Karibu Jukwaa la Mkulima

Share on facebook
Facebook
Share on twitter
Twitter
Share on linkedin
LinkedIn
Share on email
Email
Share on facebook
Share on twitter
Share on email
Share on whatsapp
Share on linkedin

Habari ndugu msomaji wa mtandao wa Mogriculture.com, ni matumaini yangu uko salama na unaendelea vyema na shughuri za ujenzi wa Taifa.

Karibu Jukwaa la Mkulima

Jukwaa la Mkulima” si maneno mageni kwako kama ulikuwa pamoja nasi tangu siku za mwanzo wakati tunaanza kuelimishana juu ya masuala haya ya kilimo.

Jukwaa la Mkulima ni nini? Jukwaa la Mkulima ni jukwaa (kama ilivyo JamiiForums) ambalo tumeliandaa kwa ajili ya mijadala, hoja, maswali na majibu baina ya wakulima, wafugaji, wataalamu wa kilimo na mifugo na wadau wengine wa kilimo na ufugaji.

Ndani ya Jukwaa la Mkulima kila mdau anaweza kuanzisha mada/hoja, na kuzijibu hoja za wengine. Pia, ukiwa jukwaani utaweza kuuliza na kujibu maswali na utaweza ku-subscribe kwenye mijadala mbalimbali unayoipenda na utatumiwa email kila zinapowekwa hoja za wadau.Sifa za kujiunga na Jukwaa la Mkulima

Kuna vigezo vya mtu kujiunga na Jukwaa la Mkulima? Mmmmh…. ndio vipo! Soma kwa makini hapa chini;

 • Ni lazima uwe na simu au computer inayoweza kuingia kwenye mtandao. Kama unaweza kusoma hapa, basi wewe umefuzu kigezo hiki, yeah!
 • Uwe na barua pepe (email address) unayoitumia mara kwa mara. Kama unatumia smartphone wewe ulishafuzu tayari, twende mbele!
 • Uwe mdau mkereketwa wa sekta ya kilimo na ufugaji. Kama unasoma makala hii, bila shaka wewe ni kereketwa haswa!
 • Uwe tayari kujiunga na Jukwaa la Mkulima. Usipojiunga utaweza kusoma mijadala tu, hutaweza kuchangia hoja zako.

Hivyo ndio vigezo wa mtu kuweza kujiunga na Jukwaa la Mkulima. Kama bado unasoma sentensi hii, basi wewe ni mdau wetu nambari moja. Na kilichobaki kwako ni kujiunga tu. Endelea kusoma…Jinsi ya kujiunga na Jukwaa la Mkulima

Fuatilia kwa umakini sana hatua zifuatazo ili uweze kujiunga na kuanza kutumia Jukwaa la Mkulima mara moja.

 • Bofya “Jukwaa la Mkulima” ili uingie jukwaani, kisha bofya “Register” ili uweze kuunda profile yako. Andika “username” yako na kisha email unayoitumia sasa hivi halafu bofya kwenye viboksi vitatu vinavyfuata chini yake. Na mwisho kabisa bofya “register”.
 • 1.1 click register menu jukwaa la mkulima
 • 2.2 registration page jukwaa la mkulima
 • Ukimaliza hatua ya kwanza hapo juu, utatumiwa email muda huo huo. Hivyo hakikisha umeweka email sahihi. Nenda kwenye email inbox yako kisha angalie email yenye “subject” [Jukwaa la Mkulima] kisha bofya ili ufuate maelekezo.
 • Kama hujaiona, nenda kwenye “spam box” halafu bofya “Report not spam” ili email zitakazo kujia wakati mwingine uzione kwa urahisi.
3.3 username msg jukwaa la mkulima
 • Ukibofya kwenye email uliyotumiwa kwenye hatua ya hapo juu, utafunguka ukurasa ambao utakutaka uweke password, halafu uirudie tena ili kuthibitisha. Hakikisha kuwa unaikumbuka password yako. Fanya hivyo kwa umakini na usahihi kisha bofya “Reset password”.
5.5. password rest jukwaa la mkulima
 • Baada ya kubofya “Reset Password”, utapewa ujumbe kuonyesha umefanikiwa kubadilisha password yako. Na muda huo huo utakuwa ume-login moja kwa moja na utaweza kuanzisha mada au kuchangia mada zilizopo.
6.6 password reset confirmatin jukwaa la mkulima

Mpaka hapa umeshajifunza namna ya kujiunga na Jukwaa la Mkulima, na unaweza kuanza kulitumia mara moja. Jukwaa hili bado jipya, na mada zilizopo ziliwekwa kwa ajili ya majaribio ili kuhakiksiha kuwa linafanya kazi sawasawa, hivyo utahitaji kuanzisha mada mbalimbali katika majukwaa kadha wa kadhalika yaliyoandaliwa kwa ajili yako.

Jinsi ya kuanzisha mada jukwaani

 • Kwanza kabisa hakikisha kuwa ume-register na ume-login.
 • Chagua Jukwaa unalotaka uanzishe mada ndani yake. Yapo majukwaa (Main forums) matatu: (1) Jukwaa la kilimo cha mazao, (2) la Ufugaji na (3) la Maswali na majibu. Ndani ya kila majukwaa haya, kuna majukwaa madogo madogo. Chagua jukwaa dogo linaloendana na mada yako kisha ubofye hapo.
 • Ukishabofya jukwaa dogo (sub-forum), utaona maelezo ya aina gani ya mada zinaweza kuwekwa hapo. Na utaona button imeandikwa “Add topic” au “Ask question” kulingana na jukwaa ulilochagua kwa mada yako. Bofya hiyo button.
 • Baada ya kubofya button, utakuja ukarasa wenye sehemu mbili za kuandika: ya kwanza (inayotosha sentensi moja tu) utaandika kichwa cha habari cha mada yako na sehemu ya pili utaandika maelezo yote kuhusu mada yako. Hakuna ukomo wa idadi ya maneno.
 • Baada ya hapo bofya “Add topic” au “Ask question” iliypo chini ya ukurasa uliojaza mada yako.
 • Yap! Tayari umeshaanzisha mada, utaarifiwa kwa email kila itakapo wekwa hoja kwenye mada yako.
 • Unaweza kupitia mada za wadau wengine ili ujifunze au kuchangia hoja. Pitia hatua kama hizi ili uweze ku-add reply kwenye mada za wadau wengine.
jukwaa la mkulima

Natumai nimeeleza kwa lugha rahisi na umenielewa vyema. Sasa ni wakati wako. Bofya viungo muhimu vifuatavyo:

 1. Ingia jukwaani
 2. Kama bado hujajiunga, Register hapa
 3. Kama umeshajiunga, Login hapa

Tafadhali weka comment yako hapa chini ikiwa utapata changamoto yoyote.

Share on facebook
Facebook
Share on twitter
Twitter
Share on linkedin
LinkedIn
Share on email
Email
Share on facebook
Share on twitter
Share on email
Share on whatsapp
Share on linkedin
MAKALA NILIZOKUCHAGULIA
COMMENTS
Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
2
0
Would love your thoughts, please comment.x

Sharing is caring...

Share on facebook
Facebook
Share on twitter
Twitter
Share on linkedin
LinkedIn
Share on email
Email
Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp

Join Our Farming Community