Mbolea vunde [Mboji]: Jinsi ya kutengeneza, matumizi na faida zake
Mbolea vunde [mboji] ni aina ya mbolea ya asili yenye rangi nyeusi na harufu nzuri ya kidongo ambayo hutokana na kuoza kwa mchanganyiko wa masalia ya mimea kunakosababishwa na vijidudu na wadudu rafiki wa mazao. Hii inaweza kutengenezwa kwa urahisi sana nyumbani.
