Mvua za Vuli zinazoendelea katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka zilianza mwezi Septemba, hususani katika maeneo machache ya Ukanda wa Ziwa Victoria na yale ya pwani ya Kaskazini. Mtawanyiko wa mvua hizi bado ni hafifu katika maeneo mengi.

Soma hapa: Mwelekeo wa mvua za vuli Septemba – Disemba 2018

Kwa upande wa Nyanda za Juu Kaskazini-mashariki, mvua bado hazijaanza. Hali hii imetokana na joto la bahari kuendelea kuwa juu ya wastani katika pwani ya nchi ya Somalia na kupelekea unyevunyevu kuwa hafifu katika nchi yetu, hususani katika maeneo ya pwani ya Kaskazini na yale ya Nyanda za Juu Kaskazini-mashariki.

Mvua katika maeneo ya Ukanda wa Ziwa Victoria zinatarajiwa kuendelea vizuri katika kipindi kilichobakia cha msimu. Katika maeneo ya pwani ya Kaskazini, mtawanyiko wa mvua unatarajiwa kuanza kuimarika katika wiki ya nne ya mwezi Oktoba na kuendelea vizuri katika mwezi Novemba, 2018.

utabiri-wa-mvua-za-vuli-2018
Utabiri wa mvua za vuli 2018

Kwa upande wa Nyanda za Juu Kaskazini-mashariki, mvua zinatarajiwa kuanza kuelekea mwishoni mwa mwezi Oktoba na kuimarika katika mwezi Novemba, 2018.

Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na mvua chache katika mwezi Disemba, 2018 katika maeneo mengi ya pwani ya Kaskazini na Nyanda za Juu Kaskazini-mashariki.

Soma hapa: Mvua za Msimu Novemba 2018 hadi Aprili 2019

Hivyo wakulima wanaendelea kushauriwa kufuatilia utabiri wa siku kumi (10) na kupata ushauri kwa Maafisa Ugani.


Makala Muhimu:


  Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Bofya kupata taarifa kamili

  0 0 vote
  Article Rating

  Mtalula Mohamed

  I like blogging. In order utilize my profession I chose to share, to blog, a few tips and tricks about farming and agriculture to anyone interested.

  Subscribe
  Notify of
  guest
  0 Comments
  Inline Feedbacks
  View all comments
  error: Content is protected !!
  0
  Would love your thoughts, please comment.x
  ()
  x

  Join Our Farming Community