Ushauri Kilimo

Ushauri wa kitaalam kwa wakulima na wafugaji kuku makini

Huduma ya ushauri kilimo wa kitaalam ni kwa wakulima wa mazao na wafugaji wa kuku wanaotaka matokeo ya uhakika, sio majibu ya haraka ya kubahatisha. Tunatoa ushauri wa kitaalamu unaokuwezesha kuweka mipango sahihi ya uzalishaji, kutambua na kutatua matatizo shambani kwa usahihi, kutumia mbinu sahihi za uzalishaji, na kupunguza hasara na kuongeza faida.

Tunatoa huduma hii kwa njia zifuatazo… 

  1. Ushauri kwa simu au Whatsapp
  2. Kutembelea shambani na
  3. Kupitia vitabu (PDF) na miongozo ya kilimo biashara.

Je, huduma ya ushauri kilimo inakufaa?

Ushauri wa kitaalam utakufaa wewe ikiwa…

  • Unajiandaa au tayari umewekeza kwenye kilimo.
  • Unataka kufanya kilimo kama biashara, sio majaribio.
  • Uko tayari kulipia na kufuata utaratibu wa ushauri wa kitaalamu.

Huduma hii haitakufaa kama…

  • Unataka majibu ya haraka bila kujali usahihi wake. 
  • Hutaki kufuata maelekezo ya kitaalam.
  • Hutaki kulipia na kuwekeza kwenye utaalam wa kukuwezesha kufanikiwa.

Fanya booking sasa tuanze kazi

Ili tukuhudumie kwa ufanisi, huduma ya ushauri wa kitaalam ni ya kulipia. Kama uko tayari kuendelea, tafadhali jaza fomu hapa chini. Taarifa zako zitapitiwa, kisha utapokea utaratibu na gharama za huduma. Baada ya malipo kuthibitishwa tutaanza kazi mara moja.

Customer's Name

Physical Address​

Malolo, Kilosa (Shop)
Kihonda, Morogoro (Consultation)

Contacts

Email: [email protected]
Mobile: +255 655 570 084