IIi uweze kudhibiti magonjwa ya kuku yanayotokea katika kundi lako unahitaji kufahamu dalili za jumla za magonjwa hayo. Unapoigundua moja au zaidi ya dalili za ugonjwa au wadudu chukua hatua mara moja.
Magonjwa ya kuku yapo mengi. Hata hivyo siyo yote yanatokea mara kwa mara hapa Tanzania. IIi uweze kudhibiti yale yanayotokea katika kundi lako unahitaji kufahamu dalili za jumla za magonjwa hayo. Unapoigundua moja au zaidi ya dalili za ugonjwa au wadudu chukua hatua mara moja.
Yapo magonjwa ambayo yanaweza kuangamiza kundi lote la kuku katika muda mfupi. Jihadhari na uwezekano wa kupatwa na hasara zinazoletwa na magonjwa ambayo unaweza kuyazuia.
Dalili za Jumla za Magonjwa ya Kuku
- Kuku kupoteza hamu ya kula.
- Kuzubaa na kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu (Kutochangamka).
- Kushuka kwa kiwango cha utagaji wa mayai.
- Vifaranga kutokua upesi au kudumaa. – Macho kuwa na rangi nyekundu.
- Kujikunja shingo.
- Kutetemeka, kutoa majimaji puani, mdomoni na machoni.
- Kutoa mharo (kinyesi) wa rangi ya kijani au wenye mchanganyiko na damu au cheupe.
- Kukonda.
- Kukohoa.
Ukiona moja au zaidi ya dalili hizi katika kundi lako chukua hatua za kutibu zilizoelezwa hapa chini. Kama hali ni ngumu zaidi omba msaada kwa mtaalam wa tiba ya mifugo ili achunguze mara moja na kukushauri jambo la kufanya.
![]() |
| Kuku akichanjwa |
Hili ni jedwali linaloonesha ugonjwa, chanzo dalili na kinga au chanjo ya ugonjwa husika wa kuku
UGONJWA | CHANZO | DALILI | KINGA / CHANJO |
|---|---|---|---|
1. Kideri (NewCastle) | Virusi |
|
|
2. Kuhara damu (Coccidiosis) | Bakteria |
|
|
3. Ndui ya kuku (Fowl Pox) | Virusi |
|
|
4. Mafua ya kuku (Fowl Cryza) | Bakteria |
|
|
5. Kuharisha Nyeupe | Bakteria |
|
|
Njia kuu za ujumla za kudhibiti magonjwa ni:
- Kutunza hali ya usafi ndani ya banda na kudhiditi kusiwe na unyevu
- Matandazo yakichafuka yabadilishwe.
- Vyombo vya maji visafishwe kila siku
- Jitahidi uepuke kufuga kwa njia ya huria ili kuku wako wasiambukizwe magonjwa kirahisi
- Epuka kufuga kuku wako pamoja na bata na khanga.Hawa ni wabebaji wa vimelea vya magonjwa ya kuku japo wao hubaki salama
- Zingatia ratiba za chanjo kwa magonja yasiyo na tiba kama kideri na mengineyo ya virusi
Hayo ndo magonjwa ya kuku kwa ufupi lakini tumeakuandalia makala zingine zinazohusiana na ufugaji wa kuku, hizi hapa chini, bofya kuzisoma:


Nashukuru kwa elimu ya ufugaji,nahitaji Kuwa mfugaji wa kuku wa kienyeji naanzaje?