Kilimo bora cha Migomba / Ndizi – 1

Share on facebook
Facebook
Share on twitter
Twitter
Share on linkedin
LinkedIn
Share on email
Email
Share on facebook
Share on twitter
Share on email
Share on whatsapp
Share on linkedin

Asili ya migomba ni nchi za Malaysia na India ambazo ziko Kusini Mashariki mwa Asia. Migomba inayolimwa sasa imetokana na migomba ijulikanayo …

Utangulizi

Hapa Tanzania kilimo cha migomba kimekuwepo Kwa miaka mingi. Kilimo hiki ni maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika kama chakula kikuu kwa baadhi ya mikoa kama vile Kagera, Kilimanjarona Mbeya na hivyo kulifanya muhimu, kufuatia mazao ya mahindi, mpunga, mtama, muhogo,viazi na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharage. 

Zao la ndizi linaweza kuwa moja kati ya mazao ya biashara iwapo litazalishwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hilo, ikiwa ni pamoja na kupanda aina bora ya migomba inayozaa ndizi zinazotambulika katika masoko ya kimataifa.

Ndizi
Mkungu wa ndizi mchanga

Usipitwe na makala hizi muhimu:


Asili ya migomba

Asili ya migomba ni nchi za Malaysia na India ambazo ziko Kusini Mashariki mwa Asia. Migomba inayolimwa sasa imetokana na migomba ijulikanayo kama Musa balbisiana ambayo asili yake ni India, na Musa acuminata ambayo asili yake ni Malaysia. Kutoka Malaysia na India migomba ilifika Afrika Mashariki katika karne ya tano.


Aina za ndizi

Kuna aina nyigi sana za ndizi. Nchini Tanzania ndizi zinazozalishwa, zipo za aina nyingi ambazo hutofautiana kwa majina kutokana na eneo au mkoa unaozalisha. Hata hivyo zinaweza kugawanywa katika makundi mawili.

 1. Aina ambayo huliwa kwa kuzichoma, kukaanga au kupikwa zikichanganywa na vyakula vingine kama vile nyama.Aina za ndizi hizo ni pamoja na Mzuzu, Mshare, Matoke, Bokoboko na Mkono wa Tembo.
 2. Aina nyingine ni zile ambazo huliwa kama matunda, aina hizo ni kama vile Kisukari, Kimalindi, Mzungu na Mtwike.

Kuna aina nyingine za ndizi ambazo kwa sasa huzalishwa hapa nchini ambazo zina fahamika kwa ubora wake katika masoko ya ndizi ya kimataifa. Aina hizi ni pamoja na Williams, Grand Naine, Pazz, Jamaica, Gold Finger. Nyingine ni Uganda green, Embwailuma Giant na Chinese Cavendish.


Maeneo yanayolimwa migomba nchini

Nchini Tanzania mikoa inayoshughulika na kilimo cha migomba na kuzalisha zao la ndizi kwa wingi ni pamoja na Kagera, Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Manyara, Mara, Tanga, Morogoro, Kigoma, na Pwani.

Hata hivyo zao hili linaendelea kuenea katika mkoa mingine nchini ikiwa ni pamoja na Dar es salaam, Mwanza, Ruvuma, Shinyanga na Lindi. Pia Dodoma na Singida. Kilimo cha migomba kinaweza kufanyika katika kipindi chote cha mwaka kulingana na kiasi na mtawanyiko wa mvua hasa mabondeni au kwa umwagiliaji.


Matumizi ya Ndizi

Kilimo cha migomba kina faida nyingi, baadhi ya faida za migomba nazao la ndizi ni: –

 • Zao la chakula
 • Zao la Biashara
 • Kutengenezea pombe
 • Kulisha mifugo
 • Kutengenezea mbolea (mboji)
 • Matandazwa shambani (mulch)
 • Kutoa kivuli
 • Kutoa nyuzi
 • Kutengenezea vitu vya sanaa
 • Kamba
 • Kufungia vitu
 • Malighafi ya kutengeneza vyakula na vinywaji mbalimbali.
 • Dawa
 • Majani kama miamvuli, sahani, vikombe na kata
 • Kuezekea.

Ndizi kwa ajili ya chakula hutumika kwa kutengeneza vitu mbalimbali kama:-

 • Makangale (Banana figs)
 • Poda (Powder)
 • Chenge (chips)
 • Jeya (flakes),
 • Juisi,
 • Lahamu (jam)
 • Vinywaji baridi, kama soda
 • Mvinyo (Wine)
 • Pombe kali
 • Hamira 

Kilimo cha migomba kinaendelea hapa:

Je, wewe unalima migomba au unapenda kulima siku moja? Ulishawahi kukutana na changamoto yoyote katika kilimo cha migomba? Weka comment yako hapa chini.

Share on facebook
Facebook
Share on twitter
Twitter
Share on linkedin
LinkedIn
Share on email
Email
Share on facebook
Share on twitter
Share on email
Share on whatsapp
Share on linkedin
COMMENTS
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x

Sharing is caring...

Share on facebook
Facebook
Share on twitter
Twitter
Share on linkedin
LinkedIn
Share on email
Email
Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp

Join Our Farming Community