Salaam,
Mtalula Mohamed hapa
Mwanzilishi na Msimamizi mwendeshaji wa Mogriculture.com
Nina shahada ya Sayansi ya Kilimo kutoka SUA.
Nilianzisha mtandao huu mwaka 2016 kwa lengo la kutatua kero za wakulima kama wewe.
Nimekuwa kwenye sekta ya kilimo tangu nilipomaliza elimu ya juu, kama mtaalamu wa kilimo (Mtibwa Sugar Estates ltd – mpaka sasa) na mkulima vile vile.
Shughuri yetu kubwa ni kuwashauri wakulima kufanya kilimo chenye tija. Na tunafanikisha hili kwa kuandika miongozo ya kilimo biashara na vitabu vya kilimo bora, pamoja na kuandika makala mbalimbali za kuelimisha juu ya kilimo bora na cha kibiashara.
Ukiwa kama mkulima tutakusaidia kuongeza uzalishaji wa mazao yako kwa kutumia ushauri wetu wa kitaalamu na miongozo yetu ya kilimo biashara.
Professionalism: Kilimo ni taaluma yetu na tuna uzoefu nayo.
Transparency: Tutashauriana na wewe katika kila hatua, hakuna siri.
Honesty: Uaminifu ni asili yetu na msingi wa kazi yetu, amana yako iko kwenye mikono salama.
Tunapatikana Morogoro (Turiani). Kwa sasa hatuna physical office, tunafanyia kazi mtandaoni.
Copyright 2020 © Mogriculture.com. All Rights Reserved