, zinapatikana wapi?
Hatuuzi mbegu David. Jaribu kuzitafuta kwenye maduka ya pembejeo za kilimo.
Asante kutupa elimu nzr ya kilimo
Asante kwa kutupatia elimu ya kilimo
Asante sana kwa elimu bora ya kilimo
Mim niko Arusha meru naomba kujua nimbegu ipi nzuri kwa ardhi yenye miinuko na mawe mawe
Asante sana. Sikuwa najua kama kuna mbegu bora za mahindi ya kawaida. Ila nisaidie, ukisema HEKTA unamaanisha HEKARI au ndo HEKTA kwa maana ya hekari 2.47105 ambazo ni sawa na HEKTA 1
Mbegu bora za mahindi zipo aina nyingi sana. Hekta 1 = Ekari 2.5 (Approximately)
Naomba nipatiwe maelezo ya kina sababu nimelima hekari mbili za mahindi hadi sasa nimeona umuhimu wa kutumia kilimo cha kisasa kutokana kila mwaka kupata mazao machache nimeona nauchosha mwili pia kuiingizia hasara muda wangu ninao utumia katika jambo hilo
Nazidi kujifunza kutoka kwenu…..Mwanafunzi wa Kilimo toka Chuo cha Maendeleo ya Wananchi
Asanteni kwa machapisho yenu pamoja na ushauri ila naomba kujua tofauti kati ya hekta na hekari
Hamjazungumzia mbegu ya mahundi inayoitwa AMINIKA
Ya simanjiro
He inafaa AMINIKA wilaya ya cmanjiro namalulu?
Nazipataje mbegu zenu za mahindi
Nimefurahia elimu hii ya mbegu bora ya mahindi na aina za mbegu, ila swali au ushauri kuhusu miinuko toka usawa wa bahari kwa mkulima wa kawaida pengine si rahisi kujua mahali alipo ni muinuko kiasi gani toka usawa wa bahari na hivyo ni mbegu ipi inafaa kwa eneo hilo. Je haiwezekani mbali tu ya kuweka vipimo vya miinuko, mngeainisha pia labda maeneo katika nchi yetu hata labda kwa kanda labda ingesaidia pia mkulima kujua ni mbegu ipi inafaa eneo lake.
Naishi Fukayose, Bagamoyo. kwa maelezo ya aina za mbegu inaonyesha aina za 2. NATA K 8 na
5. WE4112 ndio zinafaa ukanda huu. Naweza kuzipataje?
Pia, kama una ushauri mwingine wa aina za mbegu za mahindi au mazao mengine yanayoweza kulimwa huku kwetu tafadhali tujuze.
Alfred Junior Kipoo
Mbegu ipi ya mahindi inayofaa kulimwa sehemu ya Bukobainayoimili mvua nyingi na ukame
Natafuta mbegu Aina ya advanta
Advanta ni kampuni inayozalisha mbegu boss, ina mbegu nyingi mbalimbali
Nipo dsr s saram tunanunuwa mbegu hazinasifa rebo fekiukipandahatakamanamborea mahindiyakuwanjano
Natamani nipate mawasiliano ya wanazalisha mbegu inayokomaa kwa siku 120 na kuendelea kuepuka mahindi kuoza nilipo Kuna mvua nyingi sana
Ahsante sana kwa makala yako na tumaini nitakuwa mkulima bora, kwa kuwa ndio mara yangu ya kwanza kulima kisasa zaid, pia takuwa pamoja nanyi kwa ushauri zaidi. shukrani
Mungu ni mwema hongera sana sana mm pia nahitaji kujifunza nasomea kilimo na mifugo lakini naomba pia nipate mwongozo kutoka kwenu mafunzo mbali mbali kuhusu swala Zima la kilimo
Asante kwa ufafanuzi mzuri, pia sisi wakulima tunatamani kujua mbegu zinazochanua mapema yaan zinachanuwa zikiwa fupi na ndefu. Pia ufafanuzi kama mbegu inastahimili sehemu za joto au baridi. Kwani mkitutolea kwa namna ya miinuko kwa mfano mita 300 hadi 1500 au 0 hadi mita 1800 wengi hatuelewi au hatukupitia madarasa ya juu kidogo. Ila ukisema mbegu hizi zinafaa ukanda wa joto au baridi tunaelewa haraka na kuwa washauri wa wengine, ni mtazamo wangu au wetu tulioko vijijini Mpanda-Katavi
Ahsante kwa maoni yako, tutayazingatia katika matoleo yajayo.