Dondoo Muhimu za Mvua za Vuli 2019

  • Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli kipindi cha Oktoba – Disemba 2019, ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na wanyamapori, n.k.
  • Utabiri huu ni mahsusi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka (Nyanda za juu kaskazini mashariki, Pwani ya kaskazini, Ukanda wa Ziwa Viktoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma).
  • Katika msimu wa mvua za vuli 2019, maeneo mengi ya nyanda za juu kaskazini mashariki pamoja na pwani ya kaskazini yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani. Aidha, mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Viktoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.
mvua za vuli 2019
Kielelezo kinachoonesha mgawanyiko wa mvua za vuli 2019

Makala muhimu;

Kanda ya Ziwa Viktoria: Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga

Maeneo machache ya mkoa wa Kagera mvua za nje ya msimu zinaendelea toka mwezi Agosti na zinatarajiwa kusambaa katika maeneo mengine ya ziwa Viktoria hadi kufikia wiki ya pili ya mwezi Oktoba, Hivyo kuungana na msimu wa mvua za Vuli. Mvua hizo zinatarajiwa kuendelea kusambaa katika mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Simiyu na Shinyanga katika wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Oktoba.

Kiwango cha mvua kinachotarajiwa katika msimu huu ni mvua za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya ukanda huo. Msimu wa mvua za Vuli katika maeneo haya unatarajiwa kuisha kati ya wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Januari, 2020.

Ukanda wa Pwani ya Kaskazini: Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, pwani Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Morogoro

Mvua za vuli katika maeneo haya zinatarajiwa kuanza katika wiki ya pili ya mwezi Oktoba ingawa mtawanyiko wake unatarajiwa kuwa hafifu. Vipindi virefu vya ukavu na mvua chache pia vinatarajiwa katika maeneo mengi ya ukanda wa pwani ya kaskazini.

Hata hivyo, mvua zinatarajiwa kunyesha katika kiwango cha wastani kuanzia wiki ya pili ya mwezi Novemba. Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuisha katika wiki ya nne ya mwezi Disemba.


Nyanda za juu Kaskazini Mashariki: Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara

Mvua za vuli katika maeneo ya Nyanda za juu Kaskazini Mashariki zinatarajiwa kuanza katika wiki ya nne ya mwezi Oktoba na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara. Mvua hizi zinatarajiwa kuisha katika wiki ya nne ya mwezi Disemba 2019.

Athari za Mvua za Vuli na Ushauri Kwa Kilimo na Usalama wa Chakula, Mifugo na Wanyamapori

Katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za vuli za wastani hadi chini ya wastani, upungufu wa unyevunyevu ardhini unatarajiwa kujitokeza. Upungufu wa malisho na maji kwa ajili ya mifugo pia unatarajiwa hivyo kusababisha uwezekano wa migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Wafugaji wanahamasishwa na kushauriwa kuvuna mifugo yao ikiwa bado katika hali nzuri. Wafugaji pia wanashauriwa kutunza mifugo yao kwa kuzingatia ushauri kutoka kwa maafisa ugani katika maeneo yao.

Sekta ya uvuvi, katika maeneo hayo, inaweza kuathiriwa kutokana na upungufu wa maji katika mabwawa ya samaki na hivyo wafugaji wanashauriwa kuimarisha miundombinu ya ufugaji wa samaki na kuzingatia matumizi sahihi ya maji.

Katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani, shughuli za kawaida za kilimo zinatarajiwa. Aidha, malisho na maji ya kutosha kwa ajili ya mifugo na wanyamapori vinatarajiwa.


Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Taarifa kamili hii hapa

0 0 vote
Article Rating

Mtalula Mohamed

I like blogging. In order utilize my profession I chose to share, to blog, a few tips and tricks about farming and agriculture to anyone interested.

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Leo Lyimo
Leo Lyimo
9 months ago

Asante kwa utabiri

Mtalula Mohamed
Mtalula Mohamed
Reply to  Leo Lyimo
9 months ago

Shukran endelea kuwa nasi

mahanda
mahanda
9 months ago

Utabiri huu,ni mzuri sana kwani unatuwezesha kupanga mambo yetu vizuri.
Asanteni sana kwa utabiri.

Mtalula Mohamed
Mtalula Mohamed
Reply to  mahanda
9 months ago

Kila la heri kwenye msimu huu wa vuli ndugu Mahanda

Juma pungu
Juma pungu
9 months ago

Asante sana

error: Content is protected !!
5
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x

Join Our Farming Community