Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua katika kipindi cha Oktoba hadi Disemba, 2018, ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbali mbali wanaohitaji taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao kama vile Kilimo na Usalama wa Chakula, Mifugo na 

Wanyamapori, Maliasili na Utalii, Uchukuzi na  Mawasiliano, Nishati na Maji, Mamlaka za Miji, Afya pamoja na Menejimenti za Maafa.


Makala muhimu:


Mvua za vuli, zinazonyesha kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba, ni mahususi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka (Ukanda wa Ziwa Viktoria, nyanda za juu kaskazini mashariki, Ukanda wa Pwani ya kaskazini na wilaya ya Kibondo). Mvua za Vuli 2018 zinatarajiwa kuanza mapema katikati ya mwezi Septemba na mwanzoni mwa Oktoba, 2018 katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua. Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani katika maeneo ya mkoa wa Kagera, Geita na wilaya ya Kibondo; mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki pamoja na maeneo ya mashariki na kusini mwa Ziwa Viktoria. Mvua za juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya pwani ya kaskazini.

Mwelekeo wa mvua katika msimu huu wa Oktoba hadi Disemba 2018
Mwelekeo wa mvua katika msimu huu wa Oktoba hadi
Disemba 2018

Kanda ya Ziwa Victoria: (Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga):
Mvua za vuli zinatarajiwa kuanza mapema, kati ya wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Septemba, 2018 katika maeneo ya mkoa wa Mara na kusambaa katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Geita na Kagera ifikapo wiki ya tatu ya mwezi Oktoba, 2018. Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga na Simiyu. Mvua za wastani na vipindi vya mvua za chini ya wastani zinatarajiwa katika mikoa ya Kagera, Geita na wilaya ya Kibondo. Mvua za msimu wa Vuli zinatarajiwa kuisha wiki ya nne ya mwezi Disemba, 2018 katika maeneo ya mikoa ya Mara na Simiyu, na kwa maeneo mengine ya ukanda wa Ziwa Viktoria mvua zinatarajiwa kuisha kati ya wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Januari, 2019.


Makala Muhimu:


Kiwango cha Wastani wa muda mrefu wa mvua za mwezi Oktoba hadi Disemba katika kipimo cha milimita za mvua
Kiwango cha Wastani wa muda mrefu wa mvua za vuli katika kipimo cha milimita za mvua

Ukanda wa Pwani ya Kaskazini: (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Pwani, Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro):
Mvua zinatarajiwa kuanza mapema wiki ya nne ya mwezi Septemba, 2018. Mvua za juu ya wastani hadi wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi. Vipindi vya ongezeko la mvua vinatarajiwa hususan katika ya miezi ya Oktoba na Novemba. Mvua za Vuli zinatarajiwa kuisha wiki ya tatu ya mwezi Disemba, 2018.

Nyanda za juu Kaskazini Mashariki: (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na
Manyara):
Mvua zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya pili ya mwezi Oktoba, 2018 na
zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi. Mvua hizi zinatarajiwa kuisha wiki ya pili ya mwezi Disemba, 2018.

Athari na Ushauri: Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Wanyamapori.
Katika kipindi cha msimu wa mvua za vuli (Oktoba hadi Disemba) 2018 hali ya unyevunyevu wa udongo na upatikanaji wa chakula cha samaki vinatarajiwa kuimarika katika maeneo mengi ya ukanda wa nyanda za juu kaskazini mashariki pamoja na pwani ya kaskazini.

Hata hivyo, mazao yasiyohitaji maji mengi yanaweza kuathiriwa na hali ya unyevunyevu wa kupitiliza na maji kutuama. Magonjwa ya wanyama na upotevu wa samaki kutokana na uharibifu wa miundombinu ya kufugia samaki vinaweza kujitokeza kutokana na mvua za juu ya wastani zinazotarajiwa katika maeneo hayo.

Upungufu wa unyevunyevu unaweza kujitokeza katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani. Hivyo, wakulima katika maeneo hayo wanashauriwa kupanda mazao yanayotumia muda mfupi kukomaa na yanayostahimili ukame.

Soma hapa baadhi ya mazao ujue mahitaji yake ya mvua ili ufanye maamuzi sahihi ya kilimo katika msimu huu wa vuli:

Malisho na upatikanaji wa maji kwa ajili ya mifugo na wanyama pori vinatarajiwa kuwa vya kuridhisha katika maeneo mengi yanayotarajiwa kupata mvua za juu ya wastani na wastani. Hata hivyo upungufu wa maji kwa ajili ya mifugo na wanyamapori, ufugaji samaki, kupungua kwa samaki katika maji ya asili kutokana na kupungua kwa chakula cha samaki unaweza kujitokeza katika maeneo machache ya magharibi mwa Ziwa Viktoria. Teknolojia ya uvunaji maji ya mvua iimarishwe ili kukidhi mahitaji ya maji katika kipindi cha ukavu.


Makala zingine za Hali ya Hewa:

Pamoja na ushauri huu watumiaji wa taarifa za hali ya hewa wanashauriwa kupata ushauri zaidi kutoka kwa wataalam wa sekta husika ikiwemo maafisa ugani. Taarifa kamili inapatikana hapa


Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

0 0 vote
Article Rating

Mtalula Mohamed

I like blogging. In order utilize my profession I chose to share, to blog, a few tips and tricks about farming and agriculture to anyone interested.

Subscribe
Notify of
guest
8 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
James
James
1 year ago

Naomba maarifa kuhusu kilimo cha mboga mboga maeneo ya kimara

Salum Mangosongo
Salum Mangosongo
1 year ago

Asante sana kwa taarifa

Salum Mangosongo
Salum Mangosongo
1 year ago

Samahan una makala ya Kilimo cha pamba ?? Katika hatua ya maandalizi kupnda kupalikia magonjwa na wadudu na dawa had I kuvuna!!

Odilo Gaspar Killenga
Odilo Gaspar Killenga
1 year ago

Kilimo gani cha mboga mgoga na jamii ya mikunde kinachofaa kwa maeneo ya Himo Makuyuni katika mkoa wa Kilimanjaro?.

error: Content is protected !!
8
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x

Join Our Farming Community