Unataka kufanya kilimo kuwa biashara yenye faida?

Tunasaidia wakulima na wafugaji wa kuku kufanya maamuzi sahihi kupitia ushauri wa kitaalam na miongozo ya vitendo inayolenga kuongeza uzalishaji, kupunguza hasara, na kuboresha faida ya kilimo chako.

Ushauri Kilimo

Tunatoa ushauri wa kitaalamu kwa wakulima wa mazao na wafugaji wa kuku wanaotaka kufanya kilimo kama biashara yenye faida, sio kubahatisha. 

Tunakusaidia wakulima …

  • Kutambua kwa usahihi magonjwa ya mazao na kuku

  • Kupanga ratiba sahihi ya mbolea, viuatilifu na uzalishaji

  • Kuepuka hasara zinazotokana na maamuzi ya kubahatisha

  • Kuongeza mavuno na faida kwa njia za kitaalamu

  • Kuandaa mipango ya biashara ya kilimo au ufugaji wa kuku.

Huduma hii inakufaa ikiwa unalima au unajiandaa kuwekeza kwenye kilimo, unataka kilimo kiwe biashara, sio majaribio, na uko tayari kulipia ushauri wa kitaalamu na kufuata maelekezo.

Bwanashamba-na-mkulima-wakishauriana-kwenye-shamba-la-maharage

Wataalam wazoefu

Utashauriwa na wataalam wabobezi katika kilimo, na sio watu tu. Wataalam wetu wana ujuzi na uzoefu wakutosha kwenye sekta ya kilimo. Hivyo, upo kwenye mikono salama.

Pembejeo bora

Tunazo pembejeo zilizothibitishwa na zenye ubora wa kuamika. Tutakupa mbegu bora za mazao, mbolea safi na viuatilifu vyenye ubora.

Weledi na Uadilifu

Weledi na Uadilifu ni nguzo muhimu katika utoaji wa huduma zetu. Tegemea kuhudumiwa kwa weledi na wakati wote huo amana yako itakuwa kwenye mikono salama.

Mwongozo-wa-kilimo-cha-nyanya

Vitabu vya Kilimo Biashara

Je, umechoka kulima kwa mazoea na kupata hasara?

Tumekuandalia miongozo ya kilimo biashara kwa mfumo wa PDF. Vitabu hivi vina mbinu za kitaalam zitakazokuwezesha kujifunza na kufanikiwa kwenye kilimo, kuanzia kuandaa shamba, kuchagua mbegu bora, kupanda, utunzaji wa shamba hadi kuvuna. Bila kusahau, uchambuzi kamili wa bajeti ya kilimo (gharama za uzalishaji katika kila hatua), pamoja na makadirio ya faida utakayopata.

Fanya maamuzi sahihi leo, wekeza kwenye maarifa ili uwekeze pesa yako kwenye mradi unaoujua vizuri.

Shuhuda za wateja wetu

Miongozo yenu imenibariki sana!

Kwa kweli vitabu vinajieleza bayana sana kiasi kwamba hata mimi ambae sina uzoefu sana naweza tekeleza vyema miongozo ya vitabu. Nimeweza kujifunza njia bora za kilimo, awali sikujua kwanini napata mavuno hafifu lakini nimegundua ni kwa sababu sikuwa na elimu ya kilimo hasa kwenye kukabiliana na wadudu na magonjwa. Vitabu vya kilimo cha mahindi na nyanya vimenibariki sana.
Willy Mtae
Mkulima - Kinondoni, Dar

Vitabu vinaeleweka. Nimejifunza mengi!

Maelezo yanaeleweka, yametumia lugha rahisi kwa mkulima wa kawaida kuelewa. Niko naendelea kuvisoma na kutumia elimu nilioipata katika kilimo cha mazao niliopanda msimu huu. Nimegundua kuna baadhi ya hatua nilikuwa nakosea hivyo msimu ujao nitarekebisha hususani katika upandaji na uwekaji wa mbolea za kupandia.
Peter Shilogile
Daktari - Mbogwe, Geita

Punguzo la 17% kwa kila kitabu

Chagua kitabu chochote na upate punguzo la 17% sasa hivi. Bofya link hapa chini kupata offer hii …

Je, wewe ni mkulima?

Ungana nasi, tujifunze na kubadilishana mbinu za mafanikio kwenye kilimo